Tetesi: Alliance Schools yalazimisha watoto kuchanga Tzs100,000 ili kushiriki mahafali 2019/viongozi mlikane hili

Tetesi: Alliance Schools yalazimisha watoto kuchanga Tzs100,000 ili kushiriki mahafali 2019/viongozi mlikane hili

Aaah wapi miaka ya elfu mbili na mbili ni zamani ? Tuliona wazazi walokuja. Ila mimi binafsi wala sikumind wa kwangu kutokuja. Hapa nakumbia hata UDSM mimi sikurudi kwenye graduation.
Hata wanangu,i thank God wanasoma shule ambayo hakuna mambo ya graduation.
Sherehe hazina mashiko.
Usipifanya graduation usidhani mwanao ndio hatafanya Kama wa kike Kuna vidume vitamfanyia au Kama wa kiume viwifi vya hiari vitamfanyia Sasa usuke au unyoe
 
Ndio maana Kuna Uhuru wa kuchagua mtoto asome shule ya kiwango gani na pia unakuwa umeshejua taratibu za shule husika, cha msingi kama huwezi peleka mtoto shule za kata.
Bei ya mahindi haitaingiliwa, nadhani kwa vile hii ni secta binafsi, sidhani kama serikali inapaswa kuingilia pia.
 
Wanafunzi waliomaliza mitihani yao kidato cha nne Alliance Schools zaidi ya 200, wanatakiwa kuchanga 100,000/-TZS ili kushiriki mahafali ya kidato cha nne 2019. Iwapo kila mwanafunzi atatoa pesa hiyo ni zaidi ya 20,000,000/- Milioni Ishirini,

Mchango huo utahusisha mwanafunzi husika na wazazi wake wawili tu, yaani watu watatu (3).

Ili kuweza kuhusisha wadogo ama wakubwa wa mwanafuzi, yaani watoto wenziwe kwenye famila inabidi kila mtu anayezidi atoke 10,000/-TZS ili kuweza kuingia ndani ya ukumbi wa mahafali, kama huna ni kubaki nje na wanafamilia hawa washindwe kushudia mdogo ama mkubwa wao akitunukiwa cheti.

Yaani imekuwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu maana laki moja kwa mahafali ambayo ni wajibu wa shule kwa wahitimu ni changamoto. Watu 3 wakati kiserikali familia ina watu 6. na ni ukweli hapa TZ kuna wajomba shangazi na watoto wao, mara zote kwenye sherehe kama hivi tunashirikishana, iweje bibi au babu kumuona mjukuu wake akihitimu form 4 alazimishwe kulipa TZS 10,000/-? inafahamika kula kwenye mahafali haiwezekani ndugu wote wa wahitimu wakala ama kwa ukweli kuwa itabidi chakula kiwe kingi sana ambacho lazima kitapoteza ubora wake, ama mtu tu hapendi kula nje ya chakula cha familia yake mwenyewe, kwa maana kwenye mahafali kula sio lazima, iweje ulazimishe mtu anayekuja kwenye mahafali ya ndugu yake atoe 10,000 eti lazima ale? unauhakika chakula unachoandaa kinakidhi mahitaji ya kila mshiriki? ya kiafya ya kijamii ya kidini etc?

Tunaomba Viongozi hasa Mkoa maana Rais naye anakazi nyingi na nyinyi ndio wasaidizi wake muingilike kati maana sio haki, kwa vile watoto ni haki yao kufanya na kuhudhuria mahafali isitumike kujipatia pesa kama kitapeli vile maana wazazi wangependa watoto wao washiriki. Ada wazazi walikwisha lipa zote, ni haki ya watoto kufanyiwa mahafali na shule. Hata kama kungekukwa na mchango basi 10,000TZS kwa mtoto. Suala la kula ni la watoto sio wazazi na familia yote maana nyumbani pia watakuwa wameandaa vyakula.

Wazazi na watoto wananyanyasika vile huwezi hitimu alliance ukafanyia mahafali Omega mfano tu.

Kama anaona lazima kuwanyonya wazazi na wahitimu basi agawe vyeti watoto warudi majumbani kwao kula na kunywa, lakni asinyime watoto na ndugu zao haki ya kushiriki mahafali kwa kisingizio cha kuwapa chakula kwa bei ya juu kupita maelezo, chakula ambacho sio lazima wote wanakihitaji na wengine hawataweza kukikutmia kwa sababu za kiafya

Asante kwa msaada wa wenu viongozi serikali-Mwanza
Waleten kayumba huku hakuna ma pesa mengi
 
Usipifanya graduation usidhani mwanao ndio hatafanya Kama wa kike Kuna vidume vitamfanyia au Kama wa kiume viwifi vya hiari vitamfanyia Sasa usuke au unyoe
How?Kuna shule hazina graduation kabisa. Mkimaliza mitihani na kufunga shule ndo basi. Hakuna cha graduation wala nini.
 
