Amri Kuu Kuliko Zote ni Upendo! Mpende Mungu, Ipende Nchi, Wapende Viongozi, Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako!. Jirani yako ni Nani?, Unampenda?

Tafsiri ya neno Jirani 'ni mtu yeyote ambaye shughuli zako zinamuhusu'. Anaweza akawa Mkeo/ Mumeo, Mtoto wako, Mfanyakazi mwenzako, Mteja wako, Muumini mwenzio, Ndugu yako au mtu anayeishi karibu na wewe.

Hivyo ukifanikiwa kuwapenda hao, Mungu anakubariki.
 
Hivi Mungu anampenda shetani!!!?
Yes, adui mpende!, Mungu ana... sana shetani, ndio maana baada ya uasi hakumuangamiza, akamuacha aitendelee kupoteza watu wa Mungu!.

Baada ya Mungu kumuumba Eva, alimuona shetani aki mtempt Eva, akamuacha!, shetani akamtempt Eve, akamuonyesha tunda, akamfundisha jinsi ya kumega tunda, akammegea, Eva akamfundisha Adamu jinsi tunda linavyomegwa na kumlazimisha kumega!.

Mungu akamtuma Mwanae mpendwa wake, Shetani aka m tempt na hadi kumsulubisha huku Mungu anaangalia tuu!.

Sababu pekee ya ni kwanini Mungu hajamdetroy shetani, jibu utalipata
P
 
Pascal Mayalla kwa nini kupotosha maandiko…wapi imesema tuwapende watawala wewe wasema viongozi… wapende wewe usitulazimishe
Wao wanawapenda wananchi acha kutufanya hatunazo….
 
Kitaifa baada ya Mungu, nchi ndio jirani yako, tuipende nchi yetu, viongozi wetu ndio jirani zetu, tuwapende viongozi wetu!, wananchi wengine wote ni jirani zetu!, tupendane sisi kwa sisi kwa upendo wa dhati, Viongozi pendaneni na wapendeni wenzenu hata wapinzani!,
Viongozi wenyewe wa kuwapenda ni hawa waliotuacha mifupa nje!!!!
 
Viongozi pendaneni na wapendeni wenzenu hata wapinzani!, ukiwa na upendo wa dhati toka moyoni mwako, haiwezekani nyinyi mkakutana na tena vikao vyenu vingine mkavifanyia hata pale patakatifu petu, lakini mkawazuia wenzenu kufanya mikutano!. Tupendane kwa dhati na tusiwatendee wengine hiyana!. Kwenye medani za siasa za vyama, CCM kama chama tawala, jirani zake ni Chadema, ACT Wazalendo, CUF, NCCR etc, wana CCM wanawajibu wa kuwapenda vyama vingine kama wanavyojipenda wenyewe!, haiwezekani wao wawe huru kufanya mikutano, lakini wanawazuia wengine!.
Kuna vitu watu tunaandika humu, vinaonekana kama tumeandika nothing!. Makala hiyo inayozungumzia upendo imefika gazetini siku ya Krisimasi. Kuna mtu alisoma hiyo paragraph ikamuingia!.

Baada ya Krisimasi angalia kilitokea nini Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote

Hivyo we are not writing for nothing!.
We are writing for something.
P
 
Pascal Mayalla kwa nini kupotosha maandiko…wapi imesema tuwapende watawala wewe wasema viongozi… wapende wewe usitulazimishe
Wao wanawapenda wananchi acha kutufanya hatunazo….
Mkuu Pakawa sijapotosha, amri inasema mpende na jirani yako kama nafsi yako!, nikauliza jirani yako ni nani?.
  1. Hapo ndani ya nyumba unapoishi, jirani yako ni mtu wa chumba cha next room, hata kama ni beki 3, ale unachokula wewe, avae unachovaa wewe na wanao.
  2. Kama ni nyumba ya kupanga, jirani yako ni next door.
  3. Kwenye utawala wa nchi, jirani yako ni viongozi wako wa nchi.
  4. Kwenye vyama vya siasa, jirani wa CCM ni opposition. Baada ya hii makala kutoka, imetenda!. Kumefanyika tendo la upendo chama.
P
 
View attachment 2473335View attachment 2473336
Heri ya Krisimasi, Merry Christmas
Sikukuu ya Krisimasi kwa mwaka huu imedondokea siku nzuri ya Jumapili! Hii ni Makala ya Jumapili ya Krismasi.

