Amos Makalla ametudhalilisha na kututukanisha wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla

Zama za upigaji ndio hizi yaani kama atakuwepo kiongozi akashindwa kupiga pesa au kujengea malaya/mchepuko wake awamu hii basi hatafanya tena hadi atakapofukiwa ardhini.
Yaani anakodi ndege na kuchukua chake % kwa ziara asiyo na kichwa wala tumbo.
 
Mkuu mimi hakuna kitu ninachochukia kama uchafu. Laiti wana Dar es salaam wangekuwa wanauchukia uchafu kama niuchukiavyo basi mji wetu ungekuwa ni zaidi ya Brussels achilia mbali Kigali nk.
Inawezekana Makala anatamani dar iwe kama Moshi,kigali au Brussel ila wadanganyike hawajataka kumuelewa ameamua kuwapeleka darasani wachafuzi wa mji,tena kwa kuwapatia hamasa kubwa,hivyo ni vyema ukamhukumu baada ya kupima ufanisi wa wazo lake,mpe muda,ili umhukumu kijani mwenzio kwa haki🤔 .Ila usiache kufuatilia kwa karibu ufanisi wa uwekezaji wake na wazo lake,kama upigaji utajua tu🤔
 
NGoja watu wale trip, next...mama ntilie, wauza matunda etc
 
Hiyo hela bora ingeongeza nguvu kwenye kuzibua mitaro,kununulia gari la takataka au kupiga sakafu baadhi ya masoko ambayo kipindi cha mvua uwa yanajaa matope ukiyaangalia uwa kama mabwawa ya kinyesi
Natamani apite hapa aone ushauri mzuri uliompa.
 
Ya kama ulivyoandika kuwa inawezekana yeye ana nia ya dhati ila sasa aliowapeleka ndo watakaomuangusha. Ndomaana sisi tumeanza kulalamika mapema maana tunajua fedha nyingi zitatumika lakin mwisho wa siku hakuna kitakachowabadilisha aliowapeleka.
 
Zama za upigaji ndio hizi yaani kama atakuwepo kiongozi akashindwa kupiga pesa au kujengea malaya/mchepuko wake awamu hii basi hatafanya tena hadi atakapofukiwa ardhini.
Yaani anakodi ndege na kuchukua chake % kwa ziara asiyo na kichwa wala tumbo.
Jamaa kaiona fursa kaamua kuitengenezea mazingira ya kuchakachua mapema.
 
Wacha waisome namba see! Ccm mbele kwa mbele
 
Umeandika kwa uchungu sanaa. wewe ni mzalendo... Lkn viongozi wetu wengi wanafanya mambo ya ovyo sanaa mkuu..
Izo hela zingefanya mambo mengine ya msingii
 
Acha ushamba kwani watu wa Dar si watanzania na wana nini cha mno zaidi?
 
wapi nimesema hawajakwea pipa?nilichopinga ni kuwa hawajakodishiwa ndege bali wametumia ndege ya abiria tu kama wengine.
Hizo pia ni gharama kutokana na ukubwa wa bei ya ticket ya Go and Return. Fikiria kama wamekwenda watu 50 ni kiasi gani cha nauli kimetumika. Hapo bado chakula, hotel, malazi nk.
 
Umeandika kwa uchungu sanaa. wewe ni mzalendo... Lkn viongozi wetu wengi wanafanya mambo ya ovyo sanaa mkuu..
Izo hela zingefanya mambo mengine ya msingii
Kweli mkuu, hizo pesa zingetumika kwa ajili ya mambo mengine ya msingi kuliko kuzichoma katika mambo ya hovyo na yasiokuwa na tija kama hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…