Kama sio sehemu ya ada atapata cheti chake hata kama hakwenda kwenye graduation iyo iko wazi
Atakapokwenda kuchukua cheti atakuta deni. Wakati huo yuko peke take
UKIWA MASIKINI USIPELEKE MWANAO SHULE KAMA HIYO
 
hujaelewa, uhudhurie usihudhurie Laki unatoa ndio ilivyo; sio tu laki ni kubwa bali ni lazima. nadhani umeelewa. na kwa vile mahafali inafanyika wiki 2 baada ya mtihani watoto wengine walikwisha safari kwenda Rukwa, Mbeya Kuja Dar Tabora etc lakni ama warudi kwa gharama zao ama wasirudi kwa hofu ya gharama laki lazima atoe wakati wa kuchukua cheti. Umeleewa???
Nyinyi ndo wale aina ya watu mkitongoza mademu mnajifanya mna pesa mnafanya kazi nzuli mnajifanya mnafanya kazi sehemu nzuli.

Siku demu akikupiga mzinga wa vocha ya jero tuu unaanza kusema Mara Ohoo sina hela Mara Ohoo mshahara haujatoka, Mara Ohoo mtandao unasumbua mwisho kabisa yakikushinda unakimbilia jf kuanzia thread
"mademu wa siku kwanini wanapenda helaa ""

Kumbe matatizo mnayatafuta wenyewe
 
hoja ni utajiri ama umaskini au suala la graduation ambayo uwepo usiwepo unaamuriwa kutoa 100,000? juu ya gharama kuwa kubwa, ukiita umasikini wala sioni maumizi maana maskni aliwalipaje ada 4yrs ? angalia hoja sio kingine mkuu

WATU MASIKINI WANA MATATIZO KWELII !!!!

HIYO SHULE NI YA WATOTO WA MATAJIRI SASA WEWE KINACHOKUUMA NI NINI KUCHANGISHWA 100,000
 
Kama mtoto hadaiwi ada na kamaliza pepa, hiyo graduu si lazima kama uwezo ni mdogo.
 
sio sehemu ya ada ndio maana iko pembeni na cha ajabu ni watu kulazimishwa kuchanga hata kama hawana muda wa kuhudhuria kwa vitisho kuwa iwapo hutachangaa hupewi cheti muda ukifika, is this how it is supposed to be?

Kama sio sehemu ya ada atapata cheti chake hata kama hakwenda kwenye graduation iyo iko wazi
 
Tupeleke watoto Shule za hadhi yetu hatujui tunawaathiri vipi Kisaikolojia tunavyoacha kuchangia baadhi ya entertainment huku wenzao wakienda
 
Hizi Tz kuna mdudu gani kichwani wakuuuu? mtu akilalamikia unjust expenditure isitafasiriwe eti hana hela, I can tell you wenye hela wote wako makini na matumizi kuliko maskini wengi wanavyofikiria .

LAKNI NIMESHANGAA NAONA POST NYINGI KAMA HUNA HELA, JIBU HILO NI SIMPLE KABISAA ASIYE NA HELA ATAKUWA ANADAIWA ADA NA HIVYO ANGEFUKUZWA KITAMBO HUKO FORM ONE OR TWO

Kama mtoto hadaiwi ada na kamaliza pepa, hiyo graduu si lazima kama uwezo ni mdogo.
 
UKO SAHIHI KABISAA, kitu anachotumia huyu ni kuwa wazazi hawataweza kutelekeza watoto wao wasifanye graduuu, misuse of trust. Najua wazazi watatoa hela kufurahisha watoto wao lakni ni very unjust. na hoja yangu ni hiyo kuwa UNJUST GAINS serikali haiwezi kuacha watu wajipatie pesa kwa njia za ujanja ujanja take my words

Tupeleke watoto Shule za hadhi yetu hatujui tunawaathiri vipi Kisaikolojia tunavyoacha kuchangia baadhi ya entertainment huku wenzao wakienda
 
Nimependa hapo uliposema RC alitazame hilo jambo,nikakumbuka pia kuna DC.
Kwa upande wangu nahisi ili ni swala ni la Afisa Elimu wa Wilaya na Bodi ya Shule ndio wahusika na wanapaswa kulisimamia kwa nguvu zote, kukiwa na walakini ndio DC alitolee tamko (Order)
Kuhusu kiwango cha mchango so kikubwa sana ukitazama na thamani ya fedha kwa sasa,sema yapaswa kupunguzwa ili kuruhusu familia zenye vipato vya chini kwa kipindi hicho cha sherehe zipate kujumuika na wapendwa wao kama ulivyopenda aina ya kujumuika,pia watu watambue kupungukiwa ni swala la kawaida na sio kitu cha kufanyia mzaha kama watu wasio na weledi wanavyodhihaki na pia ikumbukwe mchango mkubwa huumiza baadhi watu kwa kuwanyima nafasi ya kushiriki..wazo lako naliunga mkono.
 
