Mkuu nikuulize maswali machache :-
i, Unafahamu kuwa marekani anaimiliki millitary base ngapi duniani?
ii, Unafahamu hizo millitary base anazo miliki marekani anamiliki kwenye nchi ngapi ?na kiasi gani Cha fedha anazifadhiri hizo nchi kwa yeye kuweka millitary base?na namna gani anaweza kuzihakikishia usalama hizo nchi?
iii, Unafahamu kuwa marekani anatoa mchango wa asilimia ngapi kwenye mashirika ya Umoja wa mataifa mfano shirika la afya, chakula ,wakimbizi n.k?
iii, Unafahamu ni sifa zipi za kiuchumi nchi inatakiwa kuwa nazo ili iitwe dunia ya tatu ?
iv, Unafahamu ni sifa zipi za kiuchumi nchi inatakiwa kuwa nazo ili iwe dunia ya kwanza?
iv, Unafahamu budget ya fedha ya mwaka ya marekani ni ipi na nchi za dunia ya tatu budget zao ni zipi?
V, Unafahamu marekani yupo kwenye ushirikiano na muungano mingapi ya kiuchumi na kijeshi na anachangia kifedha kwa asilimia ngapi tofauti na wenzake?
Vi, Unafahamu ni mataifa mangapi marekani anayafadhiri kiuchumi duniani kupitia misaada na mikopo?
Vii, Unafahamu ni mabenki makubwa mangapi duniani marekani anaimiliki?
Vii, Unaifahamu GDP ya Marekani Ni ngapi?
Viii, Unafahamu ni mataifa mangapi yanamtegemea marekani kiulinzi pia na Kisayansi na teknolojia?
ix, Unafahamu budget ya ulinzi ya marekani ni kiasi cha fedha kumlinganisha na mataifa ya dunia ya tatu?
X, Unafahamu GDP ya china Ni ngapi na ni miaka mingapi ijayo China imepanga kumfikia marekani kiuchumi ?kwa sababu huyu pekee ndio anayemfukuzia marekani kwa ukaribu zaidi
Xi, Unafahamu marekani anaushawishi kiasi gani duniani?
Xii, Unafahamu marekani ameweka kiasi gani cha fedha na dhahabu?
Xiii, Unafahamu taasisi ngapi zinazo ongoza nchi ya marekani ? uimara wake ulivyo pia unafahamu?
Xiv, Unafahamu ni kwanini China licha ya kuwa na uchumi mkubwa na ushawishi sehemu mbalimbali dunia bado hajaweza kumwangusha marekani Ila bado anamtegemea marekani kiushirikiano mbalimbali wa kibiashara pamoja na Kisayansi na kiteknolojia?
Xv, Unafahamu ni mifumo mingapi ya kiuchumi dunia imeshikiliwa na marekani na washirika wake mfano kibiashara, kifedha, kiteknolojia n.k
Xv, Unafahamu ni viwanda vingapi marekani anamiliki ndani na nje ya nchi yake vinavyokuza uchumi wake?
Ni hayo tu maswali machache niliyonayo ninaweza kukuongezea mengine Kama kutakuwa na ulazima wa mimi kufanya hivyo