The tolerance 1
JF-Expert Member
- Sep 10, 2022
- 404
- 517
Umeongea ukweli mkuu,kuna wanaume wanajiona wao ndo wao,yani hawataki kusikiliza mtu yyte Wala ushauri,ni wajuaji,viburi na dharau wanafanya wanayoyataka,ni wababe wajeuri na hawajali,ila mbio za sakafuni huishia ukingoniMkuu kuna tabia wanaume tumeanza kuchukulia kuwa kuoa ni kama vile kutoa msaada kwa binti au wazazi wake.
Kama humtaki binti mpe ukweli kuwa hauko tayari kumuoa awe huru.
Hii danadana na sababu uchwara ni dharau.
Kila mwanaume ni mkwe mtarajiwa.
Hakuna mwanaume atapenda kuona binti anachukuliwa poa...jitu linamtumia binti yako kwa ulaghai wa kuoa mwishowe unaanza ooh silipi mahari nampa msaada rafiki.
Katika mahusiano ya ndoa hakuna wazazi wenye msaada kimaisha kama wazazi wa binti hasa wazazi waelewa.
Hawatapenda kuona binti amekwama bila kutoa msaada.
Tubadilishe mitazamo ya kikoloni