Amani ni kubwa kuliko Utulivu, utulivu ni muhimu kuliko Demokrasia, na Demokrasia ni kubwa kuliko vyama vya siasa

Amani ni kubwa kuliko Utulivu, utulivu ni muhimu kuliko Demokrasia, na Demokrasia ni kubwa kuliko vyama vya siasa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tunahitaji amani sio utulivu, lakini ni heri ya utulivu kuliko demokrasia yenye vurungu, na bila kusahau kuwa demokrasia kwa watu hata wasiokuwa na vyama; ni zaidi ya vyama vya siasa kurahisishiwa kuwa viongozi na kwenda Ikulu.

Amani: Ni kuwa na uhakika wa kuwaona wajukuu zako kutokana na kupatiwa ulinzi na usalama pamoja na kuwa na uhakika wa kupata mahitaji ya msingi (chakula, hewa safi, maji safi, malazi safi, usafiri safi, elimu safi, matibabu safi na haki zako zote).

Utulivu: Ni kwenda kulala hata kama una njaa. Unalazimika au unalazimishwa kwenda kulala hata kama hujala kitu. Unaongozwa na kiongozi ambae hamjamchagua, hamumpendi wala hamumfahamu katokea wapi. unalazika kutii hata kama hutaki au unataka; yaani unapigwa halafu unaamrishwa usilie. Hali kama hiyo au inayofanana na hiyo ndio utulivu.

Demokrasia: Ni uhuru wa kujiamulia kile unachotaka ufanyiwe na kufanyia wengine, au kujifanyia mwenyewe. Kwaasili sisi hatuna asili ya demokrasia, majumbani kwetu hakuna demokrasi na hatukulelewa kidemokrasia; utapigwa na kunyamazishwa hapohapo usipige kele, watoto wetu na wanawake hawana uhuru wa kujichagulia na kuamua majumbani. Shule na vyuoni hakuna demokrasia.

Demokrasia imeletwa kwetu kama furushi la mzigo ambao lazima ulipokee hata kama hutaki. Waliotuletea demokrasia walikuwa na malengo yao yenye maslahi kwao kuliko kwetu. Demokrasia imeletwa kwetu na watu ambao walitutawala bila hiyari yetu, walipora rasilimali zetu bila hiyari yetu, walitupiga na kutuua wapendavyo, walifanya mizengwe kwenye chaguzi tusipate uhuru.

Demokrasia lazima tuwe makini nayo, sio kuchukua kila kitu. Neno "demokrasia" kwetu ni chanzo cha maandamano, uhalifu, vita, wizi wa kura, kutekana, kuharibu mali za wengine, na kutumia muda wa kuzalisha mali kwa kufanya demokrasia; demokrasia inaondoa umoja na mshikamano hivyo divide and rule kwao waletaji. Waliotuletea walijua kuwa italeta "divide" ili wao wa "rule". Tutachapana ili wauze silaha zao, na watapata vibaraka kwa njia rahisi sana na kukomba rasilimali zetu kirahisi

Nikiona mtu katekwa huwa najiuliza kwanza kwanini katekwa yeye sio mimi? nani kamteka? kwanini katekwa? Maana Kutekwa kunaweza kufanywa kwa sababu za usalama, kwa kulipa kisasi, ugomvi wa mapenzi, ardhi na kugombea uongozi au mali. Kutekwa kunaweza kuwa kwa kichawi au fitina TU.

Vyama vya siasa: Vinatumia demokrasia kama njia kujipatia kipato kupitia kupata uongozi, kupata ruzuku na misaada ya wahisani. Kama mazingira hayawawezeshi wanasiasa kuendelea kutawala au kupata uongozi basi hakuna demokrasia.

Demokrasia ni zaidi ya viongozi wa siasa kupata au kuendelea kuwa viongozi, bali demokrasia ni kwa watu watu wote kuanzia majumbani, mashuleni, mitaani na kwenye taasisi zote lazima kuwe na mifumo ya kidemokrasia. Demokrasia haianzii ikulu bali kwenye ngazi ya familia, jamii na vyama vya siasa vyenyewe.

Tukae chini kama taifa tukubaliane tunataka tuelekee wapi na tuelekeeje bila kutegemea vikundi vya vyatu vituamulie. Tusiwe kama dodoki kuzoa kila maelekezo kutoka nje bila kuyachambua kulingana na context na background yetu. Tusiruhusu mtu au watu watuchagulie kutupa kati ya Amani, Utulivu au demokrasia kwa matakwa yake ya kundi lake..
 
Kuna amani gani kama baadhi ya ndugu zetu wanatekwa na kwenda kuuwawa na Polisi.
Wewe utakuwa hujielewi umeandika andiko kubwa ila ni upumbavu mtupi
 
Kuna amani gani kama baadhi ya ndugu zetu wanatekwa na kwenda kuuwawa na Polisi.
Wewe utakuwa hujielewi umeandika andiko kubwa ila ni upumbavu mtupi
Jambo la msingi ni kumjua mtekaji kwanza na sababu zake, sio maandaamano ambayo yataishia kwenye kuleta UTULIVU (kuumizwa, kuporwa na kuuawa watu wengine zaidi) wa nchi. Maana amani ni bora kuliko Utulivu na utulivu ni bora kuliko demokrasia na demokrasia ya watu wote ni bora kuliko chama chako cha siasa.

Kule Marekani Trump amenusurika kuawa mara mbili lakini bado wanahangaika kuujua ukweli wote, Republicans hawakuitisha maandamano kwanini mgombea wao anataka kuawa lakini yule wa Democrats yuko salama mara zote.

Maandamano yataacha watu wengi walioharibiwa mali zao, waliojeruhiwa, waliokamatwa na waliouawa. Ndicho hicho unataka?

Sisi sote tunafahamu kuwa ziko nchi zingetamani na sisi utulivu wetu uondoke ili tugawane watalii na wawekezaji, lazima tuzame kwa kina tumjue mtekaji na muuaji wa watu wetu ni nani na ana malengo gani. Lakini tujue pia hata hao wanaotekwa ni akina nani, na kwanini wametekwa wao na sio wewe na mimi.
 
Tukae chini kama taifa tukubaliane tunataka tuelekee wapi na tuelekeeje bila kutegemea vikundi vya vyatu vituamulie. Tusiwe kama dodoki kuzoa kila maelekezo kutoka nje bila kuyachambua kulingana na context na background yetu. Tusiruhusu mtu au watu watuchagulie kutupa kati ya Amani, Utulivu au demokrasia kwa matakwa yake ya kundi lake..
🗑🚮🗑🚮🗑🚮
Uzi kama huu unajaza server bila sababu.
Mods, unganisha huu uzi na ule wa kamari...
 
🗑🚮🗑🚮🗑🚮
Uzi kama huu unajaza server bila sababu.
Mods, unganisha huu uzi na ule wa kamari...
server ni yako? unataka watu wooote tulie kila mtu akitekwa bila kujiuliza kwanini ametekwa, na nani amemteka? ukiwa mpumbavu unaweza kumlilia mtu ambae alikuwa na mipango ya kuiangamiza nchi. Mataifa yenye machafuko ni wenyeji wanaoshirikiana na wageni.

Watu wote lazima tuipiganie amani yetu, lakini tukishindwa kuipata amani abgalau tupiganie tuwe na utulivu watoto wetu wasome shule na kupata chanjo zao. Watanzania wengi hawana uwezo wa kupeleka watoto wao kusoma na kutibiwa Canada au Ulaya kama utulivu ukitoweka nchini. Utulivu ni muhimu sana kuliko Demokrasia.
 
Back
Top Bottom