Kwa mafundisho ya dini ya Kikristu, tuliyopewa na huyu Masiya aliyezaliwa leo, Bwana wetu Yesu Kristu, aliulizwa amri kuu kuliko zote ni amri gani?,
Yesu Akajibu: ‘Mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ni kubwa na ya kwanza ya amri. Na ya pili inafanana na hii: Mpende jirani yako kama nafsi yako", na mimi naomba kuiongeza kidogo, upendo huo uwe ni upendo wa kweli na upendo wa dhati, Mpende Mungu, Ipende Nchi, Wapende Viongozi, Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako!. Akaulizwa tena Jirani yako ni Nani?, ilifuata story, nami nakuuliza wewe jee unampenda jirani yako?.

Japo Krisimasi nisikukuu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Masiha, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa sisi Wakristu, lakini sikukuu hii inaadhimishwa dunia nzima na watu wa dini zote na mataifa yote, hata nchi za Kiislam, kwa kitu kinachoitwa (Chirstmas Spirit" is Giving), yaani dhima ya Krismasi ni kutoa, kujitoa, kukipelekea zawadi kichanga kilichozaliwa leo, lakini kwenye maisha yetu, sio lazima kuwepo kichanga kilichozaliwa leo, hivyo hiyo spirit ni ya kutoa kwa waliotuzungungukam ukianzia kwenye familia yako, majirani waliokuzungunguka, ndipo twende kwa nduga, jamaa na marafiki hadi kwa wazazi wetu vijijini. Ni sikukuu ya kutoa na sio sikukuu ya kupokea.

Tena ukitoa, toa kwa wote bila kujali ni dini gani, maana Krismasi ni sikukuu ya wote, maana hata kwenye dini ya Kiislamu, wanamtambua Masiya, Bwana wetu Yesu Kristo, kama Nabii Issa Bin Maryam, ukisoma sifa za huyo Nabii Issa bin Maryam, utakubalia na mimi mtu huyo ni Yesu Kristo, ila kwa vile kila dini iko huru kuamini imani yake, kuna dini zinamkubali Yesu ndiye Nabii Issa, hivyo kuzaliwa kwake kunasherehekewa dunia nzima, ni sikukuu ya wote.

Hata simulizi za mwanzo wa ulimwengu kwa dini kuu mbili za Wakristo na Waislamu, sote tunakubaliana dunia iliumbwa na Mungu, mwanzo Mungu aliwaumba Adam na Eva, (Kikristu) au Adam na Hawa, (Kiislamu) hivyo sisi binadamu wote ni watoto wa baba mmoja. Adam, hata neno Mwanadamu, au Binadamu, maana yake ni Mwana wa Adamu au Bin Adam. Hata sisi nembo yetu ya Taifa yenye mwanamke na mwanaume, Bibi na Bwana, wale ni wazazi wetu, Adam na Hawa.

Kwa dini zote mbili kuu duniani, Wakristo na Waislamu, tunaamini kisa cha Nabii Abraham (Kikristo) Ibrahimu, (Kiislamu) na mkewe Sara (Kikristu), Sarai (Kiislamu), waliishi muda mrefu kwenye ndoa yao bila kubahatika kupata mtoto. Baada ya uzee kuwanyemelea na mkewe Sara siku zake kukoma, hivyo kutokuwa na uwezo tena wa kuzaa mtoto, ndipo akamtoa mjakazi wake wa Kimisri, Hagai (Kikiristu), Hagir (Kiislamu), kushiriki na mumuwe Ibrahim, ili kuweza kupata mrithi.

