antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 51,723
- 134,757
Duh,Zamani Watalii wakija Tanzania kwenye viwanja vyote vya ndege mapato yalikuwa yanakusanywa na kupelekwa Mfuko Mkuu wa Hazina na baadae Benki Kuu ya Tanzania ambapo zilikuwa zinagawanywa wa pande mbili za muungano kwa shughuli za Maendeleo. Kwa sasa mapato ya Watalii wanaoshukia Zanzibar yanabaki Zanzibar hayaingii Mfuko Mkuu wa Hazina wa Serikali ya Tanzania. Ila ya Tanganyika anaweza kuyachepusha na kuyapeleka Zanzibar kwa sababu yeye ndo muamuzi mkuu.
Zamani Mamlaka ya Kodi ilikuwa moja, kwa sasa amefanikisha Zanzibar kuwa na mamlaka yao ya Kodi ambayo iko huru na mamlaka kamili nje ya TRA.
Zamani Sheria ya TISS haikutamka chochote kuhusu uraia wa Naibu Mkurugenzi wa TISS Zanzibar sasa kabadili Sheria Naibu Mkurugenzi wa TISS Zanzibar ni lazima awe Mzanzibari. Kwa kifupi hapa ni kama kuna Idara ya Usalama ya Zanzibar iliyoanzishwa kwa shadow kisheria.
Zamani Benki Kuu ilikuwa moja, sasa hivi kalifanya Tawi la Benki Kuu ya Zanzibar kuwa Taasisi kamili ya Zanzibar inayojitegemea. Inakusanya Fedha na kujiratibia mambo yake yenyewe.
Mwanzoni kwenye mikopo iliwekwa vizuri kabisa kuhusu mgawanyo wa fedha za mikopo ili ziweze kuhudumia pande mbili za Muungano kwa uwiano. Sasahivi pesa zote za mikopo lazima ziende Zanzibar na kwa uwiano wa kuipendelea Zanzibar.
Kwa kifupi amekamilisha kuipa Zanzibar Uhuru wake kutoka Tanganyika. Haijali Tanganyika na hata ichafuke kivipi ameshajiwekea mazingira ya kurudi na kuishi kwa raha na mustarehe Zanzibar ambayo ameshaipa Mamlaka kamili na uwezo wa kujiendesha nje ya Muungano.
Kwa kifupi, hakuna wazalendo kwa saaa ndani ya ccm, wameamua kufumbia macho hayo yote dhidi ya shamba la bibi Tanganyika.
"Mitano tena" inamaanisha kiama kwa Tanganyika