Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Joined
Feb 25, 2012
Posts
419
Reaction score
2,169
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.



Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
 
Wewe kwisha habari yako, ulinyanyasa na kuwatesa sana watu, ulijivua ubinadamu, ukajivisha ukatili, ukasahau kuwa cheo ni dhamana. Leo upo kama mbwa koko. Unaishi kwa hofu ya kupoteza ubunge. Pole sana. Ndio ujifunze. Wakati mwingine usiwe limbukeni wa cheo. Waambie na wenzako.

Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndio uje uandike. Kama kawaida nadhani unatamani niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo
 
Huyu ni mroho sana, yuko tayari kufanya lolote baya ili mkono uende kinywani na awapendeze wakubwa zake.
Umetuangusha sana mheshimiwa, ukiwa waziri wa mambo ya ndani kuna mambo ya ajabu sana yalikua yanaendelea hapa nchini, natumaini kuna siku watu wote waliouawa wataipata haki yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuambie ulichowafanyia watu wa Iramba kwenye nafasi yako ya Ubunge, hayo mambo ya skafu hata hayawasaidii watu wa Jimboni kwako.


Swali la kizushi ; Hivi bado una Zile NDOTO zako za kuwania Urais?[emoji23]
URAIS SIO NDOTO ZA MTU BALI NI HITAJI LA WAKATI NA HITAJI LA WATU . HIVYO HII SIO AGENDA KWA SASA. NIULIZE KUHUSU IRAMBA
 
Back
Top Bottom