Aliyeweka video ya mwanajeshi akisachiwa kwenye mitandao kwani anatuma ujumbe gani?

Aliyeweka video ya mwanajeshi akisachiwa kwenye mitandao kwani anatuma ujumbe gani?

Wewe mtu wa hovyo sana unajuaje kama kila mtu ameiona hiyo video,shush video kusapoti mada
 
Sasa kama jirani mwenyewe nae hata ‘adder’ nyoka ambae hana sumu kuua; kumsogelea hawezi. Wakati adder unaweza kumkamata hata kwa mkono tu, huyo wa kwenda kumsaidia kweli.

Rwanda aina ubavu wa kupambana na Tanzania strategically kijiografia, uwezo wa kivita na size of the army.

Mengine ni upuuzi tu wa wanyarwanda wa JF kujitekenya na kucheka wenyewe.
Rwanda siyo ya kubeza kijeshi, Kama ilivyo kawaida ya madikteta wengi, Kagame ameimarisha sana jeshi,

Alivyokuwa anamwambia raisi wa Afrika kusini kwamba jeshi lake siyo militia, it is an army alikuwa anamaanisha.

Jeshi la Rwanda liko well trained and well armed, linatoka kwny historia ya RPF msituni kabla ya genocide, ambapo lilisifika kwa nidhamu.

Sisi tunaweza kuwashinda lakini siyo kirahisi, ukubwa wa jeshi(wingi wa wanajeshi)huwa hausaidii sana.

Inasemekana Kagame kapeleka wanajeshi 4000 tu DRC, lakini jeshi la Congo limepoteana.
 
Mimi mwenyewe nimeshangaa Tanzania tunashikwaje makalio namna ile 😭😭😭😭

Jeshi letu hii kitu wekeni kumbukumbu siku moja tutamfunza mtu adabu
 
Yani kumrekodi mwanajeshi akisachiwa na askari polisi na kupost ndiyo kuonyesha kuwa nyinyi si lolote? Nadhani wanamaanisha hivyo.

Kumrekodi askari akipigwa sachi kiasi kile kisha kutuma kwenye mitandao ni moja ya uchokozi kati ya nchi na nchi.

Poleni mnaoona ni jambo la kawaida kurekodiwa kule na kuwekwa hadharani mitandaoni.
Mtoto mkorofi akitaka kupigwa huanza vurugu, na kujifanya mwehu haambiliki anarusha vitu, anatupa mawe nk. Ipo siku huyu mwehu Kagame, atapigiwa tu, Mizengo Pinda aliwahi kusema Bungeni, mtu mkorofi, apigwe tu. Nyerere aliwahi kusema kwa Idi Amin, sababu, nia na uwezo wa kumpiga tunao. Na atapigiwa tu.
 
Rwanda siyo ya kubeza kijeshi, Kama ilivyo kawaida ya madikteta wengi, Kagame ameimarisha sana jeshi,

Alivyokuwa anamwambia raisi wa Afrika kusini kwamba jeshi lake siyo militia, it is an army alikuwa anamaanisha.

Jeshi la Rwanda liko well trained and well armed, linatoka kwny historia ya RPF msituni kabla ya genocide, ambapo lilisifika kwa nidhamu.

Sisi tunaweza kuwashinda lakini siyo kirahisi, ukubwa wa jeshi(wingi wa wanajeshi)huwa hausaidii sana.

Inasemekana Kagame kapeleka wanajeshi 4000 tu DRC, lakini jeshi la Congo limepoteana.
Kabla ya hata kupeleka wanajeshi tuna-chock uchumi wao kwa kukata supply ya mafuta na chakula (heavily dependant kutoka Tanzania).

Baada ya mwezi njaa Rwanda na uchumi unachechemea; halafu ndio tunapeleka kichapo.

Rwanda hana ubavu wa kusimama na Tanzania hadithi tu.
 
Jw ya sasa haina uwezo wa kumpiga Rwanda,dead walking army iliojaza mapandikizi ya UCCM na Machawa kwa mgongo wa koneksheni
Kwanini tupigane na Rwanda ?!!

Mbona tunakuwa kama vijana tusio na fikra tunduizi zaidi ya kuendeshwa kimihemko na jazba za kishabiki ?!!

Uwanja wa diplomasia ni mpana sana.....haswa diplomasia ya dunia ya sasa yenye maendeleo ya TEHAMA na AKILI MNEMBA kuliko ile waliyokuwa nayo akina kamarada Salim Ahmed Salim.....

