Ka historia kadogo,,,
Huyu Kaburu alikuwa mpinzani toka Enzi za Nyerere akafukuzwa shule form 3 eti kosa alimtoboa Nyerere macho (picha )
Baada ya kuanzishwa vyama vingi alirudi toka USA akajiunga na upinzani, nakumbuka mwaka 1994 nilihudhuria mkutano wake wa hadhara na akanishawishi nikajiunga na chama chake. Alisababisha vijana wengi wa sekondari kule kigoma kuingia matatani kwa kuiga staili yake ya uvaaji na akawa katibu mkuu wa CDM halafu akasepa akaenda CCM. Toka wakati huo sikuwahi tena kusikiliza wanasiasa na nawapuuza hadi leo. RIP Kaburu