Aliyetoa amri ya kubandua plate number za 3D akapimwe akili

Camera huwa zinasoma plate number au zina detect spidi ya gari inayokuja mbele?
Embu tufafanulie wewe Zile plate number na mashine kuna mechanism gani kiasi cha kwamba ukiweka 3D hauwezi kusoma?

Zipo camera za kudetect speed(Dopler's effect) na zipo camera ya kuscan namba(Number detection on the license plate) ,kwa hapa tunazizungumzia hizo za kudetect number.

Kabla ya kuimplement kitu chochote lazima ufanye test ,inaonekana test walizozifanya kudetect namba walitumia vibao plane kwahiyo inaonekana hizo 3D zinawasumbua kudetect ,ndiyo maana nikashauri waboreshe camera zao ziwe zinauwezo pia kwa kudetect 3D.
 


Kwa nini wao waingie gharama?
 
Sasa namba zisizosomeka TRA wakizipitisha ndiyo zitasomeka?

 
Sawa, nimeuliza, baada ya kubandua kwa lazima na kufuta namba za chini yake, camera ndio zinaweza kusoma?
Wewe ndio umejaribu kwa makusudi kwa kubandika hayo ma plastic. Hivyo Cha kufanya kaombe wakupe mpya achana kabisa na hilo ambalo halisomeki tena paki gari nyumbani mpaka utakapopata namba sahihi. Usirudie tena ujinga wa kufuata mkumbo kuweka vitu kwenye gari visivyo na maana
 
Hoja ni kwamba, hizo 3D hata camera zao zinasoma, ni uongo kusema hazisomi, kwahiyo hapo wanatemgenezewa watu biashara
 
Hoja ni kwamba, hizo 3D hata camera zao zinasoma, ni uongo kusema hazisomi, kwahiyo hapo wanatemgenezewa watu biashara
Whether zinasoma au hazisomi, nipe sababu ya kitaalamu ya kuzibandika hayo ma plastic

Halafu uliwahi kufanya tafiti kati ya hizo namba zililochakachuliwa kwe kubandikwa hayo ma plastic na zile zilizoithinisha kwa kuzisoma ukiwa pembeni?
 
Hutakiwi kubandua, unatakiwa kurudi kwenye macamuni yanayotoa hizo number, nenda na card yako ya gari na number ulizoziharibu, utalipia 30,000. Na kupewa number mpya zenue viwango, hizo ulizozibandua kisheria hazisomeki.
walibandika 3D kutafutia sifa mtaani,sikuwahi kujua zina faida gani ukilinganisha na number za kawaida
 
kwani plate number za kawaida zinawekwa na seikali? sio kampuni binafisi?
 
Wajinga hawawezi kukuelewa mkuu wangu
 
Wakikuta namba zimefutika utatakiwa kununua mpya. Hizo namba za magari zipo kisheria. Na ndani ya sheria hakuna masuala ya 3D. Huwezi kuvunja sheria halafu unauliza maswali. Kama baada ya kutoa zimefutika kanunue plate number mpya.
Taifa lina watu wajinga sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…