TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou, afariki dunia

TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou, afariki dunia

Nakumbuka wananchi wake walivyokuwa wana mbeba juuu kwa juuu
Pumzika kwa amani mzee
10d180ceb5f8bcd1bbc3693fc17afabd.jpg
 
R.I.P Daktari!

Huyu alisaidia sana kuifanya Kigoma kuwa ndio ngome kuu ya upinzani kupitia CHADEMA!
Siku anatia Mguu kigoma kwa mara kwanza palikuwa hapatoshi.

Alisaidia sana kuujenga upinzani kigoma ,

Baadae sijui alipatwa na nini Dr Amani.

R.I.P...Dr..
 
Ka historia kadogo,,,
Huyu Kaburu alikuwa mpinzani toka Enzi za Nyerere akafukuzwa shule form 3 eti kosa alimtoboa Nyerere macho (picha )
Baada ya kuanzishwa vyama vingi alirudi toka USA akajiunga na upinzani, nakumbuka mwaka 1994 nilihudhuria mkutano wake wa hadhara na akanishawishi nikajiunga na chama chake. Alisababisha vijana wengi wa sekondari kule kigoma kuingia matatani kwa kuiga staili yake ya uvaaji na akawa katibu mkuu wa CDM halafu akasepa akaenda CCM. Toka wakati huo sikuwahi tena kusikiliza wanasiasa na nawapuuza hadi leo. RIP Kaburu
Hiyo ndiyo hali halisi , ukishahamia CCM wanakutumia kwa muda tu kwa maslahi yao, alafu badae wanakutupa kule.

Subiri uone 2020 hawa wote waliohamia CCM kama utawasikia tena.
 
Siku anatia Mguu kigoma kwa mara kwanza palikuwa hapatoshi.

Alisaidia sana kuujenga upinzani kigoma ,

Baadae sijui alipatwa na nini Dr Amani.

R.I.P...Dr..
Alikuwa na mgogoro na mbowe,nakumbuka hata kampeni za 2005 mbowe alikuja kigoma lakini alifanya kampeni pekeake bila uwepo wa kabourou licha yakwamba alikuwa mbunge kigoma.
 
Aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma mjini Dkt. Amani Walid Kabourou, ametangulia mbele ya haki.

Alikuwa kalazwa Hospitali ya Muhimbili. Mazishi yanafanyika Kigamboni Dar Es Salaam.

Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Ameni.

KWA UFUPI:

Marehemu alizaliwa 23 Mei, 1949.

Aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia CCM mnamo mwezi Septemba 2006 na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma mwezi Oktoba mwaka 2012.

Aliwahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki kuanzia 05 Juni, 2007 hadi 04 Juni, 2012
Mazishi yapo kigamboni sehemu gani mkuu?Sipend kuto kumzika huyu Jiran yangu pale ujiji
 
Huyu ajamaa alivyo ufanyia upinzani, halafu akaja Nsanzungwako then Zitto hapo nikajikuta sina kabisa IMANI na mpinzani yeyote toka Kigoma; alivyo pokea David mzee wa EPA na yule mwingine alikuaga mbunge wa Kasuru basi nikapigia mstari kwamba WAHA sio though nimeolea huko but one of my shemeji anae penda siasa nilimwambia kuhusu hili na akasema hivi, "Shemeji uko sahihi"
 
Jamaa zangu wa pande ile huwa hawaaminiki. Vigeugeu kwelikweli.

Akapokelewe anapostahili
 
Siku anatia Mguu kigoma kwa mara kwanza palikuwa hapatoshi.

Alisaidia sana kuujenga upinzani kigoma ,

Baadae sijui alipatwa na nini Dr Amani.

R.I.P...Dr..
Sijui naye angesikilizwa labda angelisema kama ya Hizza Tambwe ili aondoke kwa amani!
Alale pema peponi
 
Back
Top Bottom