Ally Sykes na Nyaraka za Harakati za Kupigania Uhuru wa Tanganyika

Huyu mzee Kila siku anakomaa na Hawa baby zake wa kariakoo sijui kina nani.....Man get the f^ck outta here. Don't nobody give a f^ck
 
Kwani umelazimishwa kusoma mada zake, kuna kila aina ya mada humu sio lazima ujue kwenye mada zake
Na kama umesoma na kukomenti, yes you do give fak
 
Kama hautojali tuelezee kidogo kuhusu hiki kisa mzee wetu
Mnyenz,
Rhodesia ilipokuwa inakaribia kupata uhuru wake Wazungu wengi wakawa wanauza nyumba zao
wanahama nchi kutafuta maisha kwengine.

Bwana Ally yeye hii akaona ni fursa kwake kwa hiyo akanunua nyumba Rhodesia na nyumba hii ilikuwa jirani na nyumba ya Ian Smith aliyekuwa Waziri Mkuu.

Bwana Ally anasema alipofika Harare kuikagua nyumba yake akaikuta nyumba imekuwa ''vandalised.''

Hili halikumpa shida.

Alileta mafundi wakaitengeneza nyumba na akatia samani mpya nyumba nzima.

Ian Smith alipotaka kujua hiyo nyumba nani kanunua akaambiwa ni mtu mmoja jina lake AK Sykes na kainunua kutoka London, yaani malipo yamefanywa na benki ya Uingereza.

Ian Smith na majirani wote waliobakia pale mtaani wakajua kuwa nyumba ile atakuja kukaa Mzungu mwenzao.

Sasa Ally Sykes alipokuwa nyumbani kwake asubuhi moja akiwa kwenye bustani yake anafanya kazi za kwenye bustani akamuona mtu na mkewe wanaingia.

Alikuwa Ian Smith kaingia kwenye ile nyumba baada ya kumuona mtu kwenye bustani.

Hii kwake Dmith ilikuwa nafasi kumsalimia jirani yake.

Ian Smith akamuuliza Ally Sykes, ''Where is your master?''
Ally Sykes alikuwa kachafuka miguu kwa tope la kumwagia maji maua yake katika bustani.

Bwana Ally akamkaribisha ndani Smith na mkewe.

Smith na mkewe ilikuwa kawaida yao kila asubuhi wanafanya mazoezi ya kutembea na wanapita mbele ya nyumba ya Ally Sykes.

Bwana Ally akawakaribisha ndani Ian Smith na mkewe na wakaa kwenye makochi Ally Sykes akawaletea kahawa na yeye akakaa kwenye sofa pembeni yao anawaangalia.

Smith akashtuka sana na kitendo kile cha ''Shamba Boy'' kukaa mbele yake na kwa hamaki akamtazama Ally Sykes usoni akamfokea, ''You get up.''

Ilikuwa utovu wa adabu mkubwa kwa Mwafrika kukaa kwenye sofa la Master wake.

Ian Smith yeye alikuwa anadhani Ally Sykes ni ''Shamba Boy,'' haiwezekani awe ndiye mwenye nyumba ile.
Yeye alikuwa anamsubiri mwenye nyumba Mzungu ateremke aje pale wasalimiane.

Ally Sykes hakunyanyuka aliendelea kukaa kisha akajitambulisha kwa Ian Smith, ''I am Ally Sykes the owner of this house.''

Ian Smith uso uilimbadilika akawa mwekundu.

Alikiweka chini kikombe cha kahawa akanyanyuka yeye na mkewe wakaondoka bila kutazama nyuma wala kusema lolote.

Hiki kisa huu si mwisho wake lakini nachelea kitakuwa kirefu sana na tusimame hapa.
 
Mpwimbe,
Siku zote toka enzi za ukoloni Tanganyika imekuwa secular.
Unasema kuwa unajua kuwa mimi naiona nchi kama Mfumo Kristo.

Kipi kinakufanya wewe uwe na fikra hiyo?
Je, wewe ungependa nchi iwe secular?
 
View attachment 3611222
View attachment 3611221

Nimeiona picha ambayo nilipiga na Ally Sykes Muthaiga Club Nairobi mwaka wa 1989.
Miaka 37 imepita.