Somo hapa ni familia ambazo hazikujaaliwa kupata watoto kutokana na tatizo la uzazi kwa mwanamke, wanawake msiwe wachoyo wa waume zenu kupata watoto!, ukijikuta wewe ni mwanamke, na unamatatizo ya uzazi, huwezi kushika ujauzito na kuzaa mtoto, waruhusuni waume zenu kupata watoto kwa wanawake wengine!. Huu ndio upendo wa dhati!. Hii ni endapo tatizo la uzazi ni kwa mwanamke, linapokuwa tatizo ni kwa mwanaume, hili mtanisamehe bado sijajua utaratibu wake, kwasababu hata kwenye vitabu vya dini, haijasemwa.

Huyo mjakazi akashika ujauzito, akamzaa mwana wa kwanza wa Ibrahimu akaitwa Ishamel (Kikirstu) Ismail (Kiislamu), aliyemzaa na huyo mjakazi wake wa Kimisri Hagai (Kikiristu), Hagir (Kiislamu). Familia nzima ilifurahi kupata mtoto, Baba, mama na mjakazi.

Baadaye kwa muujiza wa Mungu, mke wa Ibrahimu Sara, akiwa mzee wa umri wa miaka 80, alishika ujauzito, na kumzaa mtoto aliyeitwa Isaka (Kikristu), Isihaka (Kiislamu). Isumaili ndio Baba wa Waislamu wote, na Isaka ndio baba wa Wakisto wote. Hivyo Wakristu na Waislamu ni watoto wa Baba Mmoja Nabii Ibrahim.

Ni katika ukoo huu ndio alikuja kuzaliwa Nabii Musa, na aliyewakomboa Wairaeli kutoka utumwani Misri, nan die aliyepewa Amri Kuu za Mungu, ni zile zile amri alizopewa Musa, kupitia Torati, na hata Yesu alipokuja, bado amri za Mungu ni zile zile za Musa, Yesu hakuja kuitengua Torati bali alikuja kuikamilisha, hivyo Wakristu na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, tusherekee Krismasi pamoja.

Kwa vile Krismasi ni sikukuu ya kizungu, wenzetu wazungu wanaishehekea kwa kitu kinachoitwa “The Christmas Spirit” ambacho ni kusherehekea by “Giving” and not “Receiving”, kumaanisha Chrismasi ni sikukuu ya kutoa, na sio kupokea.

Kuna Watanzania wengi wanajiandaa kwa mwaka mzima, ikiwemo kuweka akiba ya fedha za kutumia kula Krismasi, na mwaka mpya, wanajikuta wanaisherehekea kinyume cha malengo, badala ya kutoa, wao ndio kwanza wanatumia kwa kujipenda, kufanya matumizi makubwa na sherehe, kula, kunywa, kusafiri, kustarehe, kununua vitu na kujipa zawadi wenyewe badala ya kuwapa zawadi wengine haswa wahitaji!.

Amri kuu kuliko zote ni upendo, ukimpenda mtu kwa dhati, utamkia heri, fanaka na mafanikio, natoa wito kwa sisi Watanzania, baada ya kumpenda Mungu, ni kumpenda jirani yako kama nafsi yako!, jirani yako ni nani?.

Kitaifa baada ya Mungu, nchi ndio jirani yako, tuipende nchi yetu, viongozi wetu ndio jirani zetu, tuwapende viongozi wetu!, wananchi wengine wote ni jirani zetu!, tupendane sisi kwa sisi kwa upendo wa dhati, Viongozi pendaneni na wapendeni wenzenu hata wapinzani!, ukiwa na upendo wa dhati toka moyoni mwako, haiwezekani nyinyi mkakutana na tena vikao vyenu vingine mkavifanyia hata pale patakatifu petu, lakini mkawazuia wenzenu kufanya mikutano!. Tupendane kwa dhati na tusiwatendee wengine hiyana!. Kwenye medani za siasa za vyama, CCM kama chama tawala, jirani zake ni Chadema, ACT Wazalendo, CUF, NCCR etc, wana CCM wanawajibu wa kuwapenda vyama vingine kama wanavyojipenda wenyewe!, haiwezekani wao wawe huru kufanya mikutano, lakini wanawazuia wengine!.

