Kwamba Rwanda wanaweza kuwashinda Afrika Kusini, taifa ambalo linatengeneza kila aina ya silaha ya kivita hapa duniani, kuanzia Infantry Fighting Vehicles, Tanks, APCs, Attack Helicopters, Ballistic Missiles, Fighter Jets, UAVs and Heavy Artillery. Wanawauzia silaha nzito mataifa kama Ujerumani, India, UAE, Philippines na Kuwait. Mashabiki wanaposema kwamba M23 wanaweza kuvishinda vikosi vya Afrika Kusini, Malawi, Tanzania na Congo huwa nashangaa na napata ukakasi sana.
Kiuhalisia M23 wanaweza kusumbua kwa muda kwasababu wanayafahamu mazingira (Terrain) vizuri kuliko wageni na wanaungwa mkono kisiasa na raia wao (Political Support). Wanajeshi wanaweza kudhurika kwa muda mfupi, kwasababu mpaka sasa wanapambana vita ndogo, Asymmetric Warfare and Sporadic Engagement, lakini endapo vita itakuwa kubwa na kurefushwa sidhani kama M23 wanaweza kupambana hata mwezi.
Jambo ambalo watu wengi hawalifahamu ni hili, silaha za M23 na waasi wengine zinatoka kwenye BLACK-MARKET nchini Ukraine, Libya, na Sudan, kupitia Central African Republic, South Sudan, Uganda na Rwanda hadi Congo. Hivyo mbali na huu mgogoro kuwa kuonesha kwamba ni wa kisiasa, kiuhalisia ni mgogoro wa kiuchumi. Watu wanatajirika kwa kuuza silaha, kutoa mafunzo na kueneza ushawishi. Endapo itatokea vita kubwa, basi moja ya wanufaika watakuwa ni Afrika Kusini.
Tofauti na mwaka 1998, The Great Congo War, ambapo Mzee Nelson Mandela alikuwa upande wa General Paul Kagame, endapo itatokea vita kubwa kipindi hiki na kupelekea nchi kama Rwanda na Uganda kuhusika, basi Afrika Kusini itahusika moja kwa moja. Watapewa kandarasi za kijeshi na serikali ya Congo, kuanzia kuuza silaha na kutoa mafunzo ya kijeshi, jambo ambalo nadhani hakuna taifa la Afrika linawashinda Afrika Kusini. Itakuwa ni biashara kubwa yenye faida nyingi mno kwa makampuni ya silaha ya Afrika Kusini.
Zaidi ya hayo, Congo inaweza kufanya kama ilivyofanya kwa Zimbabwe baada ya majeshi yake kuiokoa serikali ya Raisi Laurent Kabila. Zimbabwe walipewa Mineral Concessions (Mikataba ya madini) yenye thamani ya trilioni nyingi. Ukisoma The UN Mapping Report iliyoandaliwa na Marehemu Dr Koffi Anan, serikali ya Zimbabwe ililipwa na Congo madini yenye thamani ya USD 5 Billion, ambazo ni sawa na TSZ 11 Trillion. Sasa kipindi hiki cha Ramaphosa, Afrika Kusini watapewa madili makubwa mno.
JAMBO LA KUJIULIZA:
General Kagame anataka nini haswa nchini Congo ilhali watusi hawako Congo peke yake. Tanzania, Uganda na Burundi zote zina watutsi, lakini kwanini hataki kujishughulisha nao ? Kama ni kupigania haki za watutsi, hivi akimaliza Congo, nini kitamzuia kupigania haki za watutsi nchini Burundi, Uganda au Tanzania? Hii ni michezo ya hatari mno ambayo endapo watutsi hawatakubali kubadilika inaweza ikaja kuwaumiza vibaya hata wao huko mbeleni.
Jambo la mwisho, hata kama General Kagame na Raisi Museveni wanaungwa mkono na mataifa kama Marekani, Uingereza na Israel katika kuivuruga Congo, hiki kipindi ni kibaya mno kwao kutaka kuanzisha vita kubwa kama ile ya 1998. Nyakati zimebadilika mno kwa Afrika, zile nguvu alizokuwa nazo Marekani na Uingereza za kupindua serikali za Afrika kirahisi tu bila madhara ya vita za muda mrefu hazipo tena. Hebu angalia kule Niger, Mali, Burkina-Faso, Libya na Sudan, ambako mpaka sasa kuna vita kubwa zinapiganwa.
