TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou, afariki dunia

TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou, afariki dunia

Kwa kadiri ya kumbukumbu zangu huyu ni miongoni mwa waasisi wa Usaliti nchini Tanzania , mwingine aliitwa James Mapalala .

Mungu amuweke anapostahili .
 
Pole kwa familia yake, mke na watoto.

Huyu ni mmoja wa wanamageuzi na wanasiasa wa kwanza wa upinzani kuwa mbunge. Vijana wa Kigoma mjini walupambana sana kwa ajili yake ili awe mbunge, waliumizwa kuhakikisha Dr. Kaburu anapata ubunge na akaupata. Awamu iliyofuata akabwagwa na mwishoe akapiga saluti na kurudi CCM. Kaburu akawa wa kwanza kabisa kuwasaliti wapinzani na kuanza kuwarushia madongo ya ajabu. Siasa kweli ni mchezo mchafu.

Vv
 
10d180ceb5f8bcd1bbc3693fc17afabd.jpg
Ahsante kwa kuweka picha
 
Siku anatia Mguu kigoma kwa mara kwanza palikuwa hapatoshi.

Alisaidia sana kuujenga upinzani kigoma ,

Baadae sijui alipatwa na nini Dr Amani.

R.I.P...Dr..
kama kile kilichompata Baba junior mume wa Mushumbusi balozi mteule wa Sweden, aka. the shoopkeeper
 
Nakumbuka huyu kabouru alikuja kigoma sec mwaka was elfu 2,wanafunz wengi walimpenda
 
Mbunge wa Kigoma mjini ni Mh.Zitto Kabwe na yupo hai akiendelea kutimiza majukumu yake,kusema "aliyekuwa" si sahihi,ilipaswa isomeke"aliyewahi kuwa".

By the way, Kifo cha mwanaCCM yeyote yule hakinihusu, siwezi kuuvika moyo wangu simanzi kwa kuomboleza vifo vya wauwaji,watesaji na watekaji,muda huo sina.

Mungu amlipe sawa sawa na matendo yake, Amen.

Mshikaji chonde chonde tusifike huko tuwasamehe wanaotukosea
 
Quinine huyu Mtu alishaondoka CDM na Kwenda CCM,akachaguliwa kuwa Mwenyekiti CCM (M) Kigoma. Hajawahi Kuondoka CCM hadi umauti umemkuta, kwa nini utambulisho wake utaje CDM au kick
 
Quinine huyu Mtu alishaondoka CDM na Kwenda CCM,akachaguliwa kuwa Mwenyekiti CCM (M) Kigoma. Hajawahi Kuondoka CCM hadi umauti umemkuta, kwa nini utambulisho wake utaje CDM au kick
 
Back
Top Bottom