Aliyetoa amri ya kubandua plate number za 3D akapimwe akili

Aliyetoa amri ya kubandua plate number za 3D akapimwe akili

Hili la kusema Mashine zao hazina uwezo wa kusoma 3d plate no Ni uongo mwepesi Sana , Ina maana ndani ya kipindi chote ambapo 3d zimekuwepo , gari zenye 3d zimekuwa hazikamatwi na torch zao ? Binafsi nilishakamatwa na hizo camera nikiwa nadaiwa na gari ilikuwa na 3d
 
Najua Police excuse yao kubwa ni namba hazisomwi na camera zao wanaotegesha zisome madeni etc.

Ila twende na technology, Police wanatakiwa wawe na magari ya patrol ambayo yapo equiped na ANPR cameras (Automatic Number Plate Recognition Cameras). Ambayo inafanya kazi kama zile camera zao wanazotegesha njiani zina detect magari yasio na bima, yenye madeni na yenye uharifu.
View attachment 2938807
Issue ya kuzingizia 3D numbers ñi kwasababu vifaa vyetu vipo outdated sana.

Baadhi ya Nchi zilioendelea wameweka 3D numbers kama premium option tu kwa magari, na wala haikatazwi.
View attachment 2938810
Naunga mkono hoja
 
Ukibandua tu inaondoka na rangi ya mwanzo inakuwa kama imefutika. Makampuni yenye tenda ya kutengeneza plate number itakuwa wamechoma utambi baada ya kuona ubunifu wao umepitwa na wakati na maa artist wa mitaani wanazibandika wanapata hela wakajisikia vibaya. Shame on them, wameshindwa nini kuboresha zao? Ni ushindani tu kati ya wenye tenda na wasio na tenda
 
Hutakiwi kubandua, unatakiwa kurudi kwenye macamuni yanayotoa hizo number, nenda na card yako ya gari na number ulizoziharibu, utalipia 30,000. Na kupewa number mpya zenue viwango, hizo ulizozibandua kisheria hazisomeki.
Hao wanaobandua kwa lazima barabarani kwa mtindo wa operesheni ni trafiki wenyewe. Kwahiyo kumbe hii ni biashara anatengenezewa mtu, si ndio?!
 
Ni ushamba uliopitiliza kubandika ma plastic mbele ya namba ambayo imeandikwa kitaalamu na madini yanayo reflect mwanga. Wewe kwa ulimbukeni wako unakuja kubandika makorokocho yanayofanya muundo wa herufi ubadilike. Ningekuwa Mimi ni serikali ilikuwa nikikukanata umejaribu plate number kwa kubandika hayo ma.plastik ni jela miezi 6 ili ukajifunze nidhamu. Jinga kabisa.
Sawa, nimeuliza, baada ya kubandua kwa lazima na kufuta namba za chini yake, camera ndio zinaweza kusoma?
 
Wakikuta namba zimefutika utatakiwa kununua mpya. Hizo namba za magari zipo kisheria. Na ndani ya sheria hakuna masuala ya 3D. Huwezi kuvunja sheria halafu unauliza maswali. Kama baada ya kutoa zimefutika kanunue plate number mpya.
Kwahiyo kumbe ni mtu anatengenezewa biashara kwa lazima sio?
 
Hili la kusema Mashine zao hazina uwezo wa kusoma 3d plate no Ni uongo mwepesi Sana , Ina maana ndani ya kipindi chote ambapo 3d zimekuwepo , gari zenye 3d zimekuwa hazikamatwi na torch zao ? Binafsi nilishakamatwa na hizo camera nikiwa nadaiwa na gari ilikuwa na 3d
Ndicho ninachosema, ni ulaji wanatengenezeana
 
Unatakiwa kuweka plate number mpya maana wakikuta plate number iliyochunika wanakamata gari yako
Wanapobandua na namba kufutika, ni kwanini wanakuachia uingie barabarani?

Kumbe ni biashara mtu anatengenezewa kwa kuumiza wananchi kikatili namna hii?!! Maana kampuni za kuprint plate ni hadi upewe tender na TRA, na wanapewna wenyewe..
 
Ndio maisha yetu kibongobongo . Huwa ni miradi ya wanaojulikana kwa ujumla kama vigogo. Ukianza kutafuta mmoja mmoja unaweza ishia kupoteza uhai wako au kupewa ulemavu wa kudumu ama kuikimbia nchi yako. Refer NIDA, kilimo kwanza (power tila) na mingine mingi
 
Polisi waweke camera zenye uwezo wa kusoma 3D license plate.
Camera huwa zinasoma plate number au zina detect spidi ya gari inayokuja mbele?
Embu tufafanulie wewe Zile plate number na mashine kuna mechanism gani kiasi cha kwamba ukiweka 3D hauwezi kusoma?
 
Wanapobandua na namba kufutika, ni kwanini wanakuachia uingie barabarani?

Kumbe ni biashara mtu anatengenezewa kwa kuumiza wananchi kikatili namna hii?!! Maana kampuni za kuprint plate ni hadi upewe tender na TRA, na wanapewna wenyewe..
Mkuu Francis,
Mimi ninafanya hii biashara ya vitu vya urembo wa magari.
Uhalisia watu wengi wanakuja ofisni ninawabandulia Na ninawatoza elf10.

Wengi hawapeleki kutengenza plate namba mpya, wanachofanya unapobandua zikatoka rangi, tunamwita fundi wale wanaochora wanawapakia rangi.

Kati ya 100% wanaonunua plate namba ni 2% ya watu wote ninaowabandulia.

Hili suala ni masilahi tu. Hakuna aliyeleta sababu mpaka sasa.
 
Camera huwa zinasoma plate number au zina detect spidi ya gari inayokuja mbele?
Embu tufafanulie wewe Zile plate number na mashine kuna mechanism gani kiasi cha kwamba ukiweka 3D hauwezi kusoma?
Kuna camera za aina mbili barabarani

1. Ya speed
2. Ya madeni.

Nijuavyo mimi hakuna shida yoyote kwenye kusoma Madeni hata kwenye speed. Nadhani ni suala la Maslahi.

Maana mimi kwa mtazamo wangu naona hizi za 3D zimekaa vizuri kimuoneka o kuliko hata hizo 2D zao
 
Back
Top Bottom