Kila nchi inasimamia yake....hivi sisi watanzania tusimamiwe maslahi yetu na Rwanda tutakubali ?!!

Ikiwa huko DRC ni shamba la bibi.....kwanini tuwazuie wengine wasijichotee?!!

Lini tumekuwa "polisi wa mataifa ya afrika"?!!
Sera yetu ya nje ni KUTOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE kwani dunia ni pana mno na huoni leo TRUMP anawaondoa "police state" wa dunia ?!!

Huoni yeye mh.Rais Trump ,Elon Musk na seneta wa Utah ,M.Lee wakishajiisha KUJITOA NATO na UN kwa sababu Marekani inatumia nguvu kubwa za kiuchumi kulinda MASLAHI ya ULAYA zaidi ya maslahi yake nyumbani ?!!

Hii ina maana kuwa TUSIKARIRI maisha na kutaka kupita katika njia zilezile walizopita wazee wetu katika migogoro dhidi ya wengine....

ZAMA ZIMEBADILIKA....tulinde maslahi ya taifa letu kulingana na USASA.....
 
Mtoto mkorofi akitaka kupigwa huanza vurugu, na kujifanya mwehu haambiliki anarusha vitu, anatupa mawe nk. Ipo siku huyu mwehu Kagame, atapigiwa tu, Mizengo Pinda aliwahi kusema Bungeni, mtu mkorofi, apigwe tu. Nyerere aliwahi kusema kwa Idi Amin, sababu, nia na uwezo wa kumpiga tunao. Na atapigiwa tu.
Ingekuwa wewe ni rais ungekwenda kumpiga mama Joyce Banda kipindi kile cha sakata la ziwa Nyasa..... kwa jazba hizohizo alisimama kiongozi mmoja mwenye nguvu pale bungeni na kwa maneno makali akaitamani VITA na ndugu zetu wa MALAWI.....haya mambo hayahitaji JAZBA ,KUKURUPUKA,na kujifanya PATRON wa kila la wengine....

Diplomasia ndio njia njema katika sintofahamu.....
 
Ile posting imepewa imaarifi sana na Zitto Kabwe.
Immigration wanafanya kazi yao halali,what are you complaining?
Kama imewasirisha JE wasche wenyewe waamue.
Usiwaambir JWTZ how to react.
Jeshi linafanya mambo by The Book.
According to what they learn on Military Colleges.
Kama kuna tatizo pale watalijadili privately na Rwanda Police.
 
Huo ilikuwa zaidi ya ukaguzi, alafu anapostiwa
 
Yani kumrekodi mwanajeshi akisachiwa na askari polisi na kupost ndiyo kuonyesha kuwa nyinyi si lolote? Nadhani wanamaanisha hivyo.

Kumrekodi askari akipigwa sachi kiasi kile kisha kutuma kwenye mitandao ni moja ya uchokozi kati ya nchi na nchi.

Poleni mnaoona ni jambo la kawaida kurekodiwa kule na kuwekwa hadharani mitandaoni.
KAPIGWA TERO
 
-Je alisechiwa kweli? Kama ni ukweli na si editing kuna tatizo gani au kuna sheria gani iliyovunjwa?
-Anerekodiwa na nchi au na mtu binafsi au chombo cha habari?
-Uhuru wa habari za ukweli tunaoulilia si huo au hatuko tayari kwa 'painful truth' ni bora tudandanywe kwamba jeshi letu limeteketeza na kuwapelekesha M23 ilhali the realities on the ground ziko kinyume chake?
-Si vizuri tukajua madhaifu yetu tu ili tuwekeze kwenye kuyarekebisha?

Nadhani hata watu wamekuwa this time around wakijiuliza umuhimu wa hivi vita kwetu baada ya humiliation iliyowakuta wajeda wetu on the battlefield, huko mpaka wanachorwa kwenye katuni (caricatures) kitu ambacho back in the day enzi za Mchonga tuliheshimiwa na kuogopwa na majirani zetu wote(except Kenya/hatujawahi kukabiliana nao lakini kiukweli hawajawahi kutuogopa) lakini kwa sasa the story is different, nobody is scared of our army anymore.

NB: Utaratibu wa kuokota kila iliye UVCCM au kutumia vimemo kwa kujuana kama kigezo kikubwa cha kupata vijana wa kuingizwa jeshini for recruitment ukomeshwe, ni vizuri wakawa wanachukua the fittest(mentally and physically) katika vijana walio JKT na kuwaingiza jeshini moja kwa moja.
 
