Hata mimi siungi mkono hayo maneno ya kisema "walking carcas", ni maneno ya kifedhuli, . Ndio maana hata kauli ya Zitto kwa wafuasi wa Magufuli nayo ni ya kishenzi sana kutolewa na kiongozi mkubwa wa chama cha siasa tena ambaye hakupata misukosuko mingi kama wale wa ChaDeMa.
Kwa nini haya mambo mimi na wewe tunakuwa na urahisi kuelewa, lakini kuna watu wanakuwa wagumu sana kuelewa?
Kuna siku nilikuwa namsikiliza Tundu Lissu, mtu ambaye kama kuna mtu ana haki kuisema vibaya serikali ya Magufuli, na kumtukana Magufuli, basi yeye ana haki hiyo.
N amahojiano haya yalikuwa baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi na kuhamia Ubelgiji. Hii ilikuwa wakati wa ziara ya Tundu Lissu Marekani.
Alilulizwa, nafikiri aliulizwa na Mubelwa Bandio, Mtanzania anayeishi Marekani na kufanya shughuli za habari.
Bandio alimuuliza Tundu Lissu, je una chuki binafsi na Magufuli?
Tundu Lissu alijieleza vizuri sana kwamba, hana matatizo binafsi na Magufuli, in fact kibinafsi wana mahusiano mazuri tu. Matatizo yake ni ya kitaasisi/kifalsafa zaidi.
Nikaona kwamba, katika hili, Tundu Lissu ameweza kuvuka kiunzi, amejua kutofautisha tofauti za kifalsafa na za kibinafsi. Na kwamba, licha ya ukweli kwamba inawezekana kapigwa risasi na serikali, ameweza ku focus kwenye mambo ya kitaasisi, hata kwenye hilo la kupigwa risasi.
Ndiyo maana hiyo point yako ya kwamba watu wanajibwatukia kuliko wale waliopata misukosuko zaidi ni ya muhimu sana.
Bootom line.
In economics, there is opportunity cost. Even if you have all the money in the world, you don't have all the time in the world.
So, you have to make choices.
Do you want to beat over a dead Magufuli in a non inpactful or even counterproductive way?
Or do you want to make institutional changes to prevent another Magufuli happening?
Watu wengi hawajaelewa hii hesabu.
Wwanaenda kwa jazba.