Kwa level ya nchi, jirani zetu ni nchi majirani zetu, Watanzania tuwapende Wakenya, Waganda, Wanyarwanda, Warundi, Wakongomani, Wamalawi, Wazambia na Wasumbiji, ndio majirani zetu.

Hebu basi kwa wiki hii, waangazie majirani zako waliokuzungunguka uone ni watu wenye hali gani, wakumbuke wagonjwa mahospitalini, wafungwa magezani, yatima kwenye nyumba za mayatima au watu wengine wowote wenye uhitaji, hebu jitoe uwashike mkono kwa kidogo chochote kitu ili kudumisha “the Christmas Spirit, to give”, kwa kujitoa kwa upendo kuwatolea chochote ili na wao pia washerekee sikukuu ya Krismasi ni sikukuu ya wote.

I wish You A Merry Christmas and Prosperous New Year.

Paskali.
Katika wasukuma wenye bahati mbaya we ni mmojawapo pamoja na kujipindua lakini bado hawakuoni tu! Sijui kwa nini?
 
Mkuu Vmatongo , nakuomba unitendee haki!, it depends mtu unaandika kwa motives gani, kama unaandika kwa motives za uchawa ili uonekane uteuliwe, then utakuwa sawa kumwambia mtu wa namna hiyo kuwa ana bahati mbaya hawamuoni, lakini kama unaandikia kuhudumia jamii na sio kufuruhisha watawala, wewe utaendelea kuandika kuhudumia jamii kwa kuwa a critical writer, wala hutategemea watawala wakuone!. Hili mimi nimeliweka wazi kabisa kuwa siandiki ili watawala wanione! Je, wajua Sio Kila Kumpongeza, ni Kujikomba/Kusaka Teuzi? Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
P
 
Kuna maswali kama haya ya kujiuliza hivi kwanini upendo unakuwa mgumu hivi… shetan na Mungu wanapendana? Maana pia mtaani tunawapenda wema na waovu pia ila ukiwa na upendo ndani yako huwezi kuwa muovu [emoji848][emoji848]
Mkuu denicy, upendo unakuwa mgumu kwasababu ya shetani. Mungu ni upendo na anampenda hadi shetani ndio maana hajamuangamiza!. Ni kweli sio tuu mtaani bali Mungu na shetani both wako ndani yetu!, ukitenda mema shetani anakimbia, ukitenda maovu ni kumkubali shetani, Mungu anakaa pembeni.

Ili kuwa na upendo wa kweli, lazima kwanza upendo huo uwe ndani yetu ndipo tuwapende na wengine. Ukiwa na upendo wa dhati ndani yako huwezi kuwatendea maovu wengine kama enzi zile!. Tanzania Tanzania tushukuru sana kwa huyu mtu Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye? alisamehe tuu.

P.
 
Mimi muumini wa mizimu ya bibi na mababu zangu ngoja nipite tu humu
Hata hiyo mizimu, inatumia the same power source, ikifanya mema ni nguvu za Mungu kupitia mizimu!, na ikifanya mabaya ni nguvu za shetani kupitia mizimu. Zile dini zetu za asili kabla ya ujio wa wazungu na waarabu, Mungu yule ndio huyu huyu! Ila tuu ni kwa majina tofauti tofauti.
P
 
View attachment 2473335View attachment 2473336
Heri ya Krisimasi, Merry Christmas
Sikukuu ya Krisimasi kwa mwaka huu imedondokea siku nzuri ya Jumapili! Hii ni Makala ya Jumapili ya Krismasi.

Kwa mafundisho ya dini ya Kikristu, tuliyopewa na huyu Masiya aliyezaliwa leo, Bwana wetu Yesu Kristu, aliulizwa amri kuu kuliko zote ni amri gani?,
Yesu Akajibu: ‘Mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ni kubwa na ya kwanza ya amri. Na ya pili inafanana na hii: Mpende jirani yako kama nafsi yako", na mimi naomba kuiongeza kidogo, upendo huo uwe ni upendo wa kweli na upendo wa dhati, Mpende Mungu, Ipende Nchi, Wapende Viongozi, Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako!. Akaulizwa tena Jirani yako ni Nani?, ilifuata story, nami nakuuliza wewe jee unampenda jirani yako?.