Ally Sykes amefariki miaka 13 iliyopita.
Bwana Ally alikuwa rafiki yangu na baba yangu lakini pia alikuwa mwalimu wangu yote kwa pamoja.

Hii picha nilipiga na camera ya bei rahisi sana mfano wa toy niliyonunua Alexandria mwaka wa 1988.
Picha hii ya 1989 nitaiweka hapa na picha hiyo hiyo baada ya matengenezo ya kisasa.

Pamoja na hayo napenda kuweka niliyoandika katika utangulizi wa kitabu cha Abdul Sykes kama shukurani zangu kwa Ally Sykes katika kunipa nyaraka zake zilizonisaidia kuandika kitabu kueleza historia ya TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kazi hii isingewezekana kama isingekuwa kwa msaada wa hali na mali nilioupata toka kwa Ally Sykes.

Ally Sykes alinipa wasaa wa kuzungumzanae kila nilipotaka, akanieleza madhila ya ukoloni pamoja na kuwa ni mtu wa shughuli nyingi.

Yeye hivi sasa anaendesha biashara yake toka ofisi yake iliyoko katikakati ya mji wa Dar es Salaam.

Aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes.

Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini.

Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani.

Kazi hii isingewezekana kama isingekuwa kwa msaada wa hali na mali nilioupata toka kwa Ally Sykes.

Ally Sykes alinipa wasaa wa kuzungumzanae kila nilipotaka, akanieleza madhila ya ukoloni pamoja na kuwa ni mtu wa shughuli nyingi.

Yeye hivi sasa anaendesha biashara yake toka ofisi yake iliyoko katikakati ya mji wa Dar es Salaam.

Aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes.

Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini.

Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ule wa harakati.

Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Julius Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru; nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA:

Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi Budohi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.

Baadaye nilipofanya utafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwamba tabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jalada kila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa.

View attachment 3611224
Hizi dini zimeletwa na Wazungu (Ukristo) Waarabu (Islam). Na hazijawahi kuwa na mpango wowote kwenye marndeleo ya Waafrica zaidi ya kuwapumbaza.

Yaani mitume ni Mwaarabu (Mohammad) Mzungu (Yesu). Yaani tusali na kuandika Kiarab kwakua Mungu haelewi lugha nyingine zaidi ya Kiarab? 🚮
 
Waislam wameihujumu Africa kuliko hata mafisadi.
Very useless people kuwai kuwepo Africa.
Kikwete na genge lake la wakora walitukosesha rais bora sana, Dr. Salim Ahmed Salim; ulimwengu mzima ulitushangaa ile 2005.

Huyu huyu Kikwete alitukosesha naibu rais bora sana, Dr. Hussein Mwinyi; chaguo halisi la mgombea Magufuli na kufanya ukiritimba wa kumchomeka yule wa 0-2-0 from 7-4-6.

Akatuletea janga la bodaboda ili wamiliki uagizaji na uzalishaji wa bodaboda nchini. Over 80% wa majeruhi wote MOI kwa sasa ni vijana hao.

Bure kabisa🚮
 
Ian Smith akamuuliza Ally Sykes, ''Where is your master?''
Ally Sykes alikuwa kachafuka miguu kwa tope la kumwagia maji maua yake katika bustani.
Hapo unatupanga mzee wetu. Hizi ni hekaya kama zile za bikira Maria.

Ian Smith, kiongozi mkubwa wa nchi, mwenye access to all security agencies asijue ni nani atakuwa jirani yake?

All affluent neighborhoods za nchi za kibaguzi Europe, America, Asia, then Zimbabwe na mpaka sasa South Africa, Namibia; huwezi nunua or kupangisha nyumba bila vetting.

Usitupange.
 
Kikwete ndio Rais wa ovyoooooooo nchi hii imewahi kuwa naye.

NI kizee cha ovyoooooo sana
 
Sasa ni kwanini Waislam huwa wanataka masuala ya dini yagharamiwe na serikali?

Mfano, Kadh na OIC?
Mpwimbe,
Ilikuwa hivyo toka wakati wa ukoloni makadhi wakigharamiwa na serikali.
 
Wakoloni pia walikuwa na Macheif, turudishe Uchief??

Walikuwa na Classes za Wahindi, wazungu na watu weusi (Manamba) tuurudishe huo utaratibu??
 
