Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
-
- #41
Mkuu KANYIMBI , asante sana kwa hii, huu ndio ukweli wa jirani ni nani, na sasa mtashangaa jinsi Taifa litakavyo barikiwa.Tafsiri ya neno Jirani 'ni mtu yeyote ambaye shughuli zako zinamuhusu'. Anaweza akawa Mkeo/ Mumeo, Mtoto wako, Mfanyakazi mwenzako, Mteja wako, Muumini mwenzio, Ndugu yako au mtu anayeishi karibu na wewe.
Hivyo ukifanikiwa kuwapenda hao, Mungu anakubariki.
Tumefunzwa adui mpende, mafisadi tuwapende ili reciprocity ya upendo, watajikuta wameacha ufisadi!.Nchi inayotafunwa na mafisadi yasiyojali utu, unaanzaje kuipenda?
Nimekuelewa Mkuu[emoji120][emoji120][emoji120]Mkuu Vmatongo , nakuomba unitendee haki!, it depends mtu unaandika kwa motives gani, kama unaandika kwa motives za uchawa ili uonekane uteuliwe, then utakuwa sawa kumwambia mtu wa namna hiyo kuwa ana bahati mbaya hawamuoni, lakini kama unaandikia kuhudumia jamii na sio kufuruhisha watawala, wewe utaendelea kuandika kuhudumia jamii kwa kuwa a critical writer, wala hutategemea watawala wakuone!. Hili mimi nimeliweka wazi kabisa kuwa siandiki ili watawala wanione! Je, wajua Sio Kila Kumpongeza, ni Kujikomba/Kusaka Teuzi? Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
P
Mkuu Mtukutu wa Nyaigela , nakuomba usichanganye madesa kati ya Christmas religious celebrations na the Christmas Spirit!. Hili ni bandiko la Christmas Spirit!, ni sikukuu ya wote!.chrismass ni upagani, haiko kibiblia
lakini kwa kuwa mnatii miongozo ya viongozi wenu kuliko kutii neno la Mungu endeleeni nayo
tuendelee kuwafurahisha wafadhili 🤣Mkuu Mtukutu wa Nyaigela , nakuomba usichanganye madesa kati ya Christmas religious celebrations na the Christmas Spirit!. Hili ni bandiko la Christmas Spirit!, ni sikukuu ya wote!.
P
Kama unaamini mimi Pasco Mayalla naandika ili kuwafurahisha wafadhili, endelea kuamini hivyo!.tuendelee kuwafurahisha wafadhili 🤣
Wanabodi,Heri ya Krisimasi, Merry Christmas
Kitaifa baada ya Mungu, nchi ndio jirani yako, tuipende nchi yetu, viongozi wetu ndio jirani zetu, tuwapende viongozi wetu!, wananchi wengine wote ni jirani zetu!, tupendane sisi kwa sisi kwa upendo wa dhati, Viongozi pendaneni na wapendeni wenzenu hata wapinzani!, ukiwa na upendo wa dhati toka moyoni mwako, haiwezekani nyinyi mkakutana na tena vikao vyenu vingine mkavifanyia hata pale patakatifu petu, lakini mkawazuia wenzenu kufanya mikutano!. Tupendane kwa dhati na tusiwatendee wengine hiyana!. Kwenye medani za siasa za vyama, CCM kama chama tawala, jirani zake ni Chadema, ACT Wazalendo, CUF, NCCR etc, wana CCM wanawajibu wa kuwapenda vyama vingine kama wanavyojipenda wenyewe!, haiwezekani wao wawe huru kufanya mikutano, lakini wanawazuia wengine!.
I wish You A Merry Christmas and Prosperous New Year.
Paskali.
Mkuu NAMBA MOJA AJAYE NCHINI , kuna watu walikuwa hawapendani, wenyewe walikuwa wanajifanyia mikutano ya chama chao, tena mingine wanaifanyia hadi pale patakatifu petu, huku wamepiga marufuku wenzao kufanya mikutano ya hadhara na sometimes kuzuia hata mikutano ya ndani, lakini baada ya wito huu wa upendo, moyo wa upendo ukamwingia mtu, akaumwaga upendo kwa kuruhusu mikutano ya siasa kwa wote. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwaPasco
"Kuna watu hawapendani huko"!?
