Ambao hatujawahi kunywa pombe au kuvuta sigara, tukutane hapa

Ambao hatujawahi kunywa pombe au kuvuta sigara, tukutane hapa

Am not addicted to anything, that one straight i have.
1. Sijawai kunywa pombe ya aina yoyote hata kuonja,
2. Sijawai kuvuta sigara yoyote, labda makaratasi utotoni
3. Sijawai kubet na sijui
4. Sijawai kunywa energy drink yoyote
5.... Niiendelee niacheeeeeeee...
Mnaongozaga kwa kupiga pul na kwenda chumvin nyie na hamtumiag ndom..wanasema pia mnaongoza kwa UTI sugu.
 
Am not addicted to anything, that one straight i have.
1. Sijawai kunywa pombe ya aina yoyote hata kuonja,
2. Sijawai kuvuta sigara yoyote, labda makaratasi utotoni
3. Sijawai kubet na sijui
4. Sijawai kunywa energy drink yoyote
5.... Niiendelee niacheeeeeeee...
Unaishije mzee??
Umeokoka?
Au ni mtu wa mbunye sana??
 
Situmii hivyo vitu, na sina mpango wa kuja kuvitumia. Nilishawahi onja pombe mara Moja, ila matokeo hayakuwa mazuri. Nikajiapia sitopata niiguse tena.

Upande wa sigara, kipindi nipo chalii tulikuwa na mtindo wa kusokota gazeti alafu tunavuta kama sigara. Mara nyingi tulifanya hivyo tukiwa shule na watoto wengine. Sasa kuna jumapili moja niko home, nikiwa jikoni nikasokota karatasi langu na kuvuta, mshua akaniona. Alinipiga makofi kadhaa ya haraka haraka, alafu pale jikoni kulikuwa na kinu Cha wastani hivi akakichukua na kunivisha kichwani.

Sharti ikawa sitakiwi kukivua kile kinu hata pawe na sababu gani. Uzuri nilikuwa nishakunywa chai tayari, ila siku hiyo mchana sikuweza kula, maana ilikuwa nikajaribu kula kile kinu kinanizidia uzito. Na nikikiangusha tu, nachezea wakofi yasiyo na idadi Wala mpangilio. Mwisho wa siku nikaamua kutulia tu. Mshua yupo kwenye kiti anasoma gazeti, Mimi nimekaa pembeni yake huku nimeshikilia kinu. Akitaka kitu ndani alikuwa hanitumi, ananyuka kufata mwenyewe na Mimi ananiambia nimfate, hivyo nazunguka tu na kinu changu.

Muda huo bi mkubwa kaenda church, lakini hadi muda ambao kawaida huwa anarudi, siku hiyo hakurudi, sijui hata alipitia wapi. Nakumbuka nilikivaa kile kinu tokea kwenye mida ya saa tatu asubuhi hivi mpaka kwenye saa nane au tisa mchana, na hapo ni baada ya a bi mkubwa kurudi. Kile kinu kilikuwa kimetoka kutwangia kisamvu, nilivyokivua nilikuwa nahisi harufu ya kisamvu kwenye Kila kitu kinachopita karibu yangu.

Mpaka leo hii tukiongelea sigara popote lazima niikumbuke Ile siku.
 
Mimi nimetumia Bangi,sigara,pombe
Nashukuru nlifanikiwa kuacha.Japo na jilaumu sana kwanini nlitumia haya mataka taka.Sasa naishi vizuri maisha ya furaha na pesa ina jaa kila kukicha.
 
Katika ukuaji wangu wote hadi leo, sija wahi kuvuta sigara au kunywa pombe.
👉Sio ushamba ila hivyo sio vipaumbele vyangu.

Vipi Kuna wenzangu na mimi??
View attachment 2893067View attachment 2893068View attachment 2893069
NB;

Hatujawai kuishi trust me...

Hujawai kua mwanaume

Trust me 🙏🙏🙏

Mimi nimekullia familia ya uchumi wa Kati way back huko....

Mimi ni handsome japo age lime enda ukiniona Kwa sura first time unajua kua this guy is innocent people...

Ndio Mungu aliniumba ivyo
 
Back
Top Bottom