Ama M23 wataiteka Goma au majeshi ya SADC yataingia Ikulu Kigali

Ama M23 wataiteka Goma au majeshi ya SADC yataingia Ikulu Kigali

Humzidi DRC matumizi kwenye silaha,akiweka watu elfu 3 mpakani,elfu 5 katikati ya Rwanda hamtakaa hapo,mtakimbilia Tanzania tuwafuge Kama ng'ombe
Hata ukimuuliza Rwanda ina silaha gani sophisticated hawezi kukupa jibu kamili.
Mama Kizimkazi kipindi ameidhinisha TPDF kwenda DRC chini ya SADC alisema jeshi limeenda kwa mwamvuli wa SADC ila muongozo hutolewa na MONUSCO.
Kama TPDF ingeenda kwa mwamvuli wa SADC na kuwa na amri yake kama Mozambique DRC kungeongeleka mengine.
Itafakari hiyo kauli.
 
Tactics za kijeshi za jamii forum ziko more advanced kuliko kile kinachotokea on battle field mambo uwa ayako hivyo jeshi linaongozwa na amri pamoja na permission za kuengage sio ukijisikia kulusha bomu unalusha popote mambo ayako hivyo.
Hahahaha dah namsaidiaga mr kipondi cha mtihan kukesha nae
Huwa ni mtu wa kuaoma kwa discussion so namimi napitia pitia baa da e namuuliza maswali kwa kutumia hizo desa
Protocol ni nyingi sana mpaka risasi ya kwanza kupigwa
Sio hovyo hovyo kama “watoto wa mbwa”
Aisee sio rahisi vitani
Maana unaemwendea anajua unakuja
 
Wewe unaota Ndoto za mchana, Kigali hauijui hata kidogo. hao M23 wenyewe Kishekedi na Majeshi yake yooote, Akisaidiwa na Jeshi la Burundi, Akisaidiwa na Kundi zima la Wazalendo ambalo ni mkusanyiko wa makundi ya wapiganaji yapatayo 120, Ongezea kikosi kutoka SA, Ongezea Kikosi kutoka Malawi, Ongezea Kikosi kutoka TZ na Jeshi zima la Monusco hao wote wameshindwa hata kuchukua mita 100 za M23 halafu eti wataenda Kigali, you dont know what you are saying.
Kwa taarifa yako sasa, vijana wenu wanateketezwa kila kukicha, jana tu APC mbili za TZ zimeunguzwa na waliokuwemo ndani hakutoa mtu. Sasa kama M23 inawatoa kamasi ndio waende Kigali!! Hakuna kitu kama hicho.
Jamaa hata muuza kahawa hakufikii
 
Hata ukimuuliza Rwanda ina silaha gani sophisticated hawezi kukupa jibu kamili.
Mama Kizimkazi kipindi ameidhinisha TPDF kwenda DRC chini ya SADC alisema jeshi limeenda kwa mwamvuli wa SADC ila muongozo hutolewa na MONUSCO.
Kama TPDF ingeenda kwa mwamvuli wa SADC na kuwa na amri yake kama Mozambique DRC kungeongeleka mengine.
Itafakari hiyo kauli.
Mkuu chambua hapa vizuri napenda hya mambo
 
Hao ndugu zetu walioenda huko chini ya. Mwavuli wa sadc lakin amri ni munsco kama sijakosea
Kwa habari nilizopata na kwa uelewa nilionao kuhusu hili jambo vikosi vya kulinda amani vya SADC vilivyoenda DRC vikijumlisha Malawi,S.A na Tanzania viko chini ya Force intervention brigade ya MONUSCO peace keeping mission.
Na kwasababu pale DRC peacekeeping organization inayoongoza ulindaji amani ni MONUSCO,hivyo hata vikosi vya SADC wanapokea maelekezo toka kwa MONUSCO kitengo cha FIB wapi washambulie na nini wafanye.
Amri haijasimama kwao asilimia mia kama ilivyo Msumbiji vikosi vya SADC vina amri yao kikamilifu.
Hiyo ni kwa mujibu wa mama Samia mkuu.
Japo TPDF pia wapo ndani ya MONUSCO na wana brigade yao ya Tanzbaat ndani ya kikosi cha UN peacekeeping ambacho wao kazi yao ni kulinda tu amani no engagement ila FIB ndio kunaruhusiwa kufanya engagement.
Kama nimekosea mtanirekebisha.
 
