Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kubali na kutambua kuwa maumivu, mateso na kifo ni marafiki wa kweli. Yakitokea maumivu na mateso yakumbatie. Kuwa tayari kufa wakati wowote na ufurahie maisha.
Sio baadhi ya madereva tu, Watanzania wote kwa ujumla hawazingatii sheria za barabarani.Today tukiwa tuna enda mishe mishe asbh Kuna jamaa tulimpakia mtu MZIMA.
Alikua mkimya Sana gafla Kuna bodaboda alifanya faulo..
Jamaa akaanza kuzungumza akasema NIMEWAI KUUA MTU KWENYE AJARI YA BARABARANI..
ILIKUA ANATOKA DAR WANAENDA BUKOBA NA PRIVATE CAR YEYE AKIWA DEREVA WALIPO FIKA KAHAMA NTATOLEA MFANO WA ENEO WALIPO PATIA AJAR NI KAMA HAPO MAENEO YA JITEGEMEE JKT..
yeye alikua highway speed bodaboda akiwa amebeba mishikaki akakatiza gafla ku cross barabara... Tena bodaboda ilikua imetoka kuchukua drip za uchungu kuwaisha ili mama akajifungue walipo fikishwa kituo Cha afya wakaambiwa Hawa si wametoka hapa muda si mrefu mmoja karudishwa akiwa MAITI.
Mzee yaan miundombinu yetu Bado sio rafiki pia na madereva baadhi hawazingatii Sheria za barabarani
Mkuu na wewe ni mpenzi wa plays za huyu jamaana pia akasema ' when sorrow comes, not a single spy ,but in batallions'. Ndio maisha yalivyo. Matatizo yakija kwenye maisha yako, huwa yanafuatana.
Kwa kua kuna maisha ng'ambo ya bahari,ni walalao katika bwana,siku moja tutakutana nao!Tumemaliza ibada ya kumuaga rafiki yangu kipenzi, jamaa kamaliza MD moja ya chuo kikuu hapa jijini, kaja mtaani wakati anasubiria ajira, akaamua ajishikize kwenye Bajaj, Jana saa moja usiku kwa bahati mbaya akapata ajali baada ya bajaj yake kugongana na coaster.
Mwamba akalala mazima. Ooh maisha nini ni sasa? Harakati zote na ndoto zote zimekwisha. Its too sad indeed.
Kwaio mkuu 😊 unataka kusema Kama ukipata nafasi vaa vizuri,kula vizuri, kunywa vizuri enjoy.Maisha ni Leo mkuu , future ni sasa . Live life to the fullest
Ni ukweli mtupu huku kwetu kutoka asbh na kurudi salama ni Kama muujiza tu.Sio baadhi ya madereva tu, Watanzania wote kwa ujumla hawazingatii sheria za barabarani.
Mfano mdogo ni kwenye zebra crossing tu, Usiku ndio kwanza wala hawajali kama kuna zebra magari yanapita hapo speed kali.
Bodaboda wao ndio kama zebra crossing haiwahusu kabisa, Yani iwe mchana au usiku, Hata wakikuta imewaka taa nyekundu wao wanavuta mafuta tu speed ..
Ila kwa wenzetu hata usiku wa manane umefika zebra crossing na hamna hata mtu mmoja anaye vuka, Lazima usimame.
Acha mawazo ya kimasikiniPoleni sana wafiwa. Ndio maana kila siku nawakumbusha acheni kujistress kulipa mamilioni kwenye shule za ENGLISH MEDIUM maisha yenyewe ndio hayo hayo. Haya sasa twende kazi, haraka sana kimbia watoe watoto wako shule za English Mediums warudishe Kayumba. Utakuja kunishukuru
Bajaji ya watu 4 wanapakizwa watu 6! na mizigo, hapo ajali, majeruhi na kifo nje njeDah so sad Mimi mwenyewe dereva bajaj sikuhizi ajali zimekuwa NYINGI Sana yani
Na hapo unakuta ni Bajaji ya watu wanne ila wanapakia hadi watu sita.Just imagine an MD riding a tricycle as a full-time job, it's very frustrating as a parent kwa kweli. Kwamba.....dah inaumiza sana!
mdau we acha kabisa , watu tunajua mavituz sema pa kuyatemea ndio changamoto+muda. Huyo jamaa kwenye huo mchezo wa kuigiza wa macbeth alitisha sana. Waingereza wenyewe wanamhusudu balaa.Mkuu na wewe ni mpenzi wa plays za huyu jamaa
Nondo nzuri Sana hiyo😅Apumzike kwa amani, nakumbuka mwakasege alisema "kimwili ishi kama hauji kufa ila kiroho jiandae kama unakufa leo"
AiseeWaafrika hasa watanzania wana kufa sana kutokana na ujinga, uzembe na upumbavu.
Kusafiri katika barabara za Tanzania ni HATARI ya kuweza kupoteza uhai wako muda wowote.
Mijitu inaendesha vyombo vya usafiri kama mapanya🐀 yanayo kimbizana darini.
Mijitu inajazwa kwenye public buses: daladala, Hiace, Noah, mwendokasi n.k kama magunia ya viazi 🥔 .
Mibodaboda barabarani kama misafara ya Siafu 🐜
Kuishi Africa tu, Ni hatari kwa uhai wako na Life expectancy yako kwa ujumla.
Exactly,na sio ukipata nafasi,nafasi siku zote ipo,ni wajibu kuchagua.Kwaio mkuu 😊 unataka kusema Kama ukipata nafasi vaa vizuri,kula vizuri, kunywa vizuri enjoy.
Na hapo unakuta ni Bajaji ya watu wanne ila wanapakia hadi watu sita.
ndo maisha yalivo mkuuInasikitisha sana, taifa linatumia gharama kubwa sana kusaidia watu wake waende shule, mwisho wake hizo ajira hakuna. MD kiuhalisia kabisa hawezi kujiajiri, ni ngumu sana coz mtaji wake sio mchezo. Sijui tunaenda wapi aisee.