Ndugu zangu Watanzania,
CCM Ni Chama ambacho huwezi ukakitabilia juu ya maamuzi yake,ni chama ambacho kinakwenda na mahitaji ya wakati ,ni chama ambacho kinawapa watanzania Radha tofauti tofauti.hii ndio sababu hakikauki midomoni mwao Watanzania wala kupungua upendo mioyoni mwa watanzania wala kushuka ushawishi wake kwa watanzania.
Sasa leo kimemteua mwana Dada maarufu na mahili na aliyeisomea siasa darasani Mheshimiwa Jokate Mwegelo kuwa katibu mkuu wa UVCCM ,ambapo unaweza kusema ni Nguli wa sayansi ya siasa kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam mahali alipopikwa akapikika.
Jokate anaifahamu vyema sana UVCCM kwani huko ndiko alikotokea ,unaweza kusema maji yamerejea katika mkondo wake na asili yake. Sasa jumuiya inakwenda kuwaka moto na kutikisa hapa nchini,hii ndio nguzo ya chama,ni tanuri la kuwapika viongozi wa kesho serikalini na ndani ya chama. Nilishamtabiria humu jukwaani jokate kuwa atafika mbali sana na kwamba mwakani lazima aingie mjengoni.Hongera sana Mheshimiwa Jokate kwa uteuzi huo.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.