Acha war propaganda unadanganya watu , APC sio land cruiser au vitz iunguzwe kirahisi hivyo na watu wasitoke, kawadanganye wasiojua
Labda wamefanikiwa kuzidamage
Na habari zimefika kuhusu hilo shambulio hakuna vifo ni askari mmoja wa JWTZ na raia mmoja wamepata minor injury na hakuna death threat.
Inamaana hako kabomu hakana nguvu.
 
Kwa habari nilizopata na kwa uelewa nilionao kuhusu hili jambo vikosi vya kulinda amani vya SADC vilivyoenda DRC vikijumlisha Malawi,S.A na Tanzania viko chini ya Force intervention brigade ya MONUSCO peace keeping mission.
Na kwasababu pale DRC peacekeeping organization inayoongoza ulindaji amani ni MONUSCO,hivyo hata vikosi vya SADC wanapokea maelekezo toka kwa MONUSCO kitengo cha FIB wapi washambulie na nini wafanye.
Amri haijasimama kwao asilimia mia kama ilivyo Msumbiji vikosi vya SADC vina amri yao kikamilifu.
Hiyo ni kwa mujibu wa mama Samia mkuu.
Japo TPDF pia wapo ndani ya MONUSCO na wana brigade yao ya Tanzbaat ndani ya kikosi cha UN peacekeeping ambacho wao kazi yao ni kulinda tu amani no engagement ila FIB ndio kunaruhusiwa kufanya engagement.
Kama nimekosea mtanirekebisha.
Kwa maana hiyo kuna peace keeper na wanaoengage
Kuna ambush hizo anga sio poa Mungu awalinde
 
Kwamba Rwanda wanaweza kuwashinda Afrika Kusini, taifa ambalo linatengeneza kila aina ya silaha ya kivita hapa duniani, kuanzia Infantry Fighting Vehicles, Tanks, APCs, Attack Helicopters, Ballistic Missiles, Fighter Jets, UAVs and Heavy Artillery. Wanawauzia silaha nzito mataifa kama Ujerumani, India, UAE, Philippines na Kuwait. Mashabiki wanaposema kwamba M23 wanaweza kuvishinda vikosi vya Afrika Kusini, Malawi, Tanzania na Congo huwa nashangaa na napata ukakasi sana.

Kiuhalisia M23 wanaweza kusumbua kwa muda kwasababu wanayafahamu mazingira (Terrain) vizuri kuliko wageni na wanaungwa mkono kisiasa na raia wao (Political Support). Wanajeshi wanaweza kudhurika kwa muda mfupi, kwasababu mpaka sasa wanapambana vita ndogo, Asymmetric Warfare and Sporadic Engagement, lakini endapo vita itakuwa kubwa na kurefushwa sidhani kama M23 wanaweza kupambana hata mwezi.

Jambo ambalo watu wengi hawalifahamu ni hili, silaha za M23 na waasi wengine zinatoka kwenye BLACK-MARKET nchini Ukraine, Libya, na Sudan, kupitia Central African Republic, South Sudan, Uganda na Rwanda hadi Congo. Hivyo mbali na huu mgogoro kuwa kuonesha kwamba ni wa kisiasa, kiuhalisia ni mgogoro wa kiuchumi. Watu wanatajirika kwa kuuza silaha, kutoa mafunzo na kueneza ushawishi. Endapo itatokea vita kubwa, basi moja ya wanufaika watakuwa ni Afrika Kusini.

