Amestaafu na kupewa shilingi milioni mia moja. Anaomba msaada

Uongo huu kwa maana dhama na banks za kibiashara zote zipo BOT
Sio uongo; mteja analipwa 1.5m halafu atasubiri hadi pale bank kuu itakao ifilisi hiyo bank na kuuza mali zake zote kile kitakacho patikana baada ya gharama zao ndio watagawiwa tena ila huo mchakato wa kuuza mali unaweza kuchukua zaidi ya miaka 10
 
Uzi umejaaa point mpaka naogopaa…
 
Kwa jinsi anavyo onekana yupo stable kimaisha nilitamani kusikia ametoa/atatoa shs 10M kwa ajili ya kusaidia watoto yatima ili aweke akiba ya MBINGUNI au pengine kubusti ndugu masikini.

Mwambia anunue bonds za bank kuu kwani security yake ni ya hali ya juu ila kabla ya hapo tunamshauri atenge fungu la kusaidia kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kumpa kazi na kumlinda hadi kumstaafisha akiwa salama
 
Kama tayari ashaamua kuziweka Bank si atembelee mabank kupata taarifa za uhakika? Au aende Bank alimoweka hizo pesa, au anazo cash nyumbani?
 
Mkuu naomba unitoe tongotongo. Hivi ukisema ''bond za miaka 20'' maana yake ni kuwa unaingia mkataba wa kuwaachia fedha zako kwa miaka 20 huku ukichukuwa ''faida'' tu?
Maana yake unaikopesha serikali na utakuwa unalipwa faida kwa miaka 20, na hapo utatudishiwa mtaji.

Lakini kuna iitwayo secondary market, ambako unaweza kuziuza bond hizo kabla ukihitaji. Mtu mwingine atanunua, yeye aendelee kula faida hadi miaka 20 itakapokamilika.

Bond za miaka 20 zinauzika kwa urahisi sana secondary market kwa vile wengi sana wanazitaka.
 
Asante sana. Kwa hiyo njia ya ''kuchukuwa'' zako kabla mkataba haujaisha ni kwa kuuza tu. Lets say mambo yakienda sivyo na ukikosa mnunuzi inakuwa huna cha kufanya.
 
Mkuu naomba unitoe tongotongo. Hivi ukisema ''bond za miaka 20'' maana yake ni kuwa unaingia mkataba wa kuwaachia fedha zako kwa miaka 20 huku ukichukuwa ''faida'' tu?
Ndio mkuu kinachofanyika hizo bond unanunua kwa muda maalum kama hivyo kuna 2,5 ,10 ,15 20 na saiv wameongeza ya 25 yrs wew ukishannunua unapata interest mara 2 kwa mwaka yaan kila baada ya miezi 6 ila pia unaweza kuziuza kwa utaratibu wa kawaida kama unavyouza share otherwise kama umenunua ya 20 yrs unakula interest after 20 yrs wanakurudishia hela yako lakin kwenye kurudisha inategemea kama ulibid kwa premium ile premium itapunguzwa au utalipa zaid wakati wa kununua mfano bond bei ni 100.0000 lakin kulingana na competition unakuata watu wanabid kwa 100.0015 hivyo hiyo 0.0015 inakuwa ni premium.

Ambayo ni ziada utakayolipa zaidi ya bei ya kawaida. ila ukinunua kwa discount utapata faida zaidi yaani unaweza kununua kwa 99.9387 yaan wew wakati wa kurudisha pesa yako wanarudisha 100.000 hivyo tofauti ndio faida yako kama una namba ya whatassap unaweza niambia nafikiri kwenye sim naweza kukuelewesha vizuri zaidi kama unataka kuinvest kwenye bond.
 
Asante sana mkuu. Umetoa maelezo mazuri na nimegundua kuwa hili jambo ni pana na linahitaji ushauri kama ulivyo-suggest. Sasa hivi bado nina mengi ya kufanya lakini kuna siku nitajaribu kuwekeza inshallah..
 
Asset sio lazima nyumba. Wabongo mnafeli sana na kuwekeza kwenye ujenzi bila ya taaluma ya real estate. FYI watu wanasomea iyo taaluma miaka mitatu ndo wanakupa na ujuzi wa kufanya maamuzi sahihi na sio kukurupuka na kujenga tu. Kuna financial asset na kuna sehem ambazo mstaafu anatakiwa awekeze especially baada ya kustaafu mana alishachelewa kuwekeza.

So anahitajistability na sio kurudi kazini tena kuanza shuhulikia nyumba na biashara. Awekeze kidogo kwenye financial assets na zengine aangalie JATU wana program nzuri na kwa yy atatumia 5million tu na atakuwa safe. Some 5m nyengine awekeze kwenye kilimo cha vanilla kwa kumwona vanilla international limited wamsaidie. Na 70million zilizo salia akanunue BONDS. au tafuta financial consultancy agency wakamshauri vizuri.

Atatumia 1-2million ila ushauri watakaompa utamuokolea mda na hasara . These agency ni muhimu na sio kukurupuka na kuja JF ushauriwe. Maybe sio mbaya coz ndo unapata ushauri wa kwenda financial consultancy agency na sio eti humu JF wakushauri uwekeze wap hela yako yote unayotegemea.
 
Hio vanila si ndio watu wanapigwa.Kilo elf 20 wao wanadai kilo sh laki 5.Wadau humu wamesema hii vanila unachavusha mwenyewe, sasa huyo mstaafu aanze kuvizia chavua badala ya kupumzika.
We umepanda hio vanila utoe ushuhuda.
 
Aende akazinunue zote hisa bank kuu. Hutajuta
 
Hio vanila si ndio watu wanapigwa.Kilo elf 20 wao wanadai kilo sh laki 5.Wadau humu wamesema hii vanila unachavusha mwenyewe, sasa huyo mstaafu aanze kuvizia chavua badala ya kupumzika.
We umepanda hio vanila utoe ushuhuda.
Explanation ni kubwa ila niliishia na kutafuta financial adviser
 
Kwa hio unataka atupe m5 zake.
Hivi unajua maana ya financial adviser? Nj msomi aliebobea huko na sio sisi ambao tutaongea tu hatuna facts wala kujua uhalisia wa hali ya soko. Aende huko ata km itamgharimu 1-2million wamshauri jinsi ya kuwekeza salama kiinua mgongo chake!! Umenielewa?
 
OK!, I CATCH YOU, NI KWELI NYUMBA SIO KILA WAKATI HUPANDA BEI,MFANO SASA HIVI ZIMEANGUKA BEI,

::KUNA UJENZI WA BANDA LA KUISHI.
::KUNA UJENZI WA JENGO LA KIBIASHARA,BANDA LA BIASHARA NI LAZIMA LIWE INVESTED KATIKA ENEO LA KIBIASHARA.
 
Kuna kitu inaitwa forex, kwa mtaji wa milioni themanini kutengeneza laki tano kwa siku ni kama unamsukuma mlevi🤣🤸🐒

On a serious note akae mbali na biashara za mtandao
Weee usiwafanye wenzo wakaweka msiba bila kutarajia ...😳😳🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…