Ama kwa hakika maisha hayana maana kabisa

Ama kwa hakika maisha hayana maana kabisa

Kweli k
Poleni.
Maisha hayana guarantee, kwamba unachokiasisi lazima ukihitimishe, hapana.

Ukiamka na afya asubuhi, mshukuru Mungu na hako kakipande kauhai ulikojaaliwa siku hiyo kasherehekee kwa furaha na kumwaga upendo kwa wengine.

Maana haujui ya kesho, uhai ukishatoka ni milele na milele, ni infinity.
Umeongea ukweli mtupu mkuu,na hyo ndio maana ya maisha ,yaani ishi leo,"our main business is not to see what lies dimly at distance bt to do what seemly clea in our hands," dale Carnegie.
 
Pole sana bro. Maisha ni fumbo kubwa ambalo Wanadamu hatuwezi kulielewa kwa ukamilifu. Sulemani katika utajiri wake wote aliandika, Mhibiri 1:14 "Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo." La muhimu ni kumcha Mungu na kusalimisha maisha yetu mikononi mwa Mungu.
 
Poleni sana wafiwa. Ndio maana kila siku nawakumbusha acheni kujistress kulipa mamilioni kwenye shule za ENGLISH MEDIUM maisha yenyewe ndio hayo hayo. Haya sasa twende kazi, haraka sana kimbia watoe watoto wako shule za English Mediums warudishe Kayumba. Utakuja kunishukuru
kwani umeambiwa kiswahili medium hawapati ajali?
 
Tumemaliza ibada ya kumuaga rafiki yangu kipenzi, jamaa kamaliza MD moja ya chuo kikuu hapa jijini, kaja mtaani wakati anasubiria ajira, akaamua ajishikize kwenye Bajaj, Jana saa moja usiku kwa bahati mbaya akapata ajali baada ya bajaj yake kugongana na coaster.

Mwamba akalala mazima. Ooh maisha nini ni sasa? Harakati zote na ndoto zote zimekwisha. Its too sad indeed.
Sikiliza dogo! Sikiliza husia wa wazee waliopitia ujana na wakakumbana na changamoto kama hizo lakini hawakuambiwa ukweli! Ukizaliwa kwa familia ya Bahkaressa utarithi utajiri wa Bahkaressa! Ukizaliwa ukoo wa J.K. Nyerere utarithi jina na ushawishi wa kisiasa wa Nyerere! Ukizaliwa katika familia ambayo haina jina inabidi ujiongeze mababu na mabibi waliingia maagano yapi na mashetani ya mizimu na mashetani yaliyohusika tangu kutungwa mimba, kulelewa, kukuzwa, mpaka kujitambua na kupata kipato. Hayo maroho kama ni ya mashetani huwe na uhakika kuwa kama hutatambua uwepo wao watakuondoa duniani maana wanakuona una dharau! Kama ni ya Mungu katika Kristo, Mungu katika Kristo atakupa muda wa kumtafuta na kutumia maarifa uliyopata ili ujue uwepo wake! (Yakobo alifanya hivyo "Mwanzo 28: 10 - 22"). Sasa vijana wa siku hizi wakipata vijisenti wanapandisha mabega na kujiona wana akili kuliko wazee maskini walio mtaani! Sasa nawaambia nyie vijana msipojirudi mtaisoma namba! Hata uzao wa Bahkaressa inabidi wajitafute wajue ni mungu yupi baba yao aliwaweka wakfu!
 
Poleni sana wafiwa. Ndio maana kila siku nawakumbusha acheni kujistress kulipa mamilioni kwenye shule za ENGLISH MEDIUM maisha yenyewe ndio hayo hayo. Haya sasa twende kazi, haraka sana kimbia watoe watoto wako shule za English Mediums warudishe Kayumba. Utakuja kunishukuru
Ha ha ha ha ha ha wawaachie madoni.mtu hana hela anajilazimisha kusomesha shule hizo ili aonekane nae yumo.maujinga kabsa jitu linajinyima hata kula likalipe ada rubish kabsa
 
"Maisha hayana maana".."maisha hayana thamani".."maisha yamejawa na tanzia.."
 
Poleni sana , kuna siku nimeuliza mbona ajali ni nyingi sana Tanzania .

Je ni tatizo ni miundombinu , vyombo au madereva?
 
shakespeare anasema hivi katika kitabu mchezo wa McBeth:
"Life's but a walking shadow,
a poor player, That struts and frets his hour upon the stage,
And then is heard no more.
It is a tale Told by an idiot,
full of sound and fury, Signifying nothing.”
na pia akasema ' when sorrow comes, not a single spy ,but in batallions'. Ndio maisha yalivyo. Matatizo yakija kwenye maisha yako, huwa yanafuatana.
 
😄😄 Mkuu umeamua tu kunipinga bt ndio uhalisia,wanasema ishi leo na usijistress kwa mambo yaliyopita au yajayo ambayo huyaoni.
Ni kwel kabisa ndugu yangu. Yan hapa ungeniona mwenzako ndio ninavyoishi. Yan huwa sijipi stress. Yalio ndani ya uwezo nafanya twna nafanya kweli, yalio nje uanajioa tabu ya nini? 😂
 
Kila mtu litampata kwa wakati wake yeye ametangulia nasi tutafuata.
 
Back
Top Bottom