Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasiyo ya Muungano

Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasiyo ya Muungano

Nusu kwa nusu!
Jeshi mtaweza kulihudumia hata siku tatu
Mtaweza kuendesha wizara ya mambo ya ndani kwa wiki
Mtaweza kuendesha ubalozi hata mmoja
n.k

Hawawezi kulipia mgonjwa iwe nusu kwa nusu.
Hawawezi bili ya umeme iwe nusu kwa nusu.
Hawawezi kudumia hata balozi moja, leo nusu kwa nusu
Hawawezi kulipia wabunge wao, halafu iwe nusu kwa nusu
Hawawezi kulipia wanafunzi wao, leo wanataka nusu kwa nusu

Ni watu milioni 1 na nusu wanaishi Tanganyika

Unachekesha sana, ndio maana unasema znz inachangia kupitia vocha za simu

Weka namba kwa bajeti ya bilioni 900, znz itatoa nini.
Kwa makusanyo ya bilioni 300 kwa mwaka znz itatoa nini

utoe 0 nitoe 10 halafu useme tumechanga! tugawane nusu kwa nusu! tehe tehe

Kwaheri

Kwa heri karibu lakini ndio hivo mnatoa mnatulinda , umeme tunatumia hatulipi, wabunge 100 mnawalipa na mawaziri wapo wanaongoza wizara. Zenu za muungano....mapolisi wapo wana tulinda...na sie tunaoa tu dada zenu...mna cha kufanya ?

Hamna na bado tutadai zaidi kila siku..itabaki kelele tu
 
Mtatulipa tu mishahara , mtatulinda , umeme mtatupa na hatulipi na tuta waolea tu dada zenu...
[emoji3][emoji851][emoji41]
Alafu bado mnalilia [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Kwa heri karibu lakini ndio hivo mnatoa mnatulinda , umeme tunatumia hatulipi, wabunge 100 mnawalipa na mawaziri wapo wanaongoza wizara. Zenu za muungano....mapolisi wapo wana tulinda...na sie tunaoa tu dada zenu...mna cha kufanya ? Hamna na bado tutadai zaidi kila siku..itabaki kelele tu
Afadhali mumeanza kuelewa, nina uhakika mtaacha hoja za mabalozi, mtajua hakuna uonevu, na mchango wa znz si kupitia vocha za simu!!! mbavu zangu jamani
 
"Wajinga ndio waliwao"
Hapana, siku hizi watu wananena bila kificho
1. Mchango wa znz uonekane si kupitia vocha za simu, kwi kwi kwi , ha!
2. Znz ichukue jukumu la watu na taasisi zake, bili hadi za wagonjwa inatisha
3. Muungano ni gharama si shamba la kupata ajira za mabalozi, bili zikisahauliwa na wznz
4. ZNZ isaidie vibili ndani ya uwezo kama za wagonjwa, umeme, wabunge n.k. inapendeza
 
Muungano kwa sasa hauna faida kwa Tanganyika bali umekuwa ni mzigo mkubwa na mzito, kule Zanzibar wamelundika Utitiri wa wabunge, madiwani na watumishi wa umma, yaani wengi kupita kiasi huku pato lao la Zanzibar likiwa Dogo sana haliwezi hata kuwalipa mishahara nusu ya Watumishi wao, Tanganyika inabeba mzigo wa kuwalipa mishahara, kuwalipia Bill za Umeme, maji na Kodi za nyumba za viongozi pia kuwalinda na majeshi kwa gharama kubwa, Ally kessy katema nyongo, Ukweli unauma na hii itawauma kweli kweli na huenda ikaleta migogoro mikubwa kati ya wabunge wa Zanzibar na Ally kesi.

Mkuu ktk bunge la jamhuri kuna wabunge wa znz aina mbili wapo wa ccm na cuf.
Kauli ya mzee kesy nikauli kinzani na katiba ya chama chake na ni kauli inayopishana na itikadi na falsafa ya ccm dhidi ya muungano.

Na hata muundo wa muungano unapishana na kauli ya mzee kesi.
Mzee kesy anataka wabunge wa znz wasishiriki mijadala ya wizara zisizo za muungano.
Je ni wabunge gani wa znz wanaoathirika au wanao faidika na kauli za mzee kesy ni wa ccm au cuf?
Je ninani wanaotakiwa kutoka nje ya bunge la jamhuri wakati wa kujadili mambo ambayo siyo ya jamhuri(YA TANGANYIKA ISIYO KUWEPO) ni hao wanata kujadili au ni wabunge wa bunge la jamhuri wanao tokea ktk majibo ya znz?

Ili mzee kesy afanikiwe matakwa ya kauli zake kwanza angehakikisha kama bunnge la tanganyika lipo na wabunge wa tanganyika wapo na wamekula kiapo cha ubunge wa tanganyika na wamechaguwa viongozo wa bunge hilo kuanzia spika nk.

Vinginevyo mzee kesy ana wananga wana ccm wenzake wa visiwani na bara na zaidi hastahiki kuwa ccm maana anakiuka katiba ya ccm ambayo ndio aliyo itumia kuingilia bungeni.
 


Mbunge wa Nkasi Ally Kessy

Na. Awadh Ali Said

Natafakari tu, kuhusiana na hoja ya Mh. Ally Kessy kuwa Wabunge kutoka Zanzibar wasishiriki shughuli za Bunge pale yanapozungumzwa mambo yasiyo ya Muungano kama vile kilimo, utalii, afya n.k; ambayo amedai kuwa kimsingi ni mambo ya Tanganyika na Wabunge wa Zanzibar hayawahusu.

