Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ila wewe mbona ishu yako ndogo ..mimi kuna mwana yeye sio tu aliahirisha ila hata manzi ake hakumwambia..Kikeni huko wamejiandaaa kishenzi mavyakula na vilaji kama unavyojua wachaga!.. e bwana eeh!!. Mshkaji hakutokea kabisaaaaaa wala manzi ake hakumwambia kitu yan ilikua bonge la soo na aibu kwa dem..ndugu jamaa walishajaa kupokea mahali na kumwona jamaa ila ikawa tee!!.

Wanawake sas wasivyo na akil wakat mwingine, manzi aliporud dar wakaendelea kuishi na mshkaji..sijui waliyamaliza vp? 😂😂😂
😅😅😅 Mapenzi ni fumbo
 
.......kuna mawili katika hili, 1.inawezekana mtu akataka kutoa mahari lakini bado hajui nafasi ya mke/mpenzi/familia katika maisha ya mwanaume halisi, lakini pia hujui nafasi ya rafiki katika maisha yake 2.kuna watu pia wanapoingia katika mahusiano tayari wanaonekana kujiona wao ni wathamani zaidi kuliko mwenzie wake(hali ya kujisikia nakujiona bora na kwamba unaweza fanya maamuzi yoyote hatakama ni ya kumuumiza au kumdhalilisha mwenzio, wazee wa kujiona wako sahihi ktk kila jambo)........Sasa basi kama mtu ana tabia mbili hizo naona bado hajawa matured enough to be in marriage, watu wadizaini hii huingia kwenye ndoa then soon wanaanza kusema kataa ndoa......
Ushauri: omba msamaha vizuri kabisa ukiwa na mahari mkononi plus faini....bibie yupo sahihi kabisa kuweka masharti coz kashagundua kuwa anadeal na mtu ambaye pengine dishi limecheza tayari.....
Duh,haya ni madini tupu mkuu
 
Nakubaliana na wewe kwenye 1&2 but napinga ushauri wako... huyu bado kinda anahitaji muda zaidi kuwa mume na mkuu wa familia... iko siku ataacha kumlipia mwanae ada kisa rafiki yake anashida ya ushuru wa kutoa gari bandarini.
 
......aisee hapana hatuwezi kufikia huko, itakuwa balaa Sasa.... ingawa kwenye makasino kuna myamba inaweka bond/stake wake zao hasa sport betting.....
 
Wewe unajilazimisha kwa huyo Mwanamke kiufupi humpendi,kama uliweza kuthamini kumsaidia rafiki yako kuliko kupeleka mahali maana yake jambo LA rafiki yako lilikuwa muhimu na thamani zaidi kuliko kutoa mahali.

Nakuhakikishia huyo Mwanamke ukimuoa lazima atakuja kulipiza kisasi kwa aibu ulihompa.

Ushauri wangu,naona ndoa yenye migogoro mingi hapo badae ukiamua kuendelea kuwa na huyo Mwanamke.
 
😄 mapenzi yana nguvu sana aisee. Mimi niliagwa kabisa kwamba nisahau lakini anataka arudi na masharti juu!
Huyo dada hana namna ndo mana ameamua kurudi...kwanza una dharau na jeuri na kujiona wewe ndo wewe....... Ukweni walikutegemea na ukapata jambo muhimu kuliko mahari ukalifanyia Kazi...sasa kwanini hukuwapa wakwe taarifa kwa kuwaheshimu!?!?

Inategemea na Familia lkn.. familia nyingine wangekudharau kama ulivyo wadharaulisha....... Pole kwa huyo dada.
 
Sina jeuri hata kidogo. I'm down to earth, humble. Ndio maana hata binti wa watu anaomba kurudi. Kuna historia zinazoumiza sana katika maisha. Msaada ni muhimu sana kwa watu wengine. Huu ni utamaduni wangu. Ninatamani kila mtu atambue kwamba sikufanya kwa lengo la kumdhalilisha mwenzangu ila alitoa maamzi ya ghafla sana.
Mimi sikatai,ulifanya vizuri kumsaidia rafiki yako,lakini mahali ulipokosea tu ni pale ambapo hukutia taarifa inayoelewka kwa mwenzako,nafikiri waliotangulia pia wame coment hivyo,nafikiri baada ya mwenzako kusema muachane usingekubali muyamalize wenyewe,kwa vile uliahidi kupeleka hiyo mahari,ungeenda uwaeleze hiyo dharura uliyoipata na uwaeleze maamuzi ya mwenzako,na hayo yote yangetakiwa kufanywa na wazee wako na sio wewe,wazee wana uwezo mkubwa wa kuongea na wazee wenzao
 
Mkuu ukubali usikubali huna vipaumbele.

Mimi nina huruma sana, naweza kuacha kula mimi nimpe mhitaji. Lakini linapokuja suala muhimu nina vipaumbele visivyobadilika.

Mtu wangu au watu wangu ni kipaumbele changu cha kwanza.

