Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

Siku ilipotoka habari ya huyo askari kuuawa mimi nilisema hapa ni bora ajiue kabla hajakamatwa kwani akikamatwa atakufa kifo cha mateso sana. Inaonekana jamaa aliteswa polepole mpaka akafa.
alijua labda ataweza kujificha huku akiwa anachat na hawala yake, teknolojia imemkamatisha
 
Lakini yote hayo yanasimamia kwenye mauaji ya yule askari awe ameenda peke yake au na wenzake.

Shahidi aliyekuwapo kwenye tukio kamtambua huyu jambazi aliyefanya tukio.
 
Unajua tatizo kubwa la kuruhusu au kufurahia polisi kufanya mauaji kama haya ni kuwa itazoeleka na kuwa tabia. (au sahihi zaidi niseme imeshazoeleka na kuwa tabia) Na ikishakuwa tabia ni lazima siku moja atakuja kuuawa mtu/watu wasio na hatia. Hii ni kanuni na ni lazima itokee. Leo kweli wanaweza kuua jambazi la kweli kabisa (kama hilo lililouawa) lakini kesho kuna uwezakano wakaua mtu asiye na hatia kwa makosa au makusudi.
 
Mtuhumiwa anakufa bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria alafu watu wanashangilia.
Banana Republic
Mkuu shangaa na wewe. Halafu kesho hawa hawa unasikia wanalalamika kuna ndugu yao ameuawa na polisi kituoni. Huu ni utapiamlo wa akili
 
Wasio na hatia waliisha uwawa, lakini sio kweli askari wote ni waovu kiasi cha kuuwa kila mshukiwa wa ujambazi.

Mara nyingi ukiona jambazi anauwawa ujue hata askari waliisha choka nae, anakamatwa akifugwa muda mfupi yupo uraiani na akiendeleza matukio hayo hayo.

Hakuna haja ya kumkamata kila mara ni risasi tu ndo jawabu.
 
"Ukiuwa kwa upanga utaondoka kwa upanga"

IGP. Simon Sirro -
Kibiti
August 12 , 2017


Atawalaye kwa upanga , atakufa kwa upanga- biblia


Nafikiri kila mtu ameelewa sasa.[emoji41]
 
Ukiishaua huna utetezi mkuu.
 
Unajua kusoma kwa ufahamu? Nani kasema askari wote ni waovu kiasi cha kuua kila mshukiwa? Sasa kama unajua kuna wasio na hatia walishaua huoni ni vizuri watuhumiwa wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kufanya wale wasio na hatia wasiuawe?
 
Kumbe hawa jamaa wanaelewa uchungu wa kimpoteza mwenzao, na wale wa Akwilina na Mwangosi Mungu atawasimamia.
 
Polisi ni kazi ya heshima Duniani kote ila hapa Tz ni laana kutokana tu na matendo ya baadhi yao.
 
Mahakama zipo kwa ajili ya nini hasa kama watu wanaopaswa kusimamia sheria wanazivunja wazi wazi alafu mazuzu kama wewe mnashangilia
 
Enzi hizo bado niko huko kwenye hiyo taasisi ndio ilikuwa michezo yetu hiyo kwa wahalifu sugu...wengine tulikuwa tunawakamata wakiwa hai tunawapeleka msituni tunawapiga risasi then tunautangazia umma kuwa wameuwawa katika fierce gun battle.
 
Tumeelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…