Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Vipi Mheshimiwa bado una ndoto ya kuwa RAIS wa Tanzania?
 
Tuambie ulichowafanyia watu wa Iramba kwenye nafasi yako ya Ubunge, hayo mambo ya skafu hata hayawasaidii watu wa Jimboni kwako.

Swali la kizushi ; Hivi bado una Zile NDOTO zako za kuwania Urais?
Kosa lako na wananchi wengi wa Tz wanadhani Mbunge au Diwani kazi yake ni kufanya, au kuleta huduma, inayofanya ni serikali unayoilipa kodi, Mbunge na Diwani wao ni visemeo
 
Yuko wapi Ben mwana wa saa 8? Hakika damu yake itakuwa juu ya kizazi chako.. Wewe ni mzazi, hebu jiweke katika nafasi ya wazazi wa Saanane, wewe ni baba na ni mme hebu jiweke katika nafasi ya familia ya Azory Gwanda.

Hawa watu wamepotea ukiwa wewe una dhamana ya kulinda watu Hawa.

Angalia watoto wako angalia mke, angalia wazazi wako wanafuraha pindi wakuonapo mzima, linganisha na hizo familia mbili, wambieni Hao wazazi, watoto, wake sehemu walipo ndugu zao hata kama wamekufa basi waonyeshe hata mabaki ya miili yao ili wawapumzishe ndugu zao kwa heshimu sehemu inapostahili bila hivyo hakika damu hii itakulilia wewe na kizazi chako..

Husiharibu future ya kizazi chako kwa mambo yasiowahusu.
Tenda uugwana Sema unalofahamu juu ya watu Hawa, vyeo vinapita, Leo umesimama kesho waweza lala chini kwa mateso.. Zingatia Karma.....
 
Mwigulu unaamini usomi sio PHD tu,na je unamini Politics ni moja ya nguzo kuu za ustaarabu wa taifa lolote?

Kama ndvo kwnn chin ya Uongozi wa Wizara yako ya mambo ya ndani Siasa Safi ilififia sana?na watu walipotezwa sana?

Je, unaamini usomi na ustaarabu vilienda pamoja ukiwa Waziri wa usalama wa watu???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unazungumziaje ubora wa shule zetu pale Iramba na kwingineko Tanzania??

Kwanini wanao wasisome pale Iramba au kwenye shule za serikali kama wapiga kura wako wafanyavyo? na wewe kipindi hichi ukiwa mbunge usiishi pale Iramba for more than 60% of your life??
 
Kosa lako na wananchi wengi wa Tz wanadhani Mbunge au Diwani kazi yake ni kufanya, au kuleta huduma, inayofanya ni serikali unayoilipa kodi, Mbunge na Diwani wao ni visemeo
Ingekuwa hivyo tusingekuwa tunauliza maswali maana maeneo mengi yangekuwa sawa kimaendeleo, nikurahisishie kidogo, pamona na yeye kuwa kisemeo ameleta mabadiliko gani? kumbuka hata wabunge wa majimbo mengine nao ni visemeo pia lakini kuna maendeleo yanayoonekana.....
 
Back
Top Bottom