Aliyewahi kuagiza Alibaba au anajua office zao zilipo kwa Dar

Mchawi ni hilo sanduku la Posta,
Au wewe wapokelea vipi mizigo yako
Fungua sanduku la Posta haizidi elf 45 tu,details za silent ocean China hizo hapo. Utampatia supplier wa alibaba ili apeleke Mzigo.
 

Attachments

  • Screenshot_2022-06-11-05-07-23.png
    57.2 KB · Views: 52
  • Screenshot_2022-06-11-05-06-24.png
    47.3 KB · Views: 52
Mkuu kuagiza mzigo si lazima kuwe na agent. Watu wanaagiza Amazon, Ebay, Alibaba, Aliexpress n.k. na wanapata mizigo. Mizigo inasafirishwa kwa njia mbalimbali zisizohitaji ofisi ya kampuni husika. Kunaweza kukawa na changamoto za hapa na pale za kusafirisha mizigo mikubwa, lakini kama waagiza mizigo mikubwa waweza watafuta Silent Ocean na GNM.
 
Mkuu nakushauri ufungue ofisi pahala endapo una exprience ya kutosha WEWE uwe guarantor kwa wateja kama "processing unit and guarantor of eBay, aliexpress and alibaba Tz Ltd, tuchaji dollar $5 tu wala ukiweza tamaa
 
Umenifungua akili, shukrani sanaaa,
eenh, Zipcode ni nini??
Naishi Dsm
 
Tumia aliexpress wana mazaga kibao bei chee nina mizigo yangu mitatu from Aliexpress naisubiri mmoja umeshafika bongo miwili bado

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
Naomba na Mimi nisaidiwe kuhusu mambo kadhaa, kwanza kutaka kufahamu ukishaagiza mzigo allexpress huwa wanaleta gharama zote za usafiri na bidhaa au zile gharama ni za bidhaa peke yake? ikiwa hakuna usafiri gharama ya usafiri utaijuaje?
pili ukiwa unataka bidhaa zaidi ya moja na ukataka kufanya bargaining na muuzaji utampataje pale kwenye website yao?
 
Jibu la swali lako la kwanza ni kwamba huwa wanaweka bidhaa na bei yake halafu kwa chini wanaweka gharama za usafiri kutokana na address uliyojaza kama ni free shipping basi hawatoweka hela bali utaona wameandika free shipping na Kwenye kulipia wataorodhesha gharama ya bidhaa na usafiri mfano saa ya mkononi inauzwa 10,000/= na usafiri 3000/=

Kwahyo utalipia jumla 13000/=


Na swali la pili Kwa Aliexpress ndio unaweza ukachat na supplier

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Niliwapata ila hawajibu message nikaachana nao,

Nawatumia Kikuu hawajawahi niangusha tatizo lao hawana bidhaa nyingi kama Aliexpress, basi nakerekaaaaa
Wagumu sana kujibu msg , kama mzigo sio mkubwa tumia aircargo kama Bashley, unique. Kama mzigo mkubwa tumia silent ocean au shamwaa , unachotakiwa ni kuwa text WhatsApp na kuomba adress yao china ambayo utampatia supplier wako atume mzigo wako kwenye hiyo adress mzigo ukifika bongo unapigiwa simu ufate. Bashley air cargo na silent ocean wana mfumo wa kutrack mzigo.. shamwaa ukiwatembelea ofisini kwao kama hauna supplier Wanakutafutia.
 
Ahsante sana mkuu vip Kodi yake bidhaa ikishafika huku? ukokotoaji wake upoje
 
Hahaha hawa jamaa customer service yao ziroo hasa kwa huyo boss wao anatukana wateja wake[emoji38]

Kutukanwa mbona kawaida tu,umesahau yule aliyekuwa DC iringa mjini alivyokuwa anatukana wananchi?[emoji28]
 
Vipi kuhusu bei ya usafiri na ushuru ni asilimia ngai
 
Hahaha hawa jamaa customer service yao ziroo hasa kwa huyo boss wao anatukana wateja wake😆
Vipi mizigo inawahi kufika ?, mimi huwa natumia Bashley aircargo mizigo inachukua mwezi mzima kufika
 
Vipi mizigo inawahi kufika ?, mimi huwa natumia Bashley aircargo mizigo inachukua mwezi mzima kufika
Ni mizigo ya aina gani hiyo ya kuchukua mwezi? Je ni meli au ndege?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…