Ndg. J. MREMA, WAAMBIYE WANACHADEMA UKWELI JUU YA HALI YA CHAMA CHAO ILI UWE HURU.
Na;
Babu Stanley Otto Mayunga.
(0621014417).
Mapema wiki hii,Dkt. Vicent Mashinji aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA alitangaza kujiunga na CCM.Haraka sana na isivyo kawaida,Mkurugenzi wa mawasiliano,itikadi,uenezi na mambo ya nje wa CHADEMA Ndg. John Mrema akapiga chafya na kutoa kijitamko ili kurejesha matumaini,uvumilivu na faraja kwa wafuasi wao katika kipindi hiki kigumu kuwahi kuweweseka!!
Bila shaka njia sahihi ya kuchangia katika kauli za Mrema ilikuwa ni kukaa kimya kwani zoezi la wapinzani kuhamia CCM si tena habari muhimu (topical issue).Hata leo nikisikia Ndugu Anthony Komu (Mbunge) kasogea CCM nitasikitika tu kwa kuchelewa kwake kufanya maamuzi sahihi.Na muhimu ni kwamba kufa kwa CHADEMA hakuna faida kwa CCM hasa baada ya vyama vya upinzani kukosa agenda za msingi kulisaidia taifa kama chachu ya kuharakisha maendeleo.Lakini japo mambo mawili tu lazima niyaandikie chochote;
Mosi,kubadilika kwa sababu zinazotolewa na CHADEMA juu ya utitiri wa vigogo wao kujiunga na CCM.Walianza na njaa(kanunuliwa) wakaja alitumwa(usalama wa taifa) kisha ameahidiwa uongozi na sasa karudi alikotoka(kwao).Kubabaika huku kunaonyesha walipropagate kuficha ukweli kuliko kutafuta kiini cha tatizo.Wakasema aende tunao wengi kumbe walidharau mwiba mguu umeota tende.
Nampongeza sana Ndg. Mrema kwa kutambua madhara ya kitendo alichofanya Dkt. Mashinji mtu muhimu na mwenye siri nyeti za chama,Mrema alizinduka na kuwaadaa wafuasi wao kuwa hali ni shwari na hakuna pengo lolote,aluta kontinua,pipozi pawa.Tuendelee kupanua vidole na kudai tume huru ya uchaguzi "no hate no fear",teh teh teh!.
Ninachoshangaa ni kukurupuka
kwake kudhani anapuliza ngonjera kuzima hoja nzito za Dkt. badala yake kapuliza upupu kuwasha mjadala juu ya hatma ya upinzani nchini.
Si kwamba tu hoja za Dkt. hazikujibiwa bali sikumsikia kabisa Mrema akitaja walau moja ya sababu walizozoea kutoa japo ile ya karudi alikotoka(kwao) kwani wanatambua Dkt. hakuwahi kuwa mwanaCCM.Sababu kuwa Dkt. alikuwa anapanga safu ya wagombea wake ni jambo la kawaida mpaka ndani ya chama makini CCM.Makundi hujitokeza wakati wa uchaguzi kisha mshindi uungwa mkono kwa nguvu zote.
Nukuu za ndugu Mrema kwa ufupi;
(i) "Taarifa hazijatushitua kwani tulizitegemea".Ikiwa ndivyo basi Dkt. angevuliwa uanachama kabisa.Walishindwa kufanya hivyo kwa kutambua kuwa Dkt. anazijua siri zao nzito hasa mikakati ya hovyo ya kuihujumu Serikali,kuhatarisha usalama,kupoteza/kuteka watu na kuleta taharuki,kuichonganisha serikali na wananchi,kumdhihaki Rais n.k.Ikiwa taarifa hazikuwashitua wasinge kurupuka kutoa tamko.Sote tunajua umuhimu wa kusema chochote haraka kabla mambo hayajaharibika!!!
(ii) "Wana intelijensia nzuri".Intelijensia nzuri haisubiri matokeo.Inawafuatilia watu wake kutambua wenye maadili,uzalendo na misimamo thabiti kabla ya kuwapa uongozi.Intelijensia inayoishia kushuhudia makatibu wakuu watatu tena Madaktari A. Kaburu,W. Slaa na V. Mashinji wakiwapuuza labda iliondoka na mzee Bob Nyanga Makani.
Wanawapatia uongozi wa juu wale wanaotoka vyama vingine.Eti chama kiko salama na intelijensia nzuri!Hivi ndani ya CCM unaanzaje kuingia mpaka kamati kuu kijinga namna hiyo.Intelijensia makini ingeshauri wakome kuazima human capital badala yake waandae watu wao.
(iii) "Tunategemea wengine watafuata na mnyororo ni mrefu".Kwa nini wasiwataje na kuwafukuza mapema ili kuonyesha ukomavu badala ya kusubiri fedhea.Au ndiyo kujitekenya na kucheka wenyewe na uwezo mdogo wa kufanya maamuzi mazito.Watabaki nguvu ya umma wakigeuka ni vivuli na vumbi!.Yako wapi matumaini na jeuri ya ushindi wao japo majimbo matatu ya uchaguzi hapo Oktoba ikiwa ndiyo kwaanza chama kinasambaratika!!!Hawajaambiwa mikakati ya kuziba pengo la wanaokimbia.
