Pre GE2025 Ally Hapi: Vyombo vya dola shughulikieni wanaotaka kuzuia uchaguzi

Pre GE2025 Ally Hapi: Vyombo vya dola shughulikieni wanaotaka kuzuia uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
VIDEO:

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ally Hapi, ameviomba vyombo vya Dola kuwachukulia hatua watu wote wanaotaka kuharibu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Hapi ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM na Jumuiya ya Wazazi wilayani Muheza, mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya mapokezi ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Matukio ya Rafu za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hapi, amesema kauli za Mwenyekiti wa Chadema na viongozi wengine wa Chama hicho kuhusu kuzuia uchaguzi mkuu hazina hoja wala mashiko, bali ni dalili za kuwa Chama hicho hakijajiandaa na uchaguzi Mkuu ujao.

Aidha amesema kauli hizo zinakinzana na ukweli kwamba yako mabadiliko yaliyofanyika katika sheria za uchaguzi nchini mwaka 2024, ambayo pamoja na mambo mengine yameondoa kupita bila kupingwa, kuundwa Tume huru ya uchaguzi (INEC) na kuondoa ulazima wa Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi na badala yake sheria kutamka kuwa afisa mwandamizi wa serikali atateuliwa na tume kuwa msimamizi wa uchaguzi.

Hapi amebainisha kuwa, katika mchakato wa mabadiliko hayo ya sheria za uchaguzi mwaka 2024, wadau wote walishirikishwa na kutoa maoni ikiwemo CHADEMA, taasisi za dini, taasisi za kiraia, vyama vingine vya siasa na wananchi kwa ujumla.“CHADEMA walitoa maoni yao kama wadau, na baadhi ya maoni hayo yaliingia katika sheria. Kama wanabisha kuwa hawakushiriki kutoa maoni watoke hadharani wakatae.” Alisema Hapi.

Kuhusu hoja ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ya kutaka uchaguzi mkuu usogezwe mbele, Hapi ameeleza kuwa huko ni kuwanyima haki wananchi ya kuchagua viongozi wao na kwamba kuna kila sababu ya kuamini kuwa CHADEMA kama Chama haijajiandaa kwa uchaguzi, na kwamba wanatafuta visingizio kutaka uchaguzi mkuu usogezwe mbele kinyume cha sheria ili wapate kutafuta fedha kwa wafadhili wao na kuponya majeraha ya ndani ya Chama chao yaliyotokana na uchaguzi wa ndani.“

Wenzetu hawajajiandaa kwa uchaguzi. Wako dhaifu na wana ukata mkubwa, ndiyo maana katika uchaguzi wa serikali za mitaa yako maeneo mengi walishindwa kusimamisha wagombea. ” Amesema Hapi.

VIDEO:

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ally Hapi, ameviomba vyombo vya Dola kuwachukulia hatua watu wote wanaotaka kuharibu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Matukio ya Rafu za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3246408
Wanaotaka uchaguzi usifanyike walisema sababu ni ccm kutumia vyombo vya dola hili kushinda uchaguzi. Kumbe ni kweli ccm inatumia vyombo vya dola kufanya inayotaka.
 
Big hand to Ally hapi, kusema tu ya kwamba uchaguzi hautafanyika, ni kosa kamilifu la jinai.
Unapinga mipango ya serekali kwa njia ambazo pengine huenda zikahusisha ugaidi/uvurugaji wa amani na usalama wa watu.
 
Up
Ingefaa zaidi kushughulika na wezi wa chaguzi kabla ya kufikiri kuhangaika na wanaolenga kuwazuia wezi kuiba.
Upinzani muwe mnajitafakari, wenzenu muda huu wanazindua miradi ya maji, mahospitali, wanakwenda kusikiliza shida Za watanzania, upinzani umekaa kiambazani unaota umeshajenga mashule, umeshajenga barabara na kura watashinda, what a shits dreams!
 
Huo ni wajibu wa kila uchao wa serikali na sii chama ila chama kinageuza hayo kuwa ni sehemu ya kampeni ya hadaa kwa watanzania hata miradi hewa inaongelewa kuwarubumi wasioelewa ni sawa na bila aibu unaleta hoja okotezi.bila kutambua huo ni wajibu wa kwanza kwa serikali kwa watu wake.Na vyote hivyo havifai kuwa sehemu ya siasa a.k.a sii hasa.
 
VIDEO:

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ally Hapi, ameviomba vyombo vya Dola kuwachukulia hatua watu wote wanaotaka kuharibu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Matukio ya Rafu za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3246408

Huyu bwege kichaa, hajui kuwa watu na taasisi zote zilizotoa maoni zilisema kuwa zinataka tume huru ya uchaguzi, na kama hakuna tume huru ni aheri uchaguzi usifanyike.
 
VIDEO:

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ally Hapi, ameviomba vyombo vya Dola kuwachukulia hatua watu wote wanaotaka kuharibu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Matukio ya Rafu za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3246408
Ccm wameanza kulialia, subirini dawa iwaingie. Vyombo vya Dola waachieni wanasiasa wapambane...
VIDEO:

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ally Hapi, ameviomba vyombo vya Dola kuwachukulia hatua watu wote wanaotaka kuharibu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Matukio ya Rafu za uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3246408
Ccm imeanza kulialia
 
Up
Upinzani muwe mnajitafakari, wenzenu muda huu wanazindua miradi ya maji, mahospitali, wanakwenda kusikiliza shida Za watanzania, upinzani umekaa kiambazani unaota umeshajenga mashule, umeshajenga barabara na kura watashinda, what a shits dreams!

Duh! Una kiwango gani cha elimu?

Yaani hata kujua kuwa hayo yanafanywa na Serikali hujui?
 
Back
Top Bottom