Yoda,
Mtu wa kusema kuwa hizo nyaraka haziaminiki ni watafiti watakaozipitia na kuzikagua.
 
Mnyenz,
Rhodesia ilipokuwa inakaribia kupata uhuru wake Wazungu wengi wakawa wanauza nyumba zao
wanahama nchi kutafuta maisha kwengine.

Bwana Ally yeye hii akaona ni fursa kwake kwa hiyo akanunua nyumba Rhodesia na nyumba hii ilikuwa jirani na nyumba ya Ian Smith aliyekuwa Waziri Mkuu.

Bwana Ally anasema alipofika Harare kuikagua nyumba yake akaikuta nyumba imekuwa ''vandalised.''

Hili halikumpa shida.

Alileta mafundi wakaitengeneza nyumba na akatia samani mpya nyumba nzima.

Ian Smith alipotaka kujua hiyo nyumba nani kanunua akaambiwa ni mtu mmoja jina lake AK Sykes na kainunua kutoka London, yaani malipo yamefanywa na benki ya Uingereza.

Ian Smith na majirani wote waliobakia pale mtaani wakajua kuwa nyumba ile atakuja kukaa Mzungu mwenzao.

Sasa Ally Sykes alipokuwa nyumbani kwake asubuhi moja akiwa kwenye bustani yake anafanya kazi za kwenye bustani akamuona mtu na mkewe wanaingia.

Alikuwa Ian Smith kaingia kwenye ile nyumba baada ya kumuona mtu kwenye bustani.

Hii kwake Dmith ilikuwa nafasi kumsalimia jirani yake.

Ian Smith akamuuliza Ally Sykes, ''Where is your master?''
Ally Sykes alikuwa kachafuka miguu kwa tope la kumwagia maji maua yake katika bustani.

Bwana Ally akamkaribisha ndani Smith na mkewe.

Smith na mkewe ilikuwa kawaida yao kila asubuhi wanafanya mazoezi ya kutembea na wanapita mbele ya nyumba ya Ally Sykes.

Bwana Ally akawakaribisha ndani Ian Smith na mkewe na wakaa kwenye makochi Ally Sykes akawaletea kahawa na yeye akakaa kwenye sofa pembeni yao anawaangalia.

Smith akashtuka sana na kitendo kile cha ''Shamba Boy'' kukaa mbele yake na kwa hamaki akamtazama Ally Sykes usoni akamfokea, ''You get up.''

Ilikuwa utovu wa adabu mkubwa kwa Mwafrika kukaa kwenye sofa la Master wake.

Ian Smith yeye alikuwa anadhani Ally Sykes ni ''Shamba Boy,'' haiwezekani awe ndiye mwenye nyumba ile.
Yeye alikuwa anamsubiri mwenye nyumba Mzungu ateremke aje pale wasalimiane.

Ally Sykes hakunyanyuka aliendelea kukaa kisha akajitambulisha kwa Ian Smith, ''I am Ally Sykes the owner of this house.''

Ian Smith uso uilimbadilika akawa mwekundu.

Alikiweka chini kikombe cha kahawa akanyanyuka yeye na mkewe wakaondoka bila kutazama nyuma wala kusema lolote.

Hiki kisa huu si mwisho wake lakini nachelea kitakuwa kirefu sana na tusimame hapa.
😄

Ova
 
Gwapole,
Hakika nina furaha kila niandikapo historia ya wazee wangu na kisha msomaji akanifahamisha kuwa kaisoma.
Sasa kwanini kitabu cgmhako, hujakiita HISTORIA YA WAZEE WAKO WA KIISLAM wa GEREZANI???
 
Hapo unatupanga mzee wetu. Hizi ni hekaya kama zile za bikira Maria.

Ian Smith, kiongozi mkubwa wa nchi, mwenye access to all security agencies asijue ni nani atakuwa jirani yake?

All affluent neighborhoods za nchi za kibaguzi Europe, America, Asia, then Zimbabwe na mpaka sasa South Africa, Namibia; huwezi nunua or kupangisha nyumba bila vetting.

Usitupange.
Real,
Nyumba ile ilinunuliwa na A.K. Sykes kutoka benki iliyoko London.

Hawakuhangaika wakajua huyu ni Mzungu.

Nyumba ipo mpaka leo.
Sina sababu ya kusema uongo.
 
Back
Top Bottom