William Mshumbusi
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,761
- 2,391
Kuna tetesi nyingi baada ya msiba wa baba, baba wadogo na marafiki wa baba waliweka vikao vya siri. Wakipinga katakata mama asiwe msimamizi wa mirathi. Wakisisitiza uwezo wake ni mdogo kuongoza nyumba kubwa yenye watoto watukutu.
Ila wajomba wakongwe walimkingia kifua. Wakiamini kuwa baba wadogo wana tamaa.
Nimejifunza kitu kuhusiana na mitazamo ya mama sasa. Ni kama kila upande kati ya wajomba na baba wadogo unampeleka unavyotaka tena kwa vitu visivyoendana na kujikuta akitoa kauli na ahadi nzuri kama mjomba na kuja kufanya vilevile kama baba.
Ahadi za uongo na kauli tata zimekuwa nyingi zikidhihilisha uwenda kuna vitu vingi havijui kiundani. Na labda hakuwa na uwezo wakuongoza kaya kweli.
1. Mwaka wa jana aliahidi kupunguza kodi kwa asilimia 2. Kwenye ujira Sawa na alivyofanya marehemu baba miaka miwili nyuma. Ila asilimia mbili ya baba ikawa ni tsh 55,000/- nyongeza cash ya mshahara kwa mtu aliyepokea milion 1. Ila hiyo hiyo asilimia mbili punguzo la mama likaongeza tsh 2000/-(elfu mbili tu) cash. Watu wakiuliza eti hamjui hesabu.
2. Alianza kutoa haki ya ujira kukua kwa wakati na nyongeza halisi ila sasa upandaji unarudi kwa mafungu kama alivyofanya baba.
3 . Nilisikia kauli tata kuhusu walimu. Wana elimu ndogo, hawajitumi, mikataba yao iwe ya muda eti wawe vibarua. Hii kauli ningeisikia kwa marehemu baba nisingeshangaa kabisa. Lkn mh!
-Hajui kumnanga mwalimu moja ni kushusha heshima ya walimu wote.
-Hajui historia ya walimu wa UPE. Kwa wakati wao walivyosaidia nchi.
4. Hili la asilimia 23.3 hapana. Mwaka 2015 JK aliwaacha na asilimia 8 tu. Ndio iliyotamkwa. Lkn watu waliona vitu vikubwa na vyakushangaza. Ila hii asilimia 23,3 ukweli kwa wenye mishahara ya milion 1.5 bora tu angewawekea ile annualy increment.
Impact ya mishahara na ajira za serikali ni kubwa kwa uchumi. Kila hela inayokuja kama mshahara au posho uongeza mzunguko wa fedha kwa mtaani. Watumishi wa umma hubaki na hizo hela kwa siku 21 tu na kisha zote kuingia mtaani. Huko huzunguka na uongeza uwezo wa serikali kukushanya mapato. Hakuna mtumishi wa kuzifungia fedha hizo ndani.
Ni uoga kudhani nyongeza ndogo za mshahara inaweza kufilisi nchi kwa kiasi hicho.
Mama anapaswa kuamua. Kama anafata sera za baba basi afate kila kitu. Asiruhusu kukosolewa, abinye vyombo vya habari, afukuzefukuze, atishe watu, abinye Democrasia, watu wapotee.
Lkn hivihivi hatofika anapopataka
Au
Awaambie washauri dira yake, wamshauri afanye nini kufikia sio kuiacha. (Democracy, maslahi kwa watumishi, bei bora za mazao, bei nzuri ya pembejeo, haki)

- Hajui upungufu mkubwa sana wa walimu vijijini ambapo sasa mwalimu moja hufanya kazi za walimu wawili
- Hajui walimu ni kada yenye maslahi duni na mazingira duni kuliko kada yoyote.
- Mwalimu hana posho yoyote. Ni mshahara tu. Polisi, majeshi, madereva, Makatibu mitasi, Kada za afya wanapata vipato vingi kupitia program nyingi sana kama Resheni laki tatu kwa mwezi, program za tohara, uzazi salama, chanjo, elimu za uzazi, uzazi wa mpango, vikao, semina, washa, safari. Mwalimu ni yeye na kimshahara chake kidogo tu lkn mama haoni hilo.