Japo Krisimasi nisikukuu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Masiha, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa sisi Wakristu, lakini sikukuu hii inaadhimishwa dunia nzima na watu wa dini zote na mataifa yote, hata nchi za Kiislam, kwa kitu kinachoitwa (Chirstmas Spirit" is Giving), yaani dhima ya Krismasi ni kutoa, kujitoa, kukipelekea zawadi kichanga kilichozaliwa leo, lakini kwenye maisha yetu, sio lazima kuwepo kichanga kilichozaliwa leo, hivyo hiyo spirit ni ya kutoa kwa waliotuzungungukam ukianzia kwenye familia yako, majirani waliokuzungunguka, ndipo twende kwa nduga, jamaa na marafiki hadi kwa wazazi wetu vijijini. Ni sikukuu ya kutoa na sio sikukuu ya kupokea.

Tena ukitoa, toa kwa wote bila kujali ni dini gani, maana Krismasi ni sikukuu ya wote, maana hata kwenye dini ya Kiislamu, wanamtambua Masiya, Bwana wetu Yesu Kristo, kama Nabii Issa Bin Maryam, ukisoma sifa za huyo Nabii Issa bin Maryam, utakubalia na mimi mtu huyo ni Yesu Kristo, ila kwa vile kila dini iko huru kuamini imani yake, kuna dini zinamkubali Yesu ndiye Nabii Issa, hivyo kuzaliwa kwake kunasherehekewa dunia nzima, ni sikukuu ya wote.

Hata simulizi za mwanzo wa ulimwengu kwa dini kuu mbili za Wakristo na Waislamu, sote tunakubaliana dunia iliumbwa na Mungu, mwanzo Mungu aliwaumba Adam na Eva, (Kikristu) au Adam na Hawa, (Kiislamu) hivyo sisi binadamu wote ni watoto wa baba mmoja. Adam, hata neno Mwanadamu, au Binadamu, maana yake ni Mwana wa Adamu au Bin Adam. Hata sisi nembo yetu ya Taifa yenye mwanamke na mwanaume, Bibi na Bwana, wale ni wazazi wetu, Adam na Hawa.

Kwa dini zote mbili kuu duniani, Wakristo na Waislamu, tunaamini kisa cha Nabii Abraham (Kikristo) Ibrahimu, (Kiislamu) na mkewe Sara (Kikristu), Sarai (Kiislamu), waliishi muda mrefu kwenye ndoa yao bila kubahatika kupata mtoto. Baada ya uzee kuwanyemelea na mkewe Sara siku zake kukoma, hivyo kutokuwa na uwezo tena wa kuzaa mtoto, ndipo akamtoa mjakazi wake wa Kimisri, Hagai (Kikiristu), Hagir (Kiislamu), kushiriki na mumuwe Ibrahim, ili kuweza kupata mrithi.

Somo hapa ni familia ambazo hazikujaaliwa kupata watoto kutokana na tatizo la uzazi kwa mwanamke, wanawake msiwe wachoyo wa waume zenu kupata watoto!, ukijikuta wewe ni mwanamke, na unamatatizo ya uzazi, huwezi kushika ujauzito na kuzaa mtoto, waruhusuni waume zenu kupata watoto kwa wanawake wengine!. Huu ndio upendo wa dhati!. Hii ni endapo tatizo la uzazi ni kwa mwanamke, linapokuwa tatizo ni kwa mwanaume, hili mtanisamehe bado sijajua utaratibu wake, kwasababu hata kwenye vitabu vya dini, haijasemwa.

Huyo mjakazi akashika ujauzito, akamzaa mwana wa kwanza wa Ibrahimu akaitwa Ishamel (Kikirstu) Ismail (Kiislamu), aliyemzaa na huyo mjakazi wake wa Kimisri Hagai (Kikiristu), Hagir (Kiislamu). Familia nzima ilifurahi kupata mtoto, Baba, mama na mjakazi.

