Amkata mumewe korodani ya kushoto akiwa usingizini

Amkata mumewe korodani ya kushoto akiwa usingizini

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667
Songea. Helena Mchauru (40) Mkazi wa Mabatini Tunduru anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kumkata mumewe korodani ya kushoto akiwa usingizini.

Akizungumza na Mwananchi kamanada wa polisi mkoa wa Ruvuma, ACP Joseph Konyo alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwezi uliopita majira ya saa kumi na moja na nusu jioni katika eneo la mtaa wa Mabatini wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakati Vintan Luiva (42) akiwa amelala na mkewe nyumbani kwao alijeruhiwa kwa kukatwa na wembe kwenye korodani ya kushoto.

Kamanda Konyo alisema, Mtuhumiwa anadaiwa kumvizia Mumewe akiwa amelala ndipo alipomjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri na hivyo kumsabishia maumivu makali.

Alifafanua zaidi kuwa, Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa polisi kukamilika.

Aidha,kamanda Konyo amewaasa wanafamilia ambao wanamigogoro ya kifamili kuripoti katika madawati ya jinsia na watoto pia wawashirikishe watu wao wa karibu, Wenyeviti wa mitaa na viongozi wa dini ili kuweza kusuluhishwa migogoro kwani wanapofumbia macho migogoro hiyo wanaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo.

Chanzo: Mwananchi
 
Inaonekana mwanamke alikuwa anajua mumewe korodani yake inatumika kwa mke mwingine, ikabidi aikate, ila mambo ya mahusiano magumu sana hasa ukutane na mwenza au mpenzi mpumbavu, ukishakaa na mpenzi mpumbavu awe wa kiume au kike piga chini haraka sana, la sivyo utabakia kufukuzana na mtu maisha yako yote.
 
Dunia ya Leo kuishi na mwanamke chumba kimoja ni Sawa na kukumbatia mtungi wa gesi unaovuja huku jiko linawaka.

90% ya vurugu za hapa duniani zinasababishwa na mwanamke.
Wacha bwana!!!
 
Katika kipindi hiki cha Mwisho wa Dunia,Ndoa Si salama tena.
Hata uwe mwangalifu vipi bado utachuma janga tu ndoani.
 
Sidhani kama inasaidia Mkuu.

Sababu kama mtu akiamua kukudhuru sehemu zipo nyingi tu mbali na huko utakakokuvisha kufuli.
Inasaidia,Mwanamke wa siku hizi anawaza kudhuru Mashine tu maana ndio ana kesi nayo,mpaka sasa ndani ya week tatu kesi zinazoripotiwa ni mashine kuumizwa
Ka mashine kenyewe kibamia nikikatwa nibaki sina kitu
 
Back
Top Bottom