Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndii uje uandike. Kama kawaida nadhan unataman niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo
Nimekuelewa sana mheshimiwa, na ni kweli kuwa yule dogo kipenzi cha baba amekuchafulia sana CV yako, ila na wewe ulikubali kumtii mjinga na kwa ujinga wake umedhalilika wewe, pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAONESHA MSISITIZO [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
1.Ule ushahidi wa ugaidi wa Rwakatare uliosema unao na hata mbinguni uko tayari kuutoa ilikuwaje usiutoe hadi kufanya gaidi aendelee kutamba mitaani?

2.Tundu Lissu alishambuliwa wakati wa uongozi wako, lakini hadi unaondoka madarakani hakuna chochote cha maana kilichofanyika zaidi ya danadana za maneno toka kwako na Polisi uliokuwa unawaongoza?

3.Polisi wako wa Dodoma chini ya uongozi wako walisema wana video za tukio zima kupitia CCTV, lakini alivyoingia LUGOLA akasema eneo hilo la makazi ya viongozi hakukuwahi kuwapo na CCTV, nani mkweli kati yenu.

4.Wakati wa uongozi wako kuliasisiwa dhana ya "Wasiojulikana" ambao walitesa Watanzania wengi na wengine kuuawa na kuokotwa fukweni na mitoni wakiwa kwenye viroba, ulipoulizwa ukasema ni wageni lakini ulipobanwa ukakaa kimya, Leo unatwambia nini kuhusu maiti hizi na dhana ya wasiojulikana ambayo ni wazi kwako walijulikana na wanajulikana?

4.Ben Saanane na Azory Gwanda walipotea/walipotezwa wakati wa uongozi wako, na ulihusishwa na upoteaji wao, hebu Leo umejitokeza baada ya kupotea JF kwa muda, ni kwa vipi usihusishwe na upoteaji wao?

5.Uzalendo ni kuipenda nchi, na huwezi kuipenda nchi bila kuwapenda wananchi. Ni vipi uzalendo upimwe kwa kuvaa Scarf yenye rangi za bendera ya Taifa, huku ukifurahia kupotea kwa maisha ya wananchi?

6.Katiba yetu inasema nchi yetu inafuata Demokrasia ya vyama vingi, Je, katazo la mikutano ya kisiasa ulilolisimamia kwa nguvu zako zote linapata uhalali kupitia sheria ipi?
 
URAIS SIO NDOTO ZA MTU BALI NI HITAJI LA WAKATI NA HITAJI LA WATU . HIVYO HII SIO AGENDA KWA SASA. NIULIZE KUHUSU IRAMBA
mbona kauliza hapo ulichowafanyia wanairamba na hujamjibu?

Musiba njia nyeupe...
Jimboni kwako anza kutia maji....
 
Unayazungumziaje haya malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa ajira?

Upi msaada wako kwa wana Iramba na watanzania kama Msomi, Waziri na Mbunge kwenye kutokomeza tatizo la ajira?
 
Unayazungumziaje haya malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa ajira??
Upi msaada wako kwa wana Iramba na watanzania kama Msomi, Waziri na Mbunge kwenye kutokomeza tatizo la ajira??
wewe ni mmoja wa wanao sifia utawala uliofitinika nadhani. Leo nashangaa unamwuliza mwigulu tatizo la ajira jambo ambalo lipo nje ya uwezo wake
 
Unayazungumziaje haya malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa ajira??
Upi msaada wako kwa wana Iramba na watanzania kama Msomi, Waziri na Mbunge kwenye kutokomeza tatizo la ajira??
Yes, HILI NI TATIZO, HII NI HOJA YA MSINGI.

Tar 20 tulikuwa na mjadala mpana SINGIDA, TATIZO HILI LINAWEZA KUPUNGUA KWA KUWEKEZA KWENYE MODERNIZATION OF PRODUCTION PRICESS MIKOANI KWETU, ILI SHUGHULI ZA UZALISHAJI ZITOE FAIDA ZINAZOLIPA HIVYO ZITENGENEZE AJIRA. HIVYO TULIKUWA NA RCC. TULICHAKATA SANA.

BUT AJIRA NI TATIZO NA NI MADA PANA SANA, HAINA JIBU MOJA
 
Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndio uje uandike. Kama kawaida nadhani unatamani niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo
Napenda unavyojibu kwa busara bila panics.

Angekuwa Mzee wa Goli la mkono (Nape) angekuwa amerusha matusi ya kutosha.
 
Back
Top Bottom