Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Hatimaye baada ya kimya kirefu, umerudi jukwaani. Hongera kwa hili👏👏👏👏.

Mbona wakati ule ulipokuwa Waziri wa Mambo ya ndani, ulishindwa kuja hapa jukwaani ili utolee maelezo wa nini kilichokuwa kinaendelea kuhusu zile maiti zilizokuwa zinaokotwa kwenye viroba? Shambulio la kinyama la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu? Kupotea kwa akina Ben Saanane, Azory Gwanda? n.k

Ulikuwa wapi Mheshimiwa Mwigulu wakati hayo yote yanatokea tena ukiwa Waziri mwenye dhamana??

Hata Kama mnakula kiapo, ila kuhusu haya nenda kawaombe msamaha waathirika wote wa unyama huu na ukatubu Kanisani🙏
 
Mh.nashukuru kwa kuwa huko humu jukwaani.

Nafikiri ungekuwa unapatikana mara kwa mara ulipokuwa waziri nadhani ungepata maoni ya wadau wengi hapa ambayo yangesaidia kujenga nchi,maana JF watu wanafunguka kuliko sehemu yoyote ile ila kwa sasa ushawishi wako ni mdogo sana katika Serikali tofauti na ulipokuwa Waziri.

Ushauri wangu kwa sasa naomba tujifunze ubinadamu kwa kuridhika kwa kile Mungu alichokupatia hata kama ni kidogo au hata kama hakikutoshelezi muhimu ni afya na uzima.

Mh.umekwisha kuwa Mbunge, Naibu Waziri na Waziri Kamili zaidi ya miaka kumi sasa, hebu kuwa na ubinadamu usiokuwa na uhitaji wa Ph.D. ya UDSM kwa kustaafu siasa na ufanye mambo yako mengine, kwa kuwachia vijana wengine wachanga nao waingie uwanjani wapambane ili utunze heshima yako.
 
Kaka Mwigulu kuhusu kuvaa scaff siyo wote wanamaanisha ni wazalendo. Wengine wanavaa kuwaadaa wakubwa wao. Hivi Kangi Lugola yale mamifuko ya shati ya bendera yote kumbe mwizi tu.
Ukipenda kitu sio lazima imsaidie mtu, kwani unapovaa jezi ya Chelsea au Man u huwa inatusaidia Nini hata UINGEREZA HUJAFIKA. MIMI NAJIVUNIA UTANZANIA WANGU, HIYO BENDERA YA TAIFA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wambie serikali waache kukwepa majukumu yao, haiwezekani wakusanye kodi halafu washindwe kutoa pesa za ujenzi wa shule!

Shule wameachiwa wananchi wachangishane ilihali kodi wanatoa... serikali pesa inazokusanya pesa inapeleka wapi?

Kununua magari ya kifahari? kununua majengo ya wizara? kununua wapinzani? kulipana posho?

Wambie wajiongeze taifa wanaliua kwa kulazimisha raia wachangishane mpaka ujenzi wa vituo vya polisi? kodi wanakusanya ya nini sasa aaaaaah.
 
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.
Mtu senior kama wewe unafungua uzi kwa kutoa ufafanuzi suala la skafu!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah Mwigulu hadi Magufuli a step down uwaziri utausikia kwenye bomba tu

Umeelewa kujipendekeza sio solution ya kila kitu?
Kasome mchezo Bashite anampa nini mzee au kwanini Kangi anafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
UWAZIRI sio agenda ya mtaani. Wewe ndio huwa unateua MAWAZIRI.? MIMI NATIMIZA MAJUKUMU YANGU KAMA MBUNGE NA KAMA KADA WA CHAMA CHANGU
 
Hahahaahah Maxence Melo inabidi utuwekee jukwaa ..la WANAOOMBA UTEUZI kwenye serikali yetu TUKUFU 😎😎😎😎😎🤣🤣🤣.. tupo wengi aisee...likiwekwa, unataja tu mimi Becky nakuomba Magufuli uwaziri wa kupika visheti..yeye anapitia maprofile yetu afu anachagua….hahahaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Huna lolote! Maovu yote uliyowafanyia watanzania damu zao zinakulilia popote ulipo ndiyo maana unawayawaya kama mtetea aliyekosa pakutagia.

By the way lini utapeleka ushahidi wako kule mbinguni kama ulivyosema unao??
Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndii uje uandike. Kama kawaida nadhan unataman niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa kama mchumi na naibu waziri wa zamani fedha, unaonaje uelekeo wa uchumi wa nchi yetu?

Ukiwa kama Mbunge wa Iramba kwa miaka mingi, umewafanyia nini wana Iramba..?

Ukiwa kama Waziri wa zamani, hivi mkikaa kwenye vikao vya baraza la mawaziri mnajadili nini vyenye manufaa kwa watanzania hawa masikini??

Ukiwa kama msomi uliyebahatika kuwa Waziri, upi mchango wako na alama kama msomi uliyoiacha mahara na tunaweza sema hapa hii ni Mwigulu legacy..?

Yale maandishi ya chagua Mwigulu kwenye miundo mbinu yetu kama madaraja na barabara, Je ni wewe ndiye uliandika kwa kutuma vijana? au ni mashabiki wako? Je unajisikiaje kwa uchafuzi ule uliohujumu miundo mbinu na umechukua hatua gani..?

Watoto wako wanasoma International school fedha pale kama sijakosea, Tunaanzaje kupima Uzalendo wako huku watoto millions wa watanzania wanasoma Govt schools..??

Kwanini unaishi Dar es salaam halafu ukawa mbunge wa Iramba??

Nitarudi tena Mh, maswali ni mengi sana..
 
Kwa hiyo Mheshimiwa unaona ulichofanya ni sawa? kwamba wewe ndio Rais 2015, pamoja na kukana kwamba hukuambiwa ufute je huoni huo ni uchafuzi wa mazingira na unapaswa kuwajibika katika hilo....
Sikuwahi kuandika, hata sijui wapi na wapi pameandikwa. Maana ilikuwa kazi ya mashabiki. Tufute tu maana swala la USAFI WA MAZINGIRA NI LETU SOTE
 
Kwa kifupi nimependa jinsi unavyojibu maswali kwa lugha nzuri bila kupanic. Maswali mengi ni ya kejeli na kutia hasira, lakini umeweza kumudu. Hongera sana.

Natamani siku Mzee wa nje ya box nae ajitokeze humu, hakika patawaka. Maana Kigwa bana hanaga swalia mtume, jinsi unavyokuja ndio jinsi anavyo kutawanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuwahi kuandika, hata sijui wapi na wapi pameandikwa. Maana ilikuwa kazi ya mashabiki. Tufute tu maana swala la USAFI WA MAZINGIRA NI LETU SOTE
Kwanini usitoe sehemu ya posho zako za ubunge kugharamia hilo suala la usafi? hamna mtanzania ambaye yupo tiyari kuwajibika kwa upuuzi huo mliofanya na wafuasi wako, hujiulizi mbona wagombea wengine hamna aliyechorwa majina yake kwenye miundombinu ni wewe tu?
 
Back
Top Bottom