Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Awa wasi tuletee sasa nchi sio yao KMK

SUBIRI KIDOGO
 
yani ili dume la ng'ombe limeanza kunusa vindama vyake pale kunapotoka kinyesi na wanafurahia kweli kweli, alafu msije kulalamika tu mmebakwa.
 
Mimi Kama mwananchi mlipa Kodi nafikiri na kuona kabisa uchaguzi usifanyike..........

Tusichezee pesa bila sababu...... Kama vipi hiyo hela ya uchaguzi (nadhani Ni hela ndefu kidogo) ipigiwe hesabu Kila mwananchi agawiwe.......

Uchaguzi wa Nini na matokeo yanajulikana????????

Watu wanavunjwa miguu bila sababu kabla hata ya kipenga.....kikilia je?????

Wengineo wapo busy kujiwekea immunity ili wasiguswe baadaye..............

Magufuli anatosha na atatosha milele........

Kwanza Kuna excuse ya Corona, Nkurunzinza si tumeona yaliyomkuta????????? Sasa uchaguzi wa Nini????
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja ndugu watanzania tujipinge kisaikolojia kuwa muda wowote sheria inaweza badilishwa na kuongezewa muda wa uongozi wa Mh JPM. Mimi binafsi naunga hoja kwani kwa kipindi cha miaka mitano aliyokaa madarakani amefanya makubwa sana kwa hiyo naamini akipita muda wa kutosha atabadilisha sura ya tanzania na na nchi ya maziwa na asali wa watz wote sio watz wachache kama miaka iliyopita.
Mpeni chochote mnachotaka atawale hadi mwisho wa dunia Ila uzuri ALLAH huwa achezewi tunawatakia kila la kheri
 
Mafisadi wanaumia sana wakisikia magu kuongezewa muda ,sisi wengine tunao penda kuwaona mafisadi wakilia tunafarijika
 
Hii ni kwa mara nyingine hoja hii inaibuka. Wahenga huwa na misemo mingi ya kujihakiki "mzaha mzaha........."
Ajabu kumekua na majaribia ya kubadilisha vifungu vya katiba .
Kwa maoni yangu yote haya hayasemwi kwa bahati mbaya . Upo msingi nyuma yake. Ni swala la muda tu tutayasikia yakiwa hadharani.
Je vumi zote hizo zina maslahi mapana kwa taifa? Pengine ndiyo swala la kujiuliza na kutafakari . Kama hoja zote hizo zinatufaa katika kizazi hiki cha sasa au la.
Ni wajibu wetu kama watanganyika na wazanzibar kuwa na mjadala mpana zaidi bila kuwaachia wawakilishi wetu pekee.
Wasiwasi wangu inawezekana wale tuliowaamini wakashindwa kuona kile tunachokiona sisi kama raia wa kawaida.
 
Ujinga wote huu anauleta Ndugai ila Kuna watu wanamchora tu, afanye ujinga wake wote ila kuongeza muda wa uraisi hilo asahau kabisa wala asijidanganye
 
Ujinga wote huu anauleta Ndugai ila Kuna watu wanamchora tu, afanye ujinga wake wote ila kuongeza muda wa uraisi hilo asahau kabisa wala asijidanganye
Tatizo ni kwamba tulio wengi tunataka hilo litokee, so wengi vs wachache kazi kwelikweli.
 
Back
Top Bottom