antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 51,723
- 134,757
Duh,Zamani Watalii wakija Tanzania kwenye viwanja vyote vya ndege mapato yalikuwa yanakusanywa na kupelekwa Mfuko Mkuu wa Hazina na baadae Benki Kuu ya Tanzania ambapo zilikuwa zinagawanywa wa pande mbili za muungano kwa shughuli za Maendeleo. Kwa sasa mapato ya Watalii wanaoshukia Zanzibar yanabaki Zanzibar hayaingii Mfuko Mkuu wa Hazina wa Serikali ya Tanzania. Ila ya Tanganyika anaweza kuyachepusha na kuyapeleka Zanzibar kwa sababu yeye ndo muamuzi mkuu.
Zamani Mamlaka ya Kodi ilikuwa moja, kwa sasa amefanikisha Zanzibar kuwa na mamlaka yao ya Kodi ambayo iko huru na mamlaka kamili nje ya TRA.
Zamani Sheria ya TISS haikutamka chochote kuhusu uraia wa Naibu Mkurugenzi wa TISS Zanzibar sasa kabadili Sheria Naibu Mkurugenzi wa TISS Zanzibar ni lazima awe Mzanzibari. Kwa kifupi hapa ni kama kuna Idara ya Usalama ya Zanzibar iliyoanzishwa kwa shadow kisheria.
Zamani Benki Kuu ilikuwa moja, sasa hivi kalifanya Tawi la Benki Kuu ya Zanzibar kuwa Taasisi kamili ya Zanzibar inayojitegemea. Inakusanya Fedha na kujiratibia mambo yake yenyewe.
Mwanzoni kwenye mikopo iliwekwa vizuri kabisa kuhusu mgawanyo wa fedha za mikopo ili ziweze kuhudumia pande mbili za Muungano kwa uwiano. Sasahivi pesa zote za mikopo lazima ziende Zanzibar na kwa uwiano wa kuipendelea Zanzibar.
Kwa kifupi amekamilisha kuipa Zanzibar Uhuru wake kutoka Tanganyika. Haijali Tanganyika na hata ichafuke kivipi ameshajiwekea mazingira ya kurudi na kuishi kwa raha na mustarehe Zanzibar ambayo ameshaipa Mamlaka kamili na uwezo wa kujiendesha nje ya Muungano.
AtawezaKwa udi na uvumba anatafuta muda mwingine ,ili akamilishe Zanzibar yenye jeshi kamili maana ake suala la majeshi lisiwe la muungano
Huduma za Afya kwa zenji ndo usiseme wajawazito wanatibiwa bure mpaka siku ya kuondoka wanapewa pampas bure, Kwenye umeme sasa ndo wanateleza tu! Ikitokea wanadeni la umeme basi ujue Tanganyika ndo italipa.
Acha kukimbia jibu hoja hizozote hizo unazoropoka ni drama nonsense kabisa gentleman 🐒
Hata ukivinjika sawa. Ila sio hela za Tanganyika anazipeleka Zanzibarsasa si ndio munavyotaka hivo muungano uvunjike? sas mbona munalalamika?
Mhhh, yaani umeandika ukiwa na akili timamu kweli au bas tu nawew uonekane umeandika? BoT, ZRA/TRA zipo Zanzibar kabla huyo anayesema hajakuwa hata Makamo wa Rais!
hiyo ni hoja, ramli, ushirikina au dhana potofu gentleman?Acha kukimbia jibu hoja hizo
Zanzibar tayari wana Jeshi lao, nashangaa kwanini watu hawalijui hili?Kwa udi na uvumba anatafuta muda mwingine ,ili akamilishe Zanzibar yenye jeshi kamili maana ake suala la majeshi lisiwe la muungano
Dhana potofu ipi? Tena haya yaliyosemwa hapa ni madogo sana.hiyo ni hoja, ramli, ushirikina au dhana potofu gentleman?
unakua hoja kweli gentleman?🐒
Hatar na nusuZamani Watalii wakija Tanzania kwenye viwanja vyote vya ndege mapato yalikuwa yanakusanywa na kupelekwa Mfuko Mkuu wa Hazina na baadae Benki Kuu ya Tanzania ambapo zilikuwa zinagawanywa wa pande mbili za muungano kwa shughuli za Maendeleo. Kwa sasa mapato ya Watalii wanaoshukia Zanzibar yanabaki Zanzibar hayaingii Mfuko Mkuu wa Hazina wa Serikali ya Tanzania. Ila ya Tanganyika anaweza kuyachepusha na kuyapeleka Zanzibar kwa sababu yeye ndo muamuzi mkuu.
