TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou, afariki dunia

TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou, afariki dunia

Ni mbunge wa kwanza wa upinzani. Alitingisha serikali ya awamu ya pili ya Mwinyi.
 
Aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma mjini Dkt. Amani Walid Kabourou, ametangulia mbele ya haki.

Alikuwa kalazwa Hospitali ya Muhimbili. Mazishi yanafanyika Kigamboni Dar Es Salaam.

Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Ameni.

KWA UFUPI:

Marehemu alizaliwa 23 Mei, 1949.

Aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia CCM mnamo mwezi Septemba 2006 na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma mwezi Oktoba mwaka 2012.

Aliwahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki kuanzia 05 Juni, 2007 hadi 04 Juni, 2012

UPDATE.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi
c916615902a3bcbbc9f5074b892388c8.jpg
Hivii umeshindwa kusema ni mwana CCM
 
Jamaa zangu wa pande ile huwa hawaaminiki. Vigeugeu kwelikweli.

Akapokelewe anapostahili

Nini maana ya kusaliti?

Hivi ukabaki Upinzani na kuacha Yale mliokuwa mnayasimamia na kuja na Mapya si usaliti huo?

Kuacha Vita ya Ufisadi kwa kuwa tu mmekaribisha Mafisadi sio usaliti?
Kabourow alisaliti Upinzani kwa kurudi CCM
Kina Mbowe nao walisalti Upinzani kwa kuachana na Yale waliyokuwa wanayasimamia
 
Mbona umetanguliza wasifu wa "CHADEMA?"

Huyo kaaga dunia akiwa ccm,n.a. wasifu mzuri ni wa kumhusisha n.a. ccm !
Sema usipotaja Chadema" cv itapwaya au?
 
Quinine huyu Mtu alishaondoka CDM na Kwenda CCM,akachaguliwa kuwa Mwenyekiti CCM (M) Kigoma. Hajawahi Kuondoka CCM hadi umauti umemkuta, kwa nini utambulisho wake utaje CDM au kick
Tido Mhando akifikishwa Mahakamani kwenye Muendelezo wa kesi yake huwa hatuitaji Azam two huwa tunasema aliekuwa Mkurugenzi mtendaji wa TBC
 
imekuwa kama yule msabaha wa cuf, nilimuona zanzibar naona kama akili sio zake, nahisi wapemba walimpiga kipapai aisee, sio bure, manake alipotoka kigoma tu, hali yake ikambadilikia

Msabaha Huyu alikuwa Mbunge wa CUF huko kisiwani Zanzibar akajiuzulu na kuunga Mkono jitihada za Mh. Rais Benjamin Mkapa!

Sijui kwanini kwenye Utawala wa Joni na Benja Masuala ya kujivua vyeo na kurejea CCM kumuunga Mkono Rais yalikuwa kwa Wingi!
 
Mbunge wa Kigoma mjini ni Mh.Zitto Kabwe na yupo hai akiendelea kutimiza majukumu yake,kusema "aliyekuwa" si sahihi,ilipaswa isomeke"aliyewahi kuwa".

By the way, Kifo cha mwanaCCM yeyote yule hakinihusu, siwezi kuuvika moyo wangu simanzi kwa kuomboleza vifo vya wauwaji,watesaji na watekaji,muda huo sina.

Mungu amlipe sawa sawa na matendo yake, Amen.
Umemaliza vema.Si jukumu letu kuhukumu,Mungu amlipe sawa na matendo yake.Hakuna mpinzani aliyependwa kama yeye kigoma mjini . Kuhama kwake kwenda ccm kuliwavunja mno moyo wakazi wa kigoma mjini.Enzi zake katika CDM kuna ndoa zilifarakana kwa sababu yake..Siwezi kuwa mnafiki kwamba kifo chake kimenigusa.
 
Aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma mjini Dkt. Amani Walid Kabourou, ametangulia mbele ya haki.

Alikuwa kalazwa Hospitali ya Muhimbili. Mazishi yanafanyika Kigamboni Dar Es Salaam.

Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Ameni.

KWA UFUPI:

Marehemu alizaliwa 23 Mei, 1949.

Aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia CCM mnamo mwezi Septemba 2006 na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma mwezi Oktoba mwaka 2012.

Aliwahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki kuanzia 05 Juni, 2007 hadi 04 Juni, 2012

UPDATE.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi
c916615902a3bcbbc9f5074b892388c8.jpg
acha apumzike atavuna atavuna alichopanda
 
NIPO NASURBIRI KIROHO SAFI NA SJASABABISHA WATU KUUANA AU KUUA KAMA YEYE ALIYEDANGANYA WANANCHI KISA TUMBO

Watu kama ww ndo huwa mnatumiwa na watu kama mangekimambi muandamane halafu baadae mkishavunjwa vichwa mnabaki mnalialia tu wakati aliewahamasisha yupo salama kabisa anakula kuku kwa mrija.
 
Angalau nimeona kuwa Magufuli anakiri kuwa hata ukiwa Mbunge toka Chama cha Upinzani unakuwa na mchango kwa taifa. Nichachojiuliza ni kwamba, Magufuli anatambua huo mchango pale tu hawa wanasiasa wanapokufa? Wakiwa hai hapana, ni maadui wa taifa? Hypocrisy.
 
Back
Top Bottom