Aliyeweka video ya mwanajeshi akisachiwa kwenye mitandao kwani anatuma ujumbe gani?

Kuna compromise pahala wanajuana behind the scene ndio maana kampiga mkwara, ha hii ilivyotokea it wa a strategic move... watu wa mayenu wametuangusha
 
Mbona mimi sijaiona!
 
Kuna compromise pahala wanajuana behind the scene ndio maana kampiga mkwara, ha hii ilivyotokea it wa a strategic move... watu wa mayenu wametuangusha
Wakata viuno wa mayenu ni mbwa kabisa, kwanza wanasidiwa vita ambavyo wanatuingiza kutapeli lakini kibaya zaidi mkiwa battleground wakihongwa pesa wanawauza mnapigika kirahisi. Yaani wao pesa kwanza uzalendo sifuri, hawako tayari kupigana lakini wanatutapeli tuwapinie vita vyao. Tumepigania nchi nyingi sana na hatujafaidika chochote, we better change and start thinking the capitalist way of thinking yaani tuwe tunaingia vitani kwa maslahi ya kiuchumi tu na si vinginevyo.
 
Tupe ushaur mkuu, tufanye nin?
Inategemea mlivyo uchukulia na kuupokea ujumbe mlio fikishiwa.
Kama nyinyi ni sehemu ya hao waliotuma ujumbe, mnaweza kujipongeza kwa kuufikisha ujumbe, huku mkisubiri kupata dalili toka kwa hao waliolengwa watakavyo upokea ujumbe wenyewe.
Kama nyinyi ni sehemu ya walengwa wa kufikishiwa ujumbe, amueni mtakavyoona inafaa. Mnaweza kufurahi kwa kupewa ujumbe huo na kuwashukuru walio wafikishia. Mnaweza pia kupuuza, au mnaweza nanyi kuwafikishia ujumbe wenu ili wajue kuwa mmeupokea na kuuelewa ujumbe wao. Bila shaka mkifanya hivyo, na wao watajuwa ujumbe wenyewe mmeuchukulia vipi. Na ikiwa hivyo, sasa inabaki kusubiri hatua zifuatazo huko mbele ya safari.
 
Hao watutsi wanatuma ujumbe kwamba jwtz sio chochote. Kwa asili watutsi ambao ni jamii ya mbari ya kihima wanajiamini ni wabaguzi kijamii na kwa asili wanataka kutawala kwenye jamii. Bila wao kuongoza basi watadai wanabaguliwa. Yaani kuongoza wanaona ni haki yao wengine hamstahili na hamuwezi. Hata kama ni uchaguzi kidemokrasia nyinyi wabantu msipomchagua mtutsi basi hapo inakua nongwa. Watalalamika eti wamebaguliwa.
 
Mi nadhani kama mama hatakuwa ameauthorize hata covert operation nicknamed "cutting the head of a snake" atakuwa anafanya makosa makubwa sana strategically
Ndugu tangu lini nyumba ambayo ni kichwa Cha familia huwa ibaheshimika ..haya ni matokeo ya mwanamke kutawala nchi
 
Mi nadhani kama mama hatakuwa ameauthorize hata covert operation nicknamed "cutting the head of a snake" atakuwa anafanya makosa makubwa sana strategically
Yuko busy analinda kichwa chake kisikatwe hivyo hiyo 'cutting the head of the snake' anaweza hisi mnamuwinda yeye mumkate kichwa.
Njia rahisi ya kumfanya aingie full force mwambieni CHADEMA wako Eastern DRC wanachota madini hapo atatuma mpaka KMKM na UVCCM wote.
 
Watu kama nyie ndo mnafanya wanajeshi wajione wako juu ya sheria na kuwapiga raia hovyo kila wanapojisikia. Kama sheria inataka wasachiwe acha wasachiwe.
 
Mi nadhani kama mama hatakuwa ameauthorize hata covert operation nicknamed "cutting the head of a snake" atakuwa anafanya makosa makubwa sana strategically
Mna hamu na vita kwa kuwa hamjawahi kuiishi vita? Hakuna mwendawazimu wa kuanzisha vita kwa sababu za kijinga kama hizo. Vita si lelemama
 
Huyu mama na waziri wa kike yule mama wote hakuna kitu,wanaonea wabongo lakini nje ya Tz ni underdog
We all know yule wazir hana qualification za kuwa pale, hana background ya jeshi lolote. It all for jinsia,

Wenzetu mawazir wa ulinzi ni formaer generals, ex high ranking police officers, hawa watu wa experience yantofauti

Unamuweka career politician unategemea nn?
 