(iv) "CCM ina mpango wa kununua wabunge na madiwani".Kwa kuwa bado hiki kisingizio kinapakwa rangi basi na wao wanunue kwani wanabajeti ya kutosha kutoka ruzuku ya chama na wadhamini ndani na nje ya Tanzania.
(v) "Dkt. Mashinji ndiye katibu akiyehudumu muda mfupi kuliko wote".Bado Mrema ameshindwa kujibu hoja nzito alizozitoa Dkt.Ikiwa zaidi ya miaka mitatu kwa katibu mkuu na mtendaji wa chama kukijua chama na mikakati yake ni muda mfupi basi nakubali lakini alikuwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Slaa na haukuwa muda wa uchaguzi ndani ya chama.Walipoona hakubaliani na style ya uendeshaji wa chama kihuni,wakamsulubu.
Labda kama nimesahau lakini nakumbuka mzee Lowasa alijiunga na CHADEMA na muda mfupi akaaminiwa na kugombea urais!!Impact yake ikaonekana kiasi cha kujisifu kuvuna wanachama wengi!!?Sembuse katibu mkuu aliyekaa miaka zaidi ya mitatu aaaaah,tuwe serious kidogo.
(vi) "Kupambana kudai tume huru ya uchaguzi".Hapa naona nisipoteze muda wangu bure kwani ni agenda ya kuficha aibu ya kukimbiwa na vigogo wao na pia kujiandaa kuifanya kichaka baada ya kipigo cha mbwa Koko hapo Oktoba,2020.Sote tunajua hiyo ni hoja ya kujitafutia nafasi za kisiasa na kujitutumua kupandisha hadhi.Watanzani tunahitaji maendeleo kama haya tunayo yashuhudia chini ya Rais Dkt. Magufuli,J.P.J.
Pili,nimemkumbuka aliyekuwa waziri wa habari wa Iraq wakati wa uvamizi wa Amerika wakimshutumu Saddam Hussein kumiliki silaha za maangamizi.Tarehe 24 Machi,2003 mbele ya luninga alijitokeza waziri Mohammed Saeed al-Sahaf (Baghdad Bob) akasema:
"Natabiri kushindwa vibaya kwa Amerika na Baghdad iko salama.Mmarekani yeyote atakaye ingia Baghdad hatatoka salama.Tumechoramstari pale jangwani.yeyote atakayejaribu kuuvuka hatapata nafasi ya kusimulia kilichomkuta"
Wakati akitangaza hivyo,nyuma yake vilikuwa vikionekana vifaru vya Amerika na tayari waamerika walikuwa wameiangusha sanamu ya Saddam Hussein pale Baghdad!!
Wakati fulani Rais George W. Bush alisema, walituhumiwa kumkodi Mohammed na kumuweka pale asema maneno yale.Alipohojiwa waziri Mohammed Saeed alisema:
"My informations was correct,but my interpretations were not" bila shaka "taarifa zangu zilikuwa sahihi lakini tafsiri haikuwa sahihi"
Najua Ndg. Mrema kwa cheo chake ndani ya CHADEMA, alikuwa anatimiza wajibu wa kuwapa wafuasi wao matumaini mfu kama alivyofanya waziri Mohammed.Na najua kisiasa ni ngumu kukiri hadharani kuwa CHADEMA iko ICU.Kabla hawajapoteza muda juu ya tume ya uchaguzi ni bora kupitia vikao vyao vya ndani wajitathmini na kukiri shutuma za muda mrefu kuwa kinadharia (theoretically) CHADEMA ni chama cha siasa lakini kivitendo (practically) ni SACCOS ambayo yeyote anayejitokeza imendea nafasi ya msimamizi wa mikopo (credit supervisor) hunyooshwa vilivyo kiasi cha kuhatarisha uai wake.
Wasome alama za nyakati kama CCM tunavyofanya kila inapobidi kisha warekebishe mifumo yao inayopelekea ubadhilifu wa mali za chama na ukosefu wa demokrasia ndio warudi kujipima dhidi ya CCM.La sivyo siku yaja sote tutaimba CCM baba laoooo!!
Napenda sana kunukuu kauli ya Hayati Mwl. Nyerere,J.K.kuwa "upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM".CCM kuna utaratibu wa kujifungia ndani ya vikao rasmi na kila mjumbe kutoa maoni kinzani na mwenziye kwa uhuru na haki.Huu ndio upinzani alosema Kambarage.mwishowe makubaliano ufikiwa mlango ukafunguliwa na tunatoka letu likiwa moja.CHADEMA jifunzeni hili kwani bado tunahitaji muwepo kukidhi matakwa ya sheria ya vyama vingi tu.
Ndugu. J. Mrema,nafasi yako ni kubwa na muhimu sana katika kujenga taswira ya chama chako.Lakini kudanganya mchana kweupe ni kugumu zaidi.Usikubali kufa na tai shigoni kama 'Baghdad Bob'.Waambiye wanachadema ukweli kuhusu hali ya chama chao ili uwe huru na historia itakukumbuka INSHAALLAH.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).