Wakata viuno wa mayenu ni mbwa kabisa, kwanza wanasidiwa vita ambavyo wanatuingiza kutapeli lakini kibaya zaidi mkiwa battleground wakihongwa pesa wanawauza mnapigika kirahisi. Yaani wao pesa kwanza uzalendo sifuri, hawako tayari kupigana lakini wanatutapeli tuwapinie vita vyao. Tumepigania nchi nyingi sana na hatujafaidika chochote, we better change and start thinking the capitalist way of thinking yaani tuwe tunaingia vitani kwa maslahi ya kiuchumi tu na si vinginevyo.
Kuna mambo muhimu ume yaandika hapa, lakini mengine hayapo sahihi.
Kwa mfano: Ninakubaliana moja kwa moja na wewe kwamba hawa wakongomani hawastahili msaada wetu hadi hapo watakapokuwa tayari wao wenyewe kujitoa mhanga kwa nchi yao. Ni aibu sana kwa nchi tajiri, kubwa kama hii kudhalilishwa kiasi hiki, tena na ki-nchi kisichokuwa na lolote!
Wakongomani wakionyesha dhamira ya kweli ya kuipigania nchi yao, ni kwa manufaa yetu kabisa kuwapa msaada, hata wa kijeshi, kwa sababu nasi tunayo maslahi ya kibiashara nao. Utulivu wa Kongo ni faida kwetu katika shughuli zote za maendeleo.
Mfano mwingine, ambao pengine nina tafsiri tofauti kidogo na yako ni huo unaelezea wao "kutuingiza kitapeli" kwenye vita yao. Binafsi sidhani kuwa "tunaingizwa kitapeli" kwenye vita hiyo. Hii tunajiingiza sisi wenyewe (soma viongozi/watawala) wa nchi yetu ndio wanatuingiza humo kitapeli kwa kuingiza jeshi letu kwenye vita kwa minajiri ya kulipwa pesa (kulinda amani kwa malipo), bila kujali anayelipa ni Umoja wa Mataifa au nani. Jeshi letu linageuzwa kuwa kitega uchumi? Mbaya zaidi ni kuwapeleka vijana wetu kuwa wahanga wa vita hiyo, bila ya kuwapa maelekezo sahihi ya nini wafanye wanapolazimika kujihami. Ni lazima vijana wetu wanapo pelekwa kokote duniani, maelekezo yawe usalama wao kwanza kabla ya masharti mengine yoyote kutoka kwa hao wanaotuingiza kwenye biashara hiyo. Mpumbavu yeyote anaye thubutu kushambulia jeshi letu wakati likiwa kwenye ulinzi wa amani, ni lazima apewe fundisho, kwa maamuzi yetu wenyewe, siyo hayo ya Umoja wa Mataifa au mwingine yeyote.
Kagame na wapwa zake M23 katumia udhaifu wa matakwa ya Umoja wa Mataifa kuwadhalilisha na kuwaumiza na kuwaua vijana wetu. Hili lisiruhusiwe tena mahali pengine popote.
Mfano wa tatu, nisiokubaliana na wewe moja kwa moja:
Tumepigania nchi nyingi sana na hatujafaidika chochote, we better change and start thinking the capitalist way of thinking yaani tuwe tunaingia vitani kwa maslahi ya kiuchumi tu na si vinginevyo.
I am very proud of what Tanzania was able to do during the liberation struggle. We cannot now seek to turn our defence forces into a mercenary force for hire.
The primary objective for our force is for the defence of our mother nation and its people.