Amulia ugomvi Ndugu!
Mkuu DR HAYA LAND, sisi wengine ni damu ya kunguni, japo sijaishika katiba ya nchi mbele ya fulani, mwaka huu ujao wote wa 2024 nitaishika katiba ya nchi kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku, kupitia kipindi cha TV cha Kwa Maslahi ya Taifa, kuwaelimisha Watanzania kuhusu katiba, sheria na haki.Asante Mkuu
Huu mwaka nakuona mahali ukishikilia katiba ya nchi ukiwa mbele ya mh Fulani
Mkuu Sir robby, kumbe wewe ndio ulikuwa hujui, JPM alikuwa anawazimia kichizi Makamanda, ndio maana akawasomba Makamanda kibao wakahamia Chadema. Huo ni Upendo mkubwa.AMRI NGUMU sana HIYO Mwendazake alishindwa kabisa kuwapenda KABISA CHADEMA[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mungu anampenda sana tuu shetani ndio maana yupo mpaka kesho!. Ndiye aliyemuumba, na kabla shetani hajafanya lolote, huomba kibali kwa Mungu, akikubaliwa ndipo anafanya ushetani wake!. Sisi Wakristu hili tumelisoma kwa Ayubu, pia Bwana wetu Yesu Kristo alijaribiwa na shetani.Hivi Mungu anampenda shetani!!!?
Yes wanatupenda sana tuu, na utashuhudia 2025!.WAO WANATUPENDA, WANAIPENDA NCHI, TUANZIE HAPA.
Anza na No. 1, endelea...Paskali ni vyema ungetuwekea na reference za hao viongoz wanaotupenda na kuipenda Tanzania kiuzalendo!!
Merry ChristmasNgoja nipite tu.
Asante, Merry ChristmasJamani mkuu pascal ametoa maoni yake tu.............upendo
Naunga mkono hoja, No. 1 kaonyesha mfano kwa kukaa nao mezani na wakakubaliana kugawana mkate, pasu kwa pasu, kila mtu kupata nusu mkate.Tuwapende wapinzani pia, tusiwachukie.
Kwa mafundisho ya dini ya Kikristu, tuliyopewa na huyu Masiya aliyezaliwa leo, Bwana wetu Yesu Kristu, aliulizwa amri kuu kuliko zote ni amri gani?,
Pascal Mayalla nimekuelewa vizuri nakubaliana nawe 80% ila kamwe sitakubaliana nawe juu ya kuwapenda viongozi hawa wanatuibia, na kutufanya wajinga miaka nenda rudi mpaka wanafikia kutaka kuitumbukiza nchi kwenye tawala za kigeni kwa kutumia rasilimali zetu.Yesu Akajibu: ‘Mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ni kubwa na ya kwanza ya amri. Na ya pili inafanana na hii: Mpende jirani yako kama nafsi yako", na mimi naomba kuiongeza kidogo, upendo huo uwe ni upendo wa kweli na upendo wa dhati, Mpende Mungu, Ipende Nchi, Wapende Viongozi, Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako!. Akaulizwa tena Jirani yako ni Nani?, ilifuata story, nami nakuuliza wewe jee unampenda jirani yako?.
Sio kila ninachoandika ni kutoka vitabuni na kwenye maandiko, vitu vingine ni vya kwangu tuu mwenyewe.Hiyo amri ya kuwapenda viongozi wako itakuwa ni bibilia iliyotungwa na CCM na siyo bibilia takatifu
Mkuu Faana , kuna wengi hawajui, love will conquer all!, ukiwapenda hao viongozi wanaotuibia, na kutufanya wajinga miaka nenda, miaka rudi mpaka wanafikia kutaka kuitumbukiza nchi kwenye tawala za kigeni kwa kutumia rasilimali zetu, wanayafanya hayo kwa ukosefu wa upendo, hivyo ukiwapenda, watapata upendo na kuacha hivyo vitendo vyao!.Pascal Mayalla nimekuelewa vizuri nakubaliana nawe 80 ila kamwe sitakubaliana nawe juu ya kuwapenda viongozi hawa wanatuibia, na kutufanya wajinga miaka nenda rudi mpaka wanafikia kutaka kuitumbukiza nchi kwenye tawala za kigeni kwa kutumia rasilimali zetu.