Aliyefanya hivyo ametututkana WATANZANIA wote.

Rais Kagame anatakuwa aombe radhi kwa kitendo cha kureko

Ujumbe ni kwamba Vikosi vyetu huko vimesarenda, sema hatuambiwi ukweli, Askari waliosarenda ndio husachiwa.

Hatuambiwi ukweli tu na hawa Viongozi wa mboga mboga fc.

Tutawaadhibu kwenye Box la kura kwa kulidhalilisha Jeshi letu la Wananchi.
Huu ni ukweli mchungu lakini CCM hawako tayari kuukubali kwani wao na jeshi kwa pamoja ndiyo waliodhalilisha nchi na ndiyo wanaopaswa kuwajibishwa, wameliharibu jeshi limekuwa la hovyo likiwa limebaki na sifa za mdomoni ukiuliza watakwambia muulize Idd Amin(that was in the seventies and Amin is dead and forgotten long time ago) ndiyo utajua ukali wetu.
 
Aliyefanya hivyo ametututkana WATANZANIA wote.

Rais Kagame anatakuwa aombe radhi kwa kitendo cha kureko

Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba Kitendo hicho ni miongoni mwa Propaganda za Vita (War Propaganda) ambapo yule aliyeshinda Vita anaonyesha Umwamba wake baada ya kupata Ushindi Mkubwa katika Uwanja wa Mapigano ya Vita. Hivyo, anafanya hivyo ili kuonyesha Dhihaka na Kejeli kwa wale walioshindwa Vita.

And in actual facts, Rwandan Forces and M23 Forces has won the Tremendous Victory, while DRC Forces together with all their counterparts including TPDF has accepted the Catastrophic Defeat!
Huu ndio Ukweli mchungu Sana ambao Kamwe hauwezi kupingika Wala kufichika.

Aidha, tukumbuke kwamba kwa scenario ya hiyo Vita huko Kivu-Goma, DRC, Askari wa nchi yetu walikuwa miongoni mwa Wanajeshi Mateka waliokuwa chini ya Vikosi vya Waasi wa M23 na Rwanda baada ya Waasi hao kushinda Vita.
Kwa jinsi ninavyofahamu, endapo kama kweli Vikosi vyetu vilikuwa vipo huru huko Goma baada ya Waasi kuuteka mji huo, basi naamini kwa dhati kabisa kwamba Wanajeshi hao wa Tanzania na Wanajeshi wengine wa SADC wangerejea katika nchi zao kwa kupitia mipaka ya nchi zingine lakini siyo Rwanda. Mathalani, Wanajeshi hao wa Tz wangeweza kupata safe passage kutoka kwa Waasi wa M23 ili waweze kutoka Goma na kupitia kwenye miji mingine ya nchi hiyo ya DRC Kama vile kutumia Uwanja wa ndege wa Kinshasa ili kurejea nyumbani.
The winner is the one who writes the history, toka enzi na enzi iko hivyo.
 
Yani kumrekodi mwanajeshi akisachiwa na askari polisi na kupost ndiyo kuonyesha kuwa nyinyi si lolote? Nadhani wanamaanisha hivyo.

Kumrekodi askari akipigwa sachi kiasi kile kisha kutuma kwenye mitandao ni moja ya uchokozi kati ya nchi na nchi.

Poleni mnaoona ni jambo la kawaida kurekodiwa kule na kuwekwa hadharani mitandaoni.
Picha
 
Hivi nchi ambayo una ugomvi nayo askari wako ambae kavaa combat za jeshi anaweza ingia kwenye mpaka wao bila ya wasiwasi wowote.

Watanzania tunaishi kwenye dunia yetu; mie mada zingine uwa naona kama wa-Congo na wanyarwanda wanataka kuingiza Tanzania katika migogoro yao.

Wapambane na hali yao tu, Tanzania aihusiki na wasitulazimishe kuingilia. Safari hii wazungu waletę wanajeshi wao huko ndio wenye shida na hizo rare earth mineral.

Siku Tanzania ikiwa na shida na nchi jirani waziri wa ulinzi au wa mambo ya nje wataongea; sio hizi mada za wa-Congo (wanaoishi Tanzania) na wanyarwanda wanaoishi Tanzania; kutulazimisha kuingilia. Mpambane na hali zenu.
100%✓
 
Back
Top Bottom