Tofauti na mwaka 1998, The Great Congo War, ambapo Mzee Nelson Mandela alikuwa upande wa General Paul Kagame, endapo itatokea vita kubwa kipindi hiki na kupelekea nchi kama Rwanda na Uganda kuhusika, basi Afrika Kusini itahusika moja kwa moja. Watapewa kandarasi za kijeshi na serikali ya Congo, kuanzia kuuza silaha na kutoa mafunzo ya kijeshi, jambo ambalo nadhani hakuna taifa la Afrika linawashinda Afrika Kusini. Itakuwa ni biashara kubwa yenye faida nyingi mno kwa makampuni ya silaha ya Afrika Kusini.

Zaidi ya hayo, Congo inaweza kufanya kama ilivyofanya kwa Zimbabwe baada ya majeshi yake kuiokoa serikali ya Raisi Laurent Kabila. Zimbabwe walipewa Mineral Concessions (Mikataba ya madini) yenye thamani ya trilioni nyingi. Ukisoma The UN Mapping Report iliyoandaliwa na Marehemu Dr Koffi Anan, serikali ya Zimbabwe ililipwa na Congo madini yenye thamani ya USD 5 Billion, ambazo ni sawa na TSZ 11 Trillion. Sasa kipindi hiki cha Ramaphosa, Afrika Kusini watapewa madili makubwa mno.

JAMBO LA KUJIULIZA:
General Kagame anataka nini haswa nchini Congo ilhali watusi hawako Congo peke yake. Tanzania, Uganda na Burundi zote zina watutsi, lakini kwanini hataki kujishughulisha nao ? Kama ni kupigania haki za watutsi, hivi akimaliza Congo, nini kitamzuia kupigania haki za watutsi nchini Burundi, Uganda au Tanzania? Hii ni michezo ya hatari mno ambayo endapo watutsi hawatakubali kubadilika inaweza ikaja kuwaumiza vibaya hata wao huko mbeleni.

Jambo la mwisho, hata kama General Kagame na Raisi Museveni wanaungwa mkono na mataifa kama Marekani, Uingereza na Israel katika kuivuruga Congo, hiki kipindi ni kibaya mno kwao kutaka kuanzisha vita kubwa kama ile ya 1998. Nyakati zimebadilika mno kwa Afrika, zile nguvu alizokuwa nazo Marekani na Uingereza za kupindua serikali za Afrika kirahisi tu bila madhara ya vita za muda mrefu hazipo tena. Hebu angalia kule Niger, Mali, Burkina-Faso, Libya na Sudan, ambako mpaka sasa kuna vita kubwa zinapiganwa.

Makundi hatari ya Kijeshi, Private Military Contractors (PMCs), kutoka Urusi, Israel na Marekani yanafanya kazi mbaya mno hapa Afrika yakitanua ushawishi. Watu kama Raisi Kagame na Museveni hawatanufaika kwa chochote kwa kuanzisha vita kubwa kipindi hiki. Hebu zingatia hizi sababu:

Mosi, kwasababu vita vitayahusisha mataifa makukwa duniani na vitakuwa virefu kiasi cha kuvuruga uchumi wa Rwanda, hata kupelekea machafuko ya kisiasa. Angalia kule Sudan, walianza na Al Bashir ila mpaka sasa Urusi, UAE, Saudi Arabia na Iran wanapambana vibaya mno na kuigeuza nchi shamba la bibi. Sidhani kama Rwanda au Uganda, hata kama wanaungwa mkono na Marekani wanaweza kupambana na magenge ya wahuni kama WEGNER GROUP bila kupata madhara.

Pili, kipindi hiki cha utandawazi huwezi kuficha chochote kinachoendelea. Isreal na nguvu yake kubwa ya PROPAGANDA, paka kufika February 2024, ameshashindwa kabisa vita ya PROPAGANDA dhidi ya Hamas. Kule TikTok, #FreePalestine ilikuwa na Views 5 billion, huku #IstandwithIsrael ikiwa na Views 125 million. Jambo lolote litakaloendelea Congo haliwezi kufichwa kama ilivyokuwa mwaka 1998-2003.