Endapo nitabadili maamuzi nisaidie mwingine.....nitatumia convincing power yangu yote nihakikishe wananiunga mkono nimtangulize mwingine badala yao.

Mwanaume hakikisha una NGUVU YA ushawishi.
Ushawishi
Ushawishi
Ushawiahi wanaume tujitahidi katika hili hatutajuta.
Wanawake ni waelewa mno ukionyesha kuwajali
Kabisa mkuu,
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha. Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea. Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.! Kabla sijatoa maamzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Mkuu
Nisikilize kwa makini.

Uliamua kutoa msaada kwa rafiki kwa ugumu alioupitia na ilipaswa ndiyo ukae nanmwenzako muyajenge lakini kitendo cha yeye kusema bora muachane ni wazi neno ndoa kwake ni STATUS na siyo mahusiano.

Angelalamika na kupiga kimya inamake sense sana kuwa anakupenda ila umemkera. Na hapo wajibu wa kuwaomba radhi nduguze ni sahihi.

Mtu kakuambia MUACHANE na akakutosa. Ameenda hukoo akagundua chaka lake limeingia ngiri ndo anarudi mbio kwako na kukutaka uombe radhi kwa nduguze. Hapo ni wazi unaingia wrong foot kwenye familia. Hujui aliwaambia nini nduguze. Usikute kawaambia umepata mwanamke ukasusa kuja ndo maana wanakumaindi kinyama.

Kikubwa, kaa na mshenga wako muite mpenzi wako muyajenge kisha akaandae yeye mazingira ya kuleta mahari. Au sivyo utaoa na utachakaa
 
Mkuu...mwanaume ni simba, kiongozi na mshawishi.

Inategemea na aprochi yake.
Angemwita amwambie....my love plz naomba tuahirishe kwani nilitegemea kupata pesa lakini nimeahirishiwa nami aitaki nikuaibishe kwa wazazi wako.
Naomba tusogeze mbele kidogo...binti asingekataa lakini kutamka wazi unamsaidia rafiki na aio ndg ilikuwa dharau mkuu
Si kila mtu anaweza makandokando. Some people are straightforward
 
Mkuu kuna tabia wanaume tumeanza kuchukulia kuwa kuoa ni kama vile kutoa msaada kwa binti au wazazi wake.

Kama humtaki binti mpe ukweli kuwa hauko tayari kumuoa awe huru.

Hii danadana na sababu uchwara ni dharau.
Kila mwanaume ni mkwe mtarajiwa.

Hakuna mwanaume atapenda kuona binti anachukuliwa poa...jitu linamtumia binti yako kwa ulaghai wa kuoa mwishowe unaanza ooh silipi mahari nampa msaada rafiki.

Katika mahusiano ya ndoa hakuna wazazi wenye msaada kimaisha kama wazazi wa binti hasa wazazi waelewa.
Hawatapenda kuona binti amekwama bila kutoa msaada.
Tubadilishe mitazamo ya kikoloni
Huu mchango ningekuwa mod ningeuweka juu kabisa..... Huyu kijana ni moja wa wale wavulana wanao jisikia na kujiona wao ni kila kitu....

Huyu hata baada ya michango ya mawazo alopewa atabaki kama alivyo kwakuwa bado anajiona yupo sahihi....

Mungu saidia hili balaa lisije kwenye familia yetu au ukoo wetu... Mungu saidia pia hiyo familia iwe ya waelewa wasiruhusu binti yao kuingia kwenye hili shimo..... Mungu pia naomba huyo binti ufungue ufahamu wake maana hapa hamna kitu 🚮🚮
 
Binti anajiingiza kwenye mateso makubwa sana
 
Mkuu
Nisikilize kwa makini.

Uliamua kutoa msaada kwa rafiki kwa ugumu alioupitia na ilipaswa ndiyo ukae nanmwenzako muyajenge lakini kitendo cha yeye kusema bora muachane ni wazi neno ndoa kwake ni STATUS na siyo mahusiano.

Angelalamika na kupiga kimya inamake sense sana kuwa anakupenda ila umemkera. Na hapo wajibu wa kuwaomba radhi nduguze ni sahihi.

Mtu kakuambia MUACHANE na akakutosa. Ameenda hukoo akagundua chaka lake limeingia ngiri ndo anarudi mbio kwako na kukutaka uombe radhi kwa nduguze. Hapo ni wazi unaingia wrong foot kwenye familia. Hujui aliwaambia nini nduguze. Usikute kawaambia umepata mwanamke ukasusa kuja ndo maana wanakumaindi kinyama.

Kikubwa, kaa na mshenga wako muite mpenzi wako muyajenge kisha akaandae yeye mazingira ya kuleta mahari. Au sivyo utaoa na utachakaa
Kwahiyo kwa mawazo yako binti ndo kakosea!?!?..... Aisee walio kwenye mchakato wa kutafuta wachumba kwasasa Mungu awasaidie.. sio kwa vichwa hivi 🚮🚮
 
Back
Top Bottom