Reactions: rr4
Mi nadhani kama mama hatakuwa ameauthorize hata covert operation nicknamed "cutting the head of a snake" atakuwa anafanya makosa makubwa sana strategically
Na kiingereza chako cha juhudi binafsi unaona umeongea point. Punguza kutazama movies
 
Video hiyo ilitengenezwa kwa kusudi maalum, kufikisha ujumbe na kueneza propaganda.
Lakini wanasahau au hawajui maana itakavyo chukuliwa na hao wanao pelekewa ujumbe.
Kuna video za kutengeneza but not that one. Unaweza tupia kwenye soft fulan itakuambia kama imetengenezwa au lah
 
Kuna mambo muhimu ume yaandika hapa, lakini mengine hayapo sahihi.
Kwa mfano: Ninakubaliana moja kwa moja na wewe kwamba hawa wakongomani hawastahili msaada wetu hadi hapo watakapokuwa tayari wao wenyewe kujitoa mhanga kwa nchi yao. Ni aibu sana kwa nchi tajiri, kubwa kama hii kudhalilishwa kiasi hiki, tena na ki-nchi kisichokuwa na lolote!
Wakongomani wakionyesha dhamira ya kweli ya kuipigania nchi yao, ni kwa manufaa yetu kabisa kuwapa msaada, hata wa kijeshi, kwa sababu nasi tunayo maslahi ya kibiashara nao. Utulivu wa Kongo ni faida kwetu katika shughuli zote za maendeleo.

Mfano mwingine, ambao pengine nina tafsiri tofauti kidogo na yako ni huo unaelezea wao "kutuingiza kitapeli" kwenye vita yao. Binafsi sidhani kuwa "tunaingizwa kitapeli" kwenye vita hiyo. Hii tunajiingiza sisi wenyewe (soma viongozi/watawala) wa nchi yetu ndio wanatuingiza humo kitapeli kwa kuingiza jeshi letu kwenye vita kwa minajiri ya kulipwa pesa (kulinda amani kwa malipo), bila kujali anayelipa ni Umoja wa Mataifa au nani. Jeshi letu linageuzwa kuwa kitega uchumi? Mbaya zaidi ni kuwapeleka vijana wetu kuwa wahanga wa vita hiyo, bila ya kuwapa maelekezo sahihi ya nini wafanye wanapolazimika kujihami. Ni lazima vijana wetu wanapo pelekwa kokote duniani, maelekezo yawe usalama wao kwanza kabla ya masharti mengine yoyote kutoka kwa hao wanaotuingiza kwenye biashara hiyo. Mpumbavu yeyote anaye thubutu kushambulia jeshi letu wakati likiwa kwenye ulinzi wa amani, ni lazima apewe fundisho, kwa maamuzi yetu wenyewe, siyo hayo ya Umoja wa Mataifa au mwingine yeyote.
Kagame na wapwa zake M23 katumia udhaifu wa matakwa ya Umoja wa Mataifa kuwadhalilisha na kuwaumiza na kuwaua vijana wetu. Hili lisiruhusiwe tena mahali pengine popote.

Mfano wa tatu, nisiokubaliana na wewe moja kwa moja:
Tumepigania nchi nyingi sana na hatujafaidika chochote, we better change and start thinking the capitalist way of thinking yaani tuwe tunaingia vitani kwa maslahi ya kiuchumi tu na si vinginevyo.
I am very proud of what Tanzania was able to do during the liberation struggle. We cannot now seek to turn our defence forces into a mercenary force for hire.
The primary objective for our force is for the defence of our mother nation and its people.
 
Mpka sasa nimegundua wew sio mtanzania. kwanin..

Kwa sabab luga unayoitumia kwanza niyakichochez.

Pili jins ulivo andka kana kwamba wew hauhusiki upande wowote je wew ni nani? Au upo tz, congo au rwanda.
 
Kuna video za kutengeneza but not that one. Unaweza tupia kwenye soft fulan itakuambia kama imetengenezwa au lah
Hapana. Hukunielewa maana yangu. Sikuwa na maana hiyo uliyo lenga wewe. Video ni halisi, na aliye itengeneza na kuruhusu kuiwekwa mitandaoni alikuwa na lengo maalum
 
Mpka sasa nimegundua wew sio mtanzania. kwanin..

Kwa sabab luga unayoitumia kwanza niyakichochez.

Pili jins ulivo andka kana kwamba wew hauhusiki upande wowote je wew ni nani? Au upo tz, congo au rwanda.
EEEEnHEEEEE!
Mbona unajihami mapema hivyo!
Mimi sina sababu ya kujificha kwenye vichaka kama unavyotaka kufanya wewe.
Huwa sina simile kabisa na 'pretenders' wa aina yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…