Amezaa na mume wa mtu, katelekezewa mwanaye

Amezaa na mume wa mtu, katelekezewa mwanaye

[emoji1318]
NJE YA MADA:
[emoji1313]
[emoji41][emoji41][emoji41]
ASANTENI DADA ZETU KWA KUZALIA NYUMBANI,
MAANA TUNAPATA WAJOMBA WA KUWATUMA BANGI!!!
Nasubiri huyu mjomba wangu akue[emoji23]
 
Wanaume marijali ambao bado hatujaoa tupo wengi Sana huku nje, ila nyie wanawake mnaamua kukurupukia waume za wenzenu na mkishazinguliwa huko mnakimbia humu kuomba ushauri.Nkt!

Huyu Wala tusimshauri chochote especially sisi wanaume.Acha apambane tu na Hali Yake mwenyewe maana Mwana kulitafuta Mwana kulipata.
[emoji1787][emoji1787]
 
Wakuuu.

Dada yangu (mtoto wa mama yangu mdogo) alipewa ujauzito na mwanaume ambaye ameshaoa na wamezaa na huyo mke wake. Dada yangu alikuwa anajua kwamba huyo mwanaume ni mume wa mtu na alishawahi kuambiwa na huyo mwanaume, "kama unavyojua mimi ni mme wa mtu, kwahiyo we niambie vyote ila usije kuniambia habari za umeshika mimba yangu!"

Kwahiyo baada ya kuunasa ujauzito alifikiria sana ile kauli aliyoambiwa na jamaa tangu mwanzo lakini haikumzuia kumpa hiyo taarifa kwamba "Bwana nna ujauzito wako". Jamaa bila kupepesa macho akamjibu "Nadhani hilo swala nilishaliongea tangu zamani, kwahiyo kama una hoja nyingine lete, ila kuhusu hiyo habari ya ujauzito sijui mimi siitambui".

Dada Yangu akamuuliza kwahiyo ichi kiumbe chako vipi? Jamaa akamjibu simple tu "Utajua wewe, utakachoamua ndiyo hicho hicho kwangu mimi sawa tu, kwanza usinisumbue isije mke wangu akajua halafu ukaniaribia ndoa yangu". Dada akabaki tu ameduwaa!

Mpaka ujauzito unafikisha miezi mitatu alikuwa anaogopa kuwaambia nyumbani, lakini kama ujuavyo mimba ya binadamu haifichiki labda ya kuku. Siku ya siku tumbo hilo, kumuuliza vipi akajibu kama mnavoona au hamjaelewa nini, wakamjibu sawa. Kimbembe kikaja kwenye kumtaja aliyempa huo ujauzito, mpaka saizi hivi mtoto kazaliwa juzi tu hapa ana kama wiki mbili hivi dada hajamtaja aliyempa ujauzito na hana mpango wa kuwatajia. Anawajibu tu "Jaman eeh aliyenipa ujauzito mwenyewe hata haeleweki, kwahiyo achaneni naye. Nyie mniangalie mimi angekuwa mtu wa kueleweka kwanza mngeshamuona hapa".

Hiyo story yote kuhusu huyo mwanaume ni nani, ni mimi nilimchimba akanipa mkasa mzima na akasisitiza nisiawaambie wazee. Nikamuuliza kwanini hakutoa (kwa kumtega tu nijue anachowaza, maana mimi ni miongoni mwa watu tunaopinga vikali iko kitendo).

Akanijibu "Nimefanya ushenzi mwingi sana uko, sasa hivi naogopa nisije kupoteza uzazi wenyewe", nikamuelewa. Baada ya kijifungua hapo juzi nikaauliza vipi umempa taarifa, akaniambia "Ujauzito aligoma kuhudumia, tarehe zilivokarbia za kijifungua nikamtaarifa akanijibu vilevile nItajua mimi, ye hayamuhusu".

Kwahiyo sasa hivi dada yupo tu nyumbani analea mtoto kama single mother, baba ye hataki kujua.

Maswali nnayo jiuliza:
1. Huyo jamaa hana hata shauku ya kumuona mwanawe?
2. Dada aliwaza nini kutoka na mume wa mtu?
3. Dada atakujaje kumsimulia mjomba hadithi ya baba yake?
4. Dada atamjibu nini mjomba siku mjomba akitaka kujua alipo baba yake?
5. Dunia ina mengi, kwenye kupita huku na huku dogo anagundua yule ni baba ake, atamchukuliaje?
6. Watoto wa yule jamaa watamchukuliaje mjomba wakija kugundua ni mdogo wao?
7. Yule jamaa si anatengeneza Mond na dimpoz mwingine?