Tatu, Afrika Kusini, baada ya International Court of Justice (ICJ) Stunt ya kufungua kesi dhidi ya Israel kuwatetea wapalestina, jambo ambalo mataifa mengi yalikuwa yanaogopa na hadi kudhani haliwezekani, wamejijenga mno kidiplomasia hasahasa kwa wafuasi wa siasa za mlengo wa kushoto, ambao wengi ni mataifa ya barani ASIA na AMERIKA KUSINI. Hivyo endapo itatokea vita, sidhani kama Rwanda, Uganda na M23 wataweza kabisa kuishinda nguvu ya KIDIPLOMASIA ya Afrika Kusini, taifa ambalo liko BRICS na G20.

Bahati mbaya sana, Tanzania siku hizi inatawaliwa na wahuni. Tofauti na mwaka 1998 ambapo tulikuwa wasuluhishi wa ugomvi wa Congo, kipindi hiki watawala wanatamani kuchuma yaliyomo Congo kama ambavyo wengine wanachuma. Hivyo ikitokea vita kwamba Rwanda na Uganda wanavamia Congo, basi ni dhahiri kabisa KIDIPLOMASIA itakuwa mbaya kwake kwasababu mataifa mengi ya SADC watavurugana naye sana. Zile Military Escapades za Mozambique hazitawasaidia.

Sidhani kama litakuwa jambo la afya kwa nchi kama Rwanda, kutengwa KIDIPLOMASIA na mataifa ya SADC, huku taifa kubwa na lenye ushawishi kama Afrika Kusini likiwa linapiga Propaganda dhidi yako. Rwanda atafurukuta weeh, lakini sidhani kama atafika mbali na vita sizizo na msingi.

Nne, Rwanda ina udhaifu mmoja mkubwa, IT HAS NO POWERFUL AIRFORCE, kitu ambacho kiliwafanywa wapigwe vibaya mno na Zimbabwe mwaka 1998. Hata mwaka 2013, vikosi vya MUNISCO Intervention Brigade viliwashinda M23 waliokuwa wanasaidiwa na Rwanda kwasababu ya Attack Helicopters za Afrika Kusini. Huu udhaifu sidhani kama Rwanda ameurekebisha, ila endapo watasema hii vita iwe kubwa sidhani kama hawatakutwa na madhara.

NAMALIZIA:
Vinchi vya ukanda wetu ni masikini kwelikweli, badala ya kufikiri ni jinsi gani tunaweza kuishi kwa kuvumuliana vimeamua kutunisha msuli. Sidhani kama huu mwisho utakuwa mzuri. Hapa, Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi, tunachezeshwa ngoma nzito na Afrika Kusini akiwa na washirika wake bila kujua. Amini nakwambia, taifa kama Afrika Kusini ambalo liko BRICS na G20 haliwezi kuja mpaka Congo kwasababu za kibanadamu bali kimaslahi na kidiplomasia.

Hivyo mpaka akawepo hapa, lazima amezungumza na washirika wake wakubwa wa kiuchumi na kuwahakikishia kwamba uwepo wake hapa hauwezi kuleta madhara, zaidi zaidi faida kwao. Sisi watanzania, wanyarwanda na wakongo, we're just pawns in a very long game.​
 
Kwa maana hiyo kuna peace keeper na wanaoengage
Kuna ambush hizo anga sio poa Mungu awalinde
Ndio mkuu kuna walinda amani na neutralizer.
Ila MONUSCO mwaka huu wanatarajiwa kuondoka na wameshapunguza vikosi nahisi vikosi pekee vitakavyobaki ni vya SADC.
Na SADC hawana kitengo cha peace keeping wao wana kitengo kimoja tu cha intervention.
 
Israel inayofichwa nyuma ya USA na UK??
Hao wavaa kobazi anaopigana nao wanadunduliza silaha ila yeye akiishiwa silaha USA ishapaki manowari ikimpea silaha na pesa za vita.
Israel bila USA na Westerns ni kama bumunda tu.
stor za madrasa
 
Back
Top Bottom