Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

jambazi huyo alikamatwa julai 27 mwaka huu Mkoani Morogoro alikokuwa amejificha kukwepa polisi na walipofika eneo la Kisongo jijini Arusha akiwa kwenye gari amefungwa pingu mkononi alijaribu kuruka kuwakimbia polisi.
πŸ™‰πŸ™ˆ
 
Huu ni uongo uliowazi kabisa..

Ni kama wale wafungwa waliouliwa mafia kwa kupigwa then baadhi ya Askari waliandika vivohivyo kwamba wameruka kwenye gari.

Na wengine wakaandika ukweli wa kilichotokea.
Nusu ya Askari wakaenda mahabusu na nusu wakabaki.

Hilo jambazi wameliua kwa makusudi na linastahiri hicho kifo.
 
Hamna kuundwa kamati wala chchte, tunajua hakuruka kwenye gari wala nn ila amepata anachostahili, Hakika kifo chake kilikua chauchungu mno.
Karma.

Ni kama alivyokuwa akimpiga mwenzake mapanga, kama angefikiria yeye angejisikiaje basi asingefanya hivyo.

Wakati mwingine ni vizuri kupigana na moto kwa moto ili haya majitu yenye roho mbaya yapungue.
 
KISONGO...... !!!!!!
 
Huyo marehemu anayeitwa jambazi ukute hakuwahi iba hata ufagio.

1. Nani anaweza prove kwamba alifungwa miaka 16 pale Kisongo kisha akatoroka ila akaendelea kuishi palepale Arusha
2. Kilichomfanya amuue askari kwa mapanga usiku kwa jirani yake aliyetakiwa kukamatwa ni nini. Hii kesi anayodaiwa kuvamia wala hakumuhusu
3. Huyo askari namna gani ameenda peke yake usiku kumkamata mtuhumiwa nyumbani kwake
4. Marehemu jambazi aliwezaje kuruka kwenye gari wakati yuko chini ya ulinzi na kafungwa pingu. Ina maana askari wetu ni wazembe kiasi hiki

Hii kesi bila hata kutumia akili ina ukakasi mwingi
 
Naomba wote tulio iamini hii taarifa kutoka Jeshi letu la polisi tukutane hapa!! Mimi naanza 100% hii taarifa ni ya kweli πŸ™„
hata Mimi mkuu naiamini hii taarifa Kama nilivyoamini Ile ya askari aliyepiga risasi juu ikakata Kona,ikajipinda na kwenda kumpiga Binti Akwilina!

Polisi wetu Wana weredi wa hali ya juu sana kuliko wale wa FBI!


Nadanganya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…