Baadaye kwa muujiza wa Mungu, mke wa Ibrahimu Sara, akiwa mzee wa umri wa miaka 80, alishika ujauzito, na kumzaa mtoto aliyeitwa Isaka (Kikristu), Isihaka (Kiislamu). Isumaili ndio Baba wa Waislamu wote, na Isaka ndio baba wa Wakisto wote. Hivyo Wakristu na Waislamu ni watoto wa Baba Mmoja Nabii Ibrahim.

Ni katika ukoo huu ndio alikuja kuzaliwa Nabii Musa, na aliyewakomboa Wairaeli kutoka utumwani Misri, nan die aliyepewa Amri Kuu za Mungu, ni zile zile amri alizopewa Musa, kupitia Torati, na hata Yesu alipokuja, bado amri za Mungu ni zile zile za Musa, Yesu hakuja kuitengua Torati bali alikuja kuikamilisha, hivyo Wakristu na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, tusherekee Krismasi pamoja.

Kwa vile Krismasi ni sikukuu ya kizungu, wenzetu wazungu wanaishehekea kwa kitu kinachoitwa “The Christmas Spirit” ambacho ni kusherehekea by “Giving” and not “Receiving”, kumaanisha Chrismasi ni sikukuu ya kutoa, na sio kupokea.

Kuna Watanzania wengi wanajiandaa kwa mwaka mzima, ikiwemo kuweka akiba ya fedha za kutumia kula Krismasi, na mwaka mpya, wanajikuta wanaisherehekea kinyume cha malengo, badala ya kutoa, wao ndio kwanza wanatumia kwa kujipenda, kufanya matumizi makubwa na sherehe, kula, kunywa, kusafiri, kustarehe, kununua vitu na kujipa zawadi wenyewe badala ya kuwapa zawadi wengine haswa wahitaji!.

Amri kuu kuliko zote ni upendo, ukimpenda mtu kwa dhati, utamkia heri, fanaka na mafanikio, natoa wito kwa sisi Watanzania, baada ya kumpenda Mungu, ni kumpenda jirani yako kama nafsi yako!, jirani yako ni nani?.

Kitaifa baada ya Mungu, nchi ndio jirani yako, tuipende nchi yetu, viongozi wetu ndio jirani zetu, tuwapende viongozi wetu!, wananchi wengine wote ni jirani zetu!, tupendane sisi kwa sisi kwa upendo wa dhati, Viongozi pendaneni na wapendeni wenzenu hata wapinzani!, ukiwa na upendo wa dhati toka moyoni mwako, haiwezekani nyinyi mkakutana na tena vikao vyenu vingine mkavifanyia hata pale patakatifu petu, lakini mkawazuia wenzenu kufanya mikutano!. Tupendane kwa dhati na tusiwatendee wengine hiyana!. Kwenye medani za siasa za vyama, CCM kama chama tawala, jirani zake ni Chadema, ACT Wazalendo, CUF, NCCR etc, wana CCM wanawajibu wa kuwapenda vyama vingine kama wanavyojipenda wenyewe!, haiwezekani wao wawe huru kufanya mikutano, lakini wanawazuia wengine!.

Kwa level ya nchi, jirani zetu ni nchi majirani zetu, Watanzania tuwapende Wakenya, Waganda, Wanyarwanda, Warundi, Wakongomani, Wamalawi, Wazambia na Wasumbiji, ndio majirani zetu.

Hebu basi kwa wiki hii, waangazie majirani zako waliokuzungunguka uone ni watu wenye hali gani, wakumbuke wagonjwa mahospitalini, wafungwa magezani, yatima kwenye nyumba za mayatima au watu wengine wowote wenye uhitaji, hebu jitoe uwashike mkono kwa kidogo chochote kitu ili kudumisha “the Christmas Spirit, to give”, kwa kujitoa kwa upendo kuwatolea chochote ili na wao pia washerekee sikukuu ya Krismasi ni sikukuu ya wote.

I wish You A Merry Christmas and Prosperous New Year.

Paskali.
chrismass ni upagani, haiko kibiblia
lakini kwa kuwa mnatii miongozo ya viongozi wenu kuliko kutii neno la Mungu endeleeni nayo
 
Back
Top Bottom