Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

😅😅😅 Mapenzi ni fumbo
 
Duh,haya ni madini tupu mkuu
 
Nakubaliana na wewe kwenye 1&2 but napinga ushauri wako... huyu bado kinda anahitaji muda zaidi kuwa mume na mkuu wa familia... iko siku ataacha kumlipia mwanae ada kisa rafiki yake anashida ya ushuru wa kutoa gari bandarini.
 
Nakubaliana na wewe kwenye 1&2 but napinga ushauri wako... huyu bado kinda anahitaji muda zaidi kuwa mume na mkuu wa familia... iko siku ataacha kumlipia mwanae ada kisa rafiki yake anashida ya ushuru wa kutoa gari bandarini.
......aisee hapana hatuwezi kufikia huko, itakuwa balaa Sasa.... ingawa kwenye makasino kuna myamba inaweka bond/stake wake zao hasa sport betting.....
 
Wewe unajilazimisha kwa huyo Mwanamke kiufupi humpendi,kama uliweza kuthamini kumsaidia rafiki yako kuliko kupeleka mahali maana yake jambo LA rafiki yako lilikuwa muhimu na thamani zaidi kuliko kutoa mahali.

Nakuhakikishia huyo Mwanamke ukimuoa lazima atakuja kulipiza kisasi kwa aibu ulihompa.

Ushauri wangu,naona ndoa yenye migogoro mingi hapo badae ukiamua kuendelea kuwa na huyo Mwanamke.
 
😄 mapenzi yana nguvu sana aisee. Mimi niliagwa kabisa kwamba nisahau lakini anataka arudi na masharti juu!
Huyo dada hana namna ndo mana ameamua kurudi...kwanza una dharau na jeuri na kujiona wewe ndo wewe....... Ukweni walikutegemea na ukapata jambo muhimu kuliko mahari ukalifanyia Kazi...sasa kwanini hukuwapa wakwe taarifa kwa kuwaheshimu!?!?

Inategemea na Familia lkn.. familia nyingine wangekudharau kama ulivyo wadharaulisha....... Pole kwa huyo dada.
 
Mimi sikatai,ulifanya vizuri kumsaidia rafiki yako,lakini mahali ulipokosea tu ni pale ambapo hukutia taarifa inayoelewka kwa mwenzako,nafikiri waliotangulia pia wame coment hivyo,nafikiri baada ya mwenzako kusema muachane usingekubali muyamalize wenyewe,kwa vile uliahidi kupeleka hiyo mahari,ungeenda uwaeleze hiyo dharura uliyoipata na uwaeleze maamuzi ya mwenzako,na hayo yote yangetakiwa kufanywa na wazee wako na sio wewe,wazee wana uwezo mkubwa wa kuongea na wazee wenzao
 
Kabisa mkuu,
 
Mkuu
Nisikilize kwa makini.

Uliamua kutoa msaada kwa rafiki kwa ugumu alioupitia na ilipaswa ndiyo ukae nanmwenzako muyajenge lakini kitendo cha yeye kusema bora muachane ni wazi neno ndoa kwake ni STATUS na siyo mahusiano.

Angelalamika na kupiga kimya inamake sense sana kuwa anakupenda ila umemkera. Na hapo wajibu wa kuwaomba radhi nduguze ni sahihi.

Mtu kakuambia MUACHANE na akakutosa. Ameenda hukoo akagundua chaka lake limeingia ngiri ndo anarudi mbio kwako na kukutaka uombe radhi kwa nduguze. Hapo ni wazi unaingia wrong foot kwenye familia. Hujui aliwaambia nini nduguze. Usikute kawaambia umepata mwanamke ukasusa kuja ndo maana wanakumaindi kinyama.

Kikubwa, kaa na mshenga wako muite mpenzi wako muyajenge kisha akaandae yeye mazingira ya kuleta mahari. Au sivyo utaoa na utachakaa
 
Si kila mtu anaweza makandokando. Some people are straightforward
 
Huu mchango ningekuwa mod ningeuweka juu kabisa..... Huyu kijana ni moja wa wale wavulana wanao jisikia na kujiona wao ni kila kitu....

Huyu hata baada ya michango ya mawazo alopewa atabaki kama alivyo kwakuwa bado anajiona yupo sahihi....

Mungu saidia hili balaa lisije kwenye familia yetu au ukoo wetu... Mungu saidia pia hiyo familia iwe ya waelewa wasiruhusu binti yao kuingia kwenye hili shimo..... Mungu pia naomba huyo binti ufungue ufahamu wake maana hapa hamna kitu 🚮🚮
 
Binti anajiingiza kwenye mateso makubwa sana
 
Kwahiyo kwa mawazo yako binti ndo kakosea!?!?..... Aisee walio kwenye mchakato wa kutafuta wachumba kwasasa Mungu awasaidie.. sio kwa vichwa hivi 🚮🚮
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…