Zamani Mamlaka ya Kodi ilikuwa moja, kwa sasa amefanikisha Zanzibar kuwa na mamlaka yao ya Kodi ambayo iko huru na mamlaka kamili nje ya TRA.
Zamani Sheria ya TISS haikutamka chochote kuhusu uraia wa Naibu Mkurugenzi wa TISS Zanzibar sasa kabadili Sheria Naibu Mkurugenzi wa TISS Zanzibar ni lazima awe Mzanzibari. Kwa kifupi hapa ni kama kuna Idara ya Usalama ya Zanzibar iliyoanzishwa kwa shadow kisheria.
Zamani Benki Kuu ilikuwa moja, sasa hivi kalifanya Tawi la Benki Kuu ya Zanzibar kuwa Taasisi kamili ya Zanzibar inayojitegemea. Inakusanya Fedha na kujiratibia mambo yake yenyewe.
Mwanzoni kwenye mikopo iliwekwa vizuri kabisa kuhusu mgawanyo wa fedha za mikopo ili ziweze kuhudumia pande mbili za Muungano kwa uwiano. Sasahivi pesa zote za mikopo lazima ziende Zanzibar na kwa uwiano wa kuipendelea Zanzibar.
Kwa kifupi amekamilisha kuipa Zanzibar Uhuru wake kutoka Tanganyika. Haijali Tanganyika na hata ichafuke kivipi ameshajiwekea mazingira ya kurudi na kuishi kwa raha na mustarehe Zanzibar ambayo ameshaipa Mamlaka kamili na uwezo wa kujiendesha nje ya Muungano.
Hapana kwa sasa ni kama vikosi mfano jku kwa jeshi la kujenga uchumi,kmkm ,ni kwa ajiri ulinzi wa kupambana na uharamia majini na mengine ,ila sio jeshi la ulinzi kamili wa mipaka ya nchi kama jwtzZanzibar tayari wana Jeshi lao, nashangaa kwanini watu hawalijui hili?
Mimi keshanipata ila nina akili kuliko wewe.Utaandika Hadi 2030 anapokabidhi madaraka.
Wajinga ndio mtawapata na bahati mbaya kwenu hawana Cha kuwasaidia 😆😆
Hapana, siviongelei hivyo vikosi vya KMKM na JKU, naongelea kikosi hiki hapaHapana kwa sasa ni kama vikosi mfano jku kwa jeshi la kujenga uchumi,kmkm ,ni kwa ajiri ulinzi wa kupambana na uharamia majini na mengine ,ila sio jeshi la ulinzi kamili wa mipaka ya nchi kama jwtz
Skuyajua hayo na nahsi ndo kwa sasa wasiojulikana ndo tuwaowaskia kutokea humoHapana, siviongelei hivyo vikosi vya KMKM na JKU, naongelea kikosi hiki hapa
Wanatumia sare, na vyeo vya JWTZ na hata mafunzo yao na kila kitu. Hilo ni Jeshi tayari linalosubiri Muungano uvunjike.
Sahihi kabisa. Mafunzo yao hayana tofauti yeyote na mafunzo ya JWTZHapana, siviongelei hivyo vikosi vya KMKM na JKU, naongelea kikosi hiki hapa
Wanatumia sare, na vyeo vya JWTZ na hata mafunzo yao na kila kitu. Hilo ni Jeshi tayari linalosubiri Muungano uvunjike.
Hilo ni Jeshi Kamili, wenyewe wanaita Kikosi Cha Valantia, hata ukiingia Makambini kwao kila kitu ni JWTZ.Skuyajua hayo na nahsi ndo kwa sasa wasiojulikana ndo tuwaowaskia kutokea humo
Hilo ni Jeshi kamili linalosubiri Muungano uvunjike ili likasimu Majukumu ya JWTZSahihi kabisa. Mafunzo yao hayana tofauti yeyote na mafunzo ya JWTZ