Kwanza nakubaliana na mtazamo wake (kwa asilimia mia) kuwa Wabunge wa Zanzibar wasishiriki shughuli za Bunge yanapokuja mambo yaliyo nje ya Orodha ya Mambo ya Muungano. Ukweli ni kuwa mambo yasiyo ya Muungano Wazanzibari hayawahusu asilani na kushiriki kuyajadili, kuyafanyia maamuzi na kuyatungia sheria SI haki wala haieandani na hata mantiki ya kawaida.

Ukiwa Mbunge unatakiwa ujadili mambo yanayowahusu wananchi wako na wewe mwenyewe, na pia huwezi kushiriki utungaji wa sheria kwa mambo ya wengine ambapo baadae sheria hio haikugusi wewe ulieshiriki kuitunga wala wananchi wako. Zaidi ya hayo ni kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliungana kupitia Orodha ya MAMBO YA MUUNGANO, nje ya mambo hayo kila upande una haki ya kujiamila mambo yake.

Mambo ya Muungano yalianza 11 na sasa yamefikia 22. Ukweli ulio bayana ni kuwa Muungano huu uliakisi Mambo ya aina tatu yaliyo tofauti kabisa. Aina ya kwanza, Mambo ya Muungano (ambayo haya yanawahusu pande zote mbili za Muungano na ndio MAMBO YA SHIRKA).

Aina ya pili, Mambo ya Tanganyika (ambayo ni mambo ya upande wa Tanganyika tu ukiondoa yale ya Muungano ) na aina ya tatu , Mambo ya Zanzibar (ambayo ni mambo ya upande wa Zanzibar tu ukiondoa yaliyo ya Muungano).

Kiinimacho cha kisiasa kilichotokea ni pale Mambo ya Muungano , ambayo ni mambo ya SHIRKA yalipochanganywa na Mambo ya Upande wa Tanganyika yakatiwa KAPU moja ikawa Mambo Mawili chini ya Serikali Moja na chini ya Bunge Moja.

Huo ndio msingi wa figisufigisu inayoukumba Muungano huu tokea kuasisiwa kwake miaka 52 iliyopita. Na ndio maana wapo wanaohoji ufasaha na udhamira wa Muungano kwa kitendo kile cha kuyamega mambo muhimu ya Nchi ya Zanzibar na kuyaondoa katika Milki na Mamlaka ya Zanzibar na kuyaingiza na kuyachanganya na mambo ya Nchi ya Tanganyika na Zanzibar ikawa haina uwezo wa kimaamuzi juu ya mambo hayo na kuwa milki na khatamu za kimaamuzi juu ya mambo yake hayo ziko kwa Nchi nyengine kupitia huo ulioitwa Muungano.

Mambo ya Tanganyika na Mambo ya Muungano ambayo Zanzibar ni mshirika yamehodhiwa na Tanganyika kupitia inayoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tanganyika haikumega chake chochote na kukiingiza.popote. Yaliyomegwa ni mambo ya Zanzibar nayo yakaingizwa katika Tumbo la Tanganyika ambayo nayo baada ya kujiongezea Mamlaka ikajibadilisha jina na kuwa Tanzania. Kiinimacho cha mchana kweupe.

Lakini eneo ambalo bado nipo kwenye tafakuri kuona usahihi wake ni pale aliposema Wabunge wa Zanzibar ndio watoke Bungeni kupisha mijadala ya Mambo ya Tanganyika.

Nadhani kwa vile lile ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania usahihi ni kwa Wabunge wa Tanganyika/Tanzania Bara kutoka wao katika Bunge la Muungano na kuunda Bunge lao makhsusi kwa shughuli zao za Tanganyika. Wasilete mambo yao ya Tanganyika kwenye Bunge la Muungano. Yawepo Mabunge matatu na Serikali Tatu kila Serikali/Bunge ishughulike na Mambo yake. Figisugisu Iwe Basi.
 
Nikimtafakari Kessy kiundani naona ana hoja tena nzito kuhusu serikali tatu ila ukimuuliza atakuruka 100m
 
Tunarudi kule kule tulikopakataa. Zanzibar ni nchi au sio nchi? katiba ya Warioba? Serikali mbili au tatu?......na kadhalika, na kadhalika!
ila ukimwambia katiba ya warioba ilipendekeza hayo atakuruka mita mia
 
Cha msingi ni kuangalia msimamo wa chama. Mtu haaminiki siku ya Kessy kubadili msimamo hakuna atakayejua bali mtaona tu akifanya msiyomzoea nayo. Ili chama kibadili msimamo mikutano na vikao vya kubadili sheria hufanyika na tafiti pia.

Hapa kila mmoja atajua kunakitu kinataka kubadilika. Huenda kuna vichocheo fulani ndivyo vinavyochagiza tabia hii ya Kessy. Huenda hivi vichocheo vikiwa mbali na yeye au vikiwekewa kinga ili visimfikie Kessy atabadili tabia yake.
 
Yan nikimuonaga uyu mzee nacheka to[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
sasa hivi watampigia makofi lakini ikiletwa Katiba ya Warioba wote wanageuka hawataki tena serikali 3
 
Back
Top Bottom