Kikubwa zaidi, mimi hata nikikosa busara, hekima na heshima, hilo halita contradict position yangu kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Kama Mungu huyo hayupo, kukosa busara, hekima na heshima kwangu si kitu cha kushangaza.
Ila, kama Mungu huyo yupo, kukosa busara, hekima na heshima kwa mtu yeyote ni kitu ambacho hakitakiwi kuwepo.
Kuna watu wengi hawana busara, hekima wala heshima.
Hilo linathibitisha Mungu huyo hayupo.
Lakini, nafikiri ni wachache sana wanaoweza kuelewa point hii.
Kwa hivyo, asiyeielewa namsamehe tangu awali.