Makundi hatari ya Kijeshi, Private Military Contractors (PMCs), kutoka Urusi, Israel na Marekani yanafanya kazi mbaya mno hapa Afrika yakitanua ushawishi. Watu kama Raisi Kagame na Museveni hawatanufaika kwa chochote kwa kuanzisha vita kubwa kipindi hiki. Hebu zingatia hizi sababu:
Mosi, kwasababu vita vitayahusisha mataifa makukwa duniani na vitakuwa virefu kiasi cha kuvuruga uchumi wa Rwanda, hata kupelekea machafuko ya kisiasa. Angalia kule Sudan, walianza na Al Bashir ila mpaka sasa Urusi, UAE, Saudi Arabia na Iran wanapambana vibaya mno na kuigeuza nchi shamba la bibi. Sidhani kama Rwanda au Uganda, hata kama wanaungwa mkono na Marekani wanaweza kupambana na magenge ya wahuni kama WEGNER GROUP bila kupata madhara.
Pili, kipindi hiki cha utandawazi huwezi kuficha chochote kinachoendelea. Isreal na nguvu yake kubwa ya PROPAGANDA, paka kufika February 2024, ameshashindwa kabisa vita ya PROPAGANDA dhidi ya Hamas. Kule TikTok, #FreePalestine ilikuwa na Views 5 billion, huku #IstandwithIsrael ikiwa na Views 125 million. Jambo lolote litakaloendelea Congo haliwezi kufichwa kama ilivyokuwa mwaka 1998-2003.
Tatu, Afrika Kusini, baada ya International Court of Justice (ICJ) Stunt ya kufungua kesi dhidi ya Israel kuwatetea wapalestina, jambo ambalo mataifa mengi yalikuwa yanaogopa na hadi kudhani haliwezekani, wamejijenga mno kidiplomasia hasahasa kwa wafuasi wa siasa za mlengo wa kushoto, ambao wengi ni mataifa ya barani ASIA na AMERIKA KUSINI. Hivyo endapo itatokea vita, sidhani kama Rwanda, Uganda na M23 wataweza kabisa kuishinda nguvu ya KIDIPLOMASIA ya Afrika Kusini, taifa ambalo liko BRICS na G20.
Bahati mbaya sana, Tanzania siku hizi inatawaliwa na wahuni. Tofauti na mwaka 1998 ambapo tulikuwa wasuluhishi wa ugomvi wa Congo, kipindi hiki watawala wanatamani kuchuma yaliyomo Congo kama ambavyo wengine wanachuma. Hivyo ikitokea vita kwamba Rwanda na Uganda wanavamia Congo, basi ni dhahiri kabisa KIDIPLOMASIA itakuwa mbaya kwake kwasababu mataifa mengi ya SADC watavurugana naye sana. Zile Military Escapades za Mozambique hazitawasaidia.
Sidhani kama litakuwa jambo la afya kwa nchi kama Rwanda, kutengwa KIDIPLOMASIA na mataifa ya SADC, huku taifa kubwa na lenye ushawishi kama Afrika Kusini likiwa linapiga Propaganda dhidi yako. Rwanda atafurukuta weeh, lakini sidhani kama atafika mbali na vita sizizo na msingi.
Nne, Rwanda ina udhaifu mmoja mkubwa, IT HAS NO POWERFUL AIRFORCE, kitu ambacho kiliwafanywa wapigwe vibaya mno na Zimbabwe mwaka 1998. Hata mwaka 2013, vikosi vya MUNISCO Intervention Brigade viliwashinda M23 waliokuwa wanasaidiwa na Rwanda kwasababu ya Attack Helicopters za Afrika Kusini. Huu udhaifu sidhani kama Rwanda ameurekebisha, ila endapo watasema hii vita iwe kubwa sidhani kama hawatakutwa na madhara.
NAMALIZIA:
Vinchi vya ukanda wetu ni masikini kwelikweli, badala ya kufikiri ni jinsi gani tunaweza kuishi kwa kuvumuliana vimeamua kutunisha msuli. Sidhani kama huu mwisho utakuwa mzuri. Hapa, Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi, tunachezeshwa ngoma nzito na Afrika Kusini akiwa na washirika wake bila kujua. Amini nakwambia, taifa kama Afrika Kusini ambalo liko BRICS na G20 haliwezi kuja mpaka Congo kwasababu za kibanadamu bali kimaslahi na kidiplomasia.
Hivyo mpaka akawepo hapa, lazima amezungumza na washirika wake wakubwa wa kiuchumi na kuwahakikishia kwamba uwepo wake hapa hauwezi kuleta madhara, zaidi zaidi faida kwao. Sisi watanzania, wanyarwanda na wakongo, we're just pawns in a very long game.