Dunia ina mengi.


#OneDayYouWillBeGone.
Dr. criminal.
Mond Gani tena?
 
Ni dada ang lakini pia ni rafiki ang sana,,yani tuna urafiki nje ya undugu kiasi kwamba tunashirikishana izo changamoto za mahusiano ndo maana akawaacha wote me ndo akanipa mkanda mzima,,We are friends.
Kama binadam na kama mwanamke ana mapungufu mengi sana na mimi huwa namshauri sana kuhusu mienendo yake anasemaga tu sawa lakini habadiriki,,all in all she is my sister, i love her kivyovyote alivyo na ntamsupport kadri niwezavyo.
Kama ni mshkaji wako basi sawa.
 
Michepuko, michepukooooooooo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119]
Wanahimarisha sana ndoa hao, maana ukikosa kupata huduma nyumbani unalala tu kwa amani kesho yake unaita mchepuko unapungiza uzito maisha yanasonga
 
Huyo dada yako kichwani alikuwa ana msemo ambao umetawala kwenye vichwa vya wanawake wengi mno "mme wa mtu anajua kulea........mme wa mtu anajua kuhonga...... ".

Huu mtego umewanasa wanawake wengi mno leo hii wamekuwa masingle mama,sababu tu tamaa ya fedha.
Wapuuzi hao..unazaa mwishowe mtoto anafichwa km ARVs ht ndugu hawamjui ni wapuuzi yaani wanawake baadhi ni wabinafsi mnoo,anaangalia starehe na status but we don't check our kids happiness anapowafahamu ndugu zake kwa baba Bora kuwa single mama kuliko kuzaa na Mme wa mtu
 
Wanahimarisha sana ndoa hao, maana ukikosa kupata huduma nyumbani unalala tu kwa amani kesho yake unaita mchepuko unapungiza uzito maisha yanasonga
Nafasi ya mchepuko katika jamii[emoji23]
 
Wapuuzi hao..unazaa mwishowe mtoto anafichwa km ARVs ht ndugu hawamjui ni wapuuzi yaani wanawake baadhi ni wabinafsi mnoo,anaangalia starehe na status but we don't check our kids happiness anapowafahamu ndugu zake kwa baba Bora kuwa single mama kuliko kuzaa na Mme wa mtu
Sure thing [emoji1666]
 
Hii habari yako iko wazi inamhusu huyo huyo mdada na huyu mtoto sio kwanza kwake. Na huyo sio dada yako umezuga. Dr.criminal mmmmhhhh kuna ishara hapa
Mpuuzi huyo dada good enough alishakuambia hataki mtoto,shida ya visichana vya siku hizi kupenda maisha mazuri wasiyoyatengeneza,kakuambia hataki mtoto mle Bata tu..how dare kakabeba mimba?afu unaazaje na Mme wa mtu?
Wajinga tu muache ale jeuri yake,Mnaosoma mniwie radhi km ntakua nimewagusa Ila hata Binti yangu akizaa na Mme wa mtu ntamshangaa Sana aseehh
 
Exactly,,me kwenye kupiga nae story nikamuuliza kwann ulitoka na mme wa mtu wakati vijana kibao tu wanakuitaji,, akanijibu"Mme wa mtu anamwaga Salio,hawazi mara mbili".
Mme wa mtu kula gud time,meza P 2 sepaaa..kuzaa akazae na mkewe ,baasii
 
Kiukweli Mimi siombei yanikute......maana hiyo ni kama ajali Tu.....lakini ikitokea nikampa mimba binti WA watu sikatai hata kama Nina mke sema tutaingia makubaliano maalumu jinsi ya kuishi Ila sitaki kero Kwa mke WA ndoa....maana Yule ndio mwenye haki zote........sema mchepu sitoutupa maana mimba akujipa MWENYEWE as long as mtoto amezaliwa na DNA check iko poa..........hapo itakuwa hamna jinsi......
 
mtu anakuambia usimletee habari za mimba, mean kwamba hana malengo na wewe na still bado unaenda kumpanulia miguu[emoji848]

Dah! nikiitwa mwanamke napigana, na nitapiga mtu sio kwa sababu sipendi hiyo jinsia ila tu sipendezwi na akili zao.
Mwisho umekosea mnoo kumbuka umezaliwa na mwanamke
 
Back
Top Bottom