"ATAKE ASITAKE"
Bunge linapotumia msemo wa Rais "ATAKE ASITAKE" linaweza kumaanisha moja au yote Kati ya haya:
1. Kumlazimisha Rais kufanya jambo asilopenda kufanya.
2. Kumlazimisha Rais asifanye analopenda kufanya.
3. Kumlazimisha Rais kuacha kuwa Rais kinyume na katiba, au kumlazimisha kuwa Rais kinyume na katiba.
Yote matatu hapo juu yakifanywa na chombo kingine utatumika msamiati mwingine.
Bunge kujiruhusu kuingiza msamiati wa ATAKE ASITAKE kwenye hansard ni kuanzisha utamaduni mpya wa:
1. Mhimili mmoja kuushambulia mhimili mwingine
2. Kumtisha Rais kuwa anaweza kulazimishwa kufanya au kutofanya kazi yake
3. Kuvichokoza vyombo vyenye wajibu wa kumlinda Rais wakiwamo wananchi ili vijiandae kumlinda Rais dhidi ya njama za kumlazimisha kufanya au kutofanya kazi yake.
4. Kuwalazimisha wananchi waharakishe jitihada za kuilinda katiba ili isitumiwe na watu kumlazimisha Rais "kutaka au kutotaka".
Mheshimiwa Rais bila kuingilia shughuli za bunge, asikalie kimya kauli hii.
Baba Askofu Bagonza