Notorious thug
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 2,817
- 10,667
Songea. Helena Mchauru (40) Mkazi wa Mabatini Tunduru anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kumkata mumewe korodani ya kushoto akiwa usingizini.
Akizungumza na Mwananchi kamanada wa polisi mkoa wa Ruvuma, ACP Joseph Konyo alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwezi uliopita majira ya saa kumi na moja na nusu jioni katika eneo la mtaa wa Mabatini wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakati Vintan Luiva (42) akiwa amelala na mkewe nyumbani kwao alijeruhiwa kwa kukatwa na wembe kwenye korodani ya kushoto.
Kamanda Konyo alisema, Mtuhumiwa anadaiwa kumvizia Mumewe akiwa amelala ndipo alipomjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri na hivyo kumsabishia maumivu makali.
Alifafanua zaidi kuwa, Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa polisi kukamilika.
Aidha,kamanda Konyo amewaasa wanafamilia ambao wanamigogoro ya kifamili kuripoti katika madawati ya jinsia na watoto pia wawashirikishe watu wao wa karibu, Wenyeviti wa mitaa na viongozi wa dini ili kuweza kusuluhishwa migogoro kwani wanapofumbia macho migogoro hiyo wanaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo.
Chanzo: Mwananchi