Yaani mimi kusema ukweli nilijiuliza sana umuhimu wa wazazi kwenda kwenye graduation. Mimi O level,A level yaani hakuna ndugu yangu alokuja kwenye graduation. Na niliona poa tu. University ndo kabisa hata kwenye graduation sikwenda maana nilikuwa kazini tayari. Yaani mimi sherehe wala huwa sioni kabisa umuhimu wake.
Nakupa ushauri,pindi utapokuwa na familia yako au kama unayo tayari..uwe unashiriki mahafali na usijetumia nafasi yako ya kutokufanya sherehe kuwanyima jamaa au watoto wako haki ya kushereheka na kihitimu kuna furaha uliikosa au waliikosa ndugu na jamaa zako.Pia kuna taarifa wahudhuriaji huzipata na kujifunza bila kusahau Baraka ya kujumuika pamoja.
 
hoja ni utajiri ama umaskini au suala la graduation ambayo uwepo usiwepo unaamuriwa kutoa 100,000? juu ya gharama kuwa kubwa, ukiita umasikini wala sioni maumizi maana maskni aliwalipaje ada 4yrs ? angalia hoja sio kingine mkuu
KILA TAASISI INA UTARATIBU WAKE NA HIYO NI SHULE INA UTARATIBU WAKE NDO MAANA WAKAWEKA UTARATIBU WAO .........

SASA WEWE NI KAMA NANI UWAPANGIE WATU TARATIBU WALIZOJIWEKEA NDO MAANA HATA VYUONI KUNA UTARATIBU WAKE

UKITAKA KUSOMA VYUO VYENYE PESA ADA KUANZIA MILIONI MOJA NENDA IFM, CBE, ST.JOSEPH,TUMAINI .....

ILA UKITAKA VYUO ADA LAKI MOJA NENDA VETA
 
bodi sijui kama ipo, na hawa ma RC ama DC ndio wanatoa maelekezo kwa watendaji kama DEO ama REO kkushughulikia na kuripoti ndio maana tuna waadress straight. wao ndio wenye wilaya na mikoa. Asante lakni kwa kuwa na mawazo ya wenye akili. Ukisoma huko juu ni huna hela huna hela huna hela, ninakubali lakn angalizo lipo pale pale wasio na hela walifukuzwa form one two or three kwa kudaiwa ada, hawakufanya mitihani allianceschools maana ni private school. cha msingi watu wapate hela halali sio kuchomekea humo humo kwenye graduuuu kuvuna pesa, 20Mil and abaove za nini?

Nimependa hapo uliposema RC alitazame hilo jambo,nikakumbuka pia kuna DC.
Kwa upande wangu nahisi ili ni swala ni la Afisa Elimu wa wilaya na Bodi ya shule ndio wahusika na wanapaswa kulisimamia kwa nguvu zote, kukiwa na walakini ndio wamtaarifu DC.
Kuhusu kiwango cha mchango so kikubwa sana ukitazama na thamani ya fedha kwa sasa,sema yapaswa kupunguzwa ili kuruhusu familia zenye vipato vya chini kwa kipindi hicho cha sherehe zipate kujumuika kama ulivyopenda aina ya kujumuika,kupungukiwa ni swala la kawaida na sio kitu cha kufanyia mzaha kama watu wasio na weledi wanavyodhihaki..wazo lako naliunga mkono.
 
kumbe graduu ni ya mmliki wa shule? huelewi shule ni mmliki wazazi na wanafunzi? mmoja akigoma hapo ujue shule si shule tena. Yaani makubaliano kwenye mambo haya ni muhimu kuliko eti namiliki, sio kituo cha mafuta hicho ahahhahaha

KILA TAASISI INA UTARATIBU WAKE NA HIYO NI SHULE INA UTARATIBU WAKE NDO MAANA WAKAWEKA UTARATIBU WAO .........

SASA WEWE NI KAMA NANI UWAPANGIE WATU TARATIBU WALIZOJIWEKEA NDO MAANA HATA VYUONI KUNA UTARATIBU WAKE

UKITAKA KUSOMA VYUO VYENYE PESA ADA KUANZIA MILIONI MOJA NENDA IFM, CBE, ST.JOSEPH,TUMAINI .....

ILA UKITAKA VYUO ADA LAKI MOJA NENDA VETA
 
Hizi Tz kuna mdudu gani kichwani wakuuuu? mtu akilalamikia unjust expenditure isitafasiriwe eti hana hela, I can tell you wenye hela wote wako makini na matumizi kuliko maskini wengi wanavyofikiria .

LAKNI NIMESHANGAA NAONA POST NYINGI KAMA HUNA HELA, JIBU HILO NI SIMPLE KABISAA ASIYE NA HELA ATAKUWA ANADAIWA ADA NA HIVYO ANGEFUKUZWA KITAMBO HUKO FORM ONE OR TWO
Tanzania wajinga wengi ndio maana hata huduma zetu za msingi tunanunua

Serikali inajenga, barabara, hospitali na Huduma mbali mbali za kijamii halafu watu wanamshukuru Rais, utafikiri anatoa pesa yake mfukoni.

Halafu mtu anashangaa kwa nini ccm inazidi kutuburuza kama ng'ombe.
 
Shule nyingi za binafsi kwa miaka ya ‘graduu’ mchango wa mahafali huwa unajumlishwa kwenye ada, na sio kutozwa kwa kuchangia pekee yake.... labda baadhi ya shule zina utaratibu tofauti.
 
Back
Top Bottom