Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Nimeiona picha ambayo nilipiga na Ally Sykes Muthaiga Club Nairobi mwaka wa 1989.
Miaka 37 imepita.
Ally Sykes amefariki miaka 13 iliyopita.
Bwana Ally alikuwa rafiki yangu na baba yangu lakini pia alikuwa mwalimu wangu yote kwa pamoja.
Hii picha nilipiga na camera ya bei rahisi sana mfano wa toy niliyonunua Alexandria mwaka wa 1988.
Picha hii ya 1989 nitaiweka hapa na picha hiyo hiyo baada ya matengenezo ya kisasa.
Pamoja na hayo napenda kuweka niliyoandika katika utangulizi wa kitabu cha Abdul Sykes kama shukurani zangu kwa Ally Sykes katika kunipa nyaraka zake zilizonisaidia kuandika kitabu kueleza historia ya TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kazi hii isingewezekana kama isingekuwa kwa msaada wa hali na mali nilioupata toka kwa Ally Sykes.
Ally Sykes alinipa wasaa wa kuzungumzanae kila nilipotaka, akanieleza madhila ya ukoloni pamoja na kuwa ni mtu wa shughuli nyingi.
Yeye hivi sasa anaendesha biashara yake toka ofisi yake iliyoko katikakati ya mji wa Dar es Salaam.
Aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes.
Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini.
Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani.
Kazi hii isingewezekana kama isingekuwa kwa msaada wa hali na mali nilioupata toka kwa Ally Sykes.
Ally Sykes alinipa wasaa wa kuzungumzanae kila nilipotaka, akanieleza madhila ya ukoloni pamoja na kuwa ni mtu wa shughuli nyingi.
Yeye hivi sasa anaendesha biashara yake toka ofisi yake iliyoko katikakati ya mji wa Dar es Salaam.
Aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes.
Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini.
Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ule wa harakati.
Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Julius Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru; nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA:
Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi Budohi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.
Baadaye nilipofanya utafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwamba tabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jalada kila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa.