Amani bila haki ni sawa na kusitisha vurugu kwa muda tu

Amani bila haki ni sawa na kusitisha vurugu kwa muda tu

Joined
Dec 9, 2025
Posts
89
Reaction score
213
1767172389232.png

​


Pindi ambapo migogoro inakomeshwa juu juu bila kushughulikia chanzo chake kama dhuluma, ukandamizaji, utekaji, mauaji, ubaguzi, umasikini au kunyimwa haki, hali ya utulivu inayopatikana huwa ya muda mfupi tu. Watu wanaweza kunyamazishwa au kuchoka kupigana, lakini maumivu, hasira na kutoridhika vinaendelea kujengeka chini kwa chini ndani yao.

Hivyo, bila haki, “amani” huwa ni kusitisha mapigano kwa muda, siyo suluhisho la kweli. Mwisho wake, vurugu hurudi tena, mara nyingi kwa nguvu zaidi, kwa sababu sababu halisi za mgogoro hazikuwahi kutatuliwa, ndiyo maana watu hawachoki kupanga tarehe za makutano wakiamini walichokipoteza wakati uliopita si la kunyamazia na tayari hawana uoga wa makombora, risasi wala majeshi yanayotapakaa nje na hata dhihaka ya kuambiwa wanapiga kelele mitandaoni bado wanaona ni nguvu ya mapambano yao kutambulika ulimwenguni

Ni kama kundi la wale walio wengi wanatambua hatua za mbele za wadhalimu wasio na aibu wakija na falsafa za kutafuta wakumtupia lawama na si wao kukubali kuwajibishwa kwa makosa yao ya ushetani.

Guys; HAKI KWANZA KISHA AMANI ITAPATIKANA TUSILAZIMISHE AMANI BILA HAKI
 
kilichootekea Leo kwenye mpira wa taifa stars vs Morocco kinaonyesha njisi Gani haki ya mtu ikiminywa huwa inauma sana...turudi wa wale masheik ubwabwa wanaosema Amani kwanza haki badae...ebu kaangalie mpira huo Kisha mjifunze
 
Back
Top Bottom