Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Mkuu Mwigulu Nchemba mimi sina swali wala sikulaumu kwa lolote maana wakati mwingine matukio ni nafasi nzuri zaidi ya kujifunzia. Sema tu, nina ushauri kidogo huko uendako (Na ushauri huu uwe ni faida kwa wengine vilevile)

1. Unapopata nafasi ya kuwa kiongozi ni bora kujitahidi kuwa 'fair' hiyo itakusaidia usiwe na cha kupoteza wakati upo kwenye uongozi au hata baada ya kuondoka.

2. Usidhulumu mtu au kuunga mkono dhuluma au uonevu kwa mtu mwingine. Ijapokuwa hii inaweza kuwa ngumu katika mazingira flani kulingana na unaofanya nao kazi, ila ni muhimu kujitahidi kwa kadiri uwezavyo, hiyo itakusaidia kukuweka huru na kukufanya ulale usingizi bila kuota ndoto mbaya.

4. Ni muhimu kujiepusha na kauli za kujikweza na kuwabeza wengine bila Kujali uko kwenye hali gani kwa sababu dunia ina mambo mengi.

5. Kwenye maisha kuna mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa mtu na mengine yapo nje ya uwezo wa mtu, katika mazingira yoyote angalia ulipo na chukua hatua sahihi kusonga mbele bila kuwaza sana ulikopita. Hata hivyo ni vizuri kuzingatia makosa ya nyuma ili mbeleni usiyarudie na uweze kufanya vizuri zaidi.

Kila la heri mkuu.
 
Yes, HILI NI TATIZO, HII NI HOJA YA MSINGI.

Tar 20 tulikuwa na mjadala mpana SINGIDA, TATIZO HILI LINAWEZA KUPUNGUA KWA KUWEKEZA KWENYE MODERNIZATION OF PRODUCTION PRICESS MIKOANI KWETU, ILI SHUGHULI ZA UZALISHAJI ZITOE FAIDA ZINAZOLIPA HIVYO ZITENGENEZE AJIRA. HIVYO TULIKUWA NA RCC. TULICHAKATA SANA.

BUT AJIRA NI TATIZO NA NI MAADA PANA SANA, HAINA JIBU MOJA
Muheshimiwa Mwigulu, hata kama unasema sio kila muda unatumia PhD yako lakini nakushauri jitahidi kufuata kanuni za uandishi.

Hali kadhalika kuhakiki unayoyaandika kabla ya kuyabandika na hata baada ya kuyabandika (ku-post).

Uandishi huakisi mambo mengi ikiwemo umakini wa mtu ktk mambo yake na majukumu kwa ujumla. Pia kupitia uandishi wa mtu waweza kujua kama mwandishi yuko 'organised' au 'disorganised' katika mambo yake.
 
Halafu Mkuu tuambie hivi huu ukwasi ulionao Sasa uliipata kwa posho tu au Kuna lingine!

Ila pole Sana leo umechokoza Moto...na Jumamosi yako imeharibika, nafsi yako itaealilia marehemu na wote uliwatesa au kujua watesi wao!
 
Muheshimiwa Mwigulu, hata kama unasema sio kila muda unatumia PhD yako lakini nakushauri jitahidi kufuata kanuni za uandishi.

Hali kadhalika kuhakiki unayoyaaindika kabla ya kuyabandika na hata baada ya kuyabandika (ku-post).

Uandishi huakisi mambo mengi ikiwemo umakini wa mtu ktk mambo yake na majukumu kwa ujumla. Pia kupitia uandishi wa mtu waweza kujua kama mwandishi yuko 'organised' au 'disorganised' katika mambo yake.
Yani huyu ndie alitaka kuwa Rais wa Watanzania 2015.


Ama kweli maajabu hayawezi kukoma...
 
Mwigulu Nchemba sio siri mkuu nakupenda sana nilikutana na wewe uhamiaji kurasini enzi ukiwa waziri sitakaa nisahau ulivonichangamkia kama ulikuwa unanijua.

Moyoni nilikuwa naomba uje upande wangu niliposimama angalau nikushike tu mkono na hilo nilifanikiwa.

Mkuu nakuombea kila lakheri katika safari yako kisiasa wewe ni kiongozi bora kabisa usivunjike moyo kutokana na maneno ya watu na kuna watu kama sisi tunakupenda sana.
 
URAIS SIO NDOTO ZA MTU BALI NI HITAJI LA WAKATI NA HITAJI LA WATU . HIVYO HII SIO AGENDA KWA SASA. NIULIZE KUHUSU IRAMBA
Unataka kutuaminisha nini kwa yule jamaa anayepayuka kila siku kwenye mimbari kwamba yeye alidipu ila akapigiwa? Ili hali chaguo la watu kwa mwaka 2015 lilijionesha wazi kuanzia ndani ya CCM watu waliimba na nyimbo kabisa kuwa wanaimani na mtu flani.?

Pili, una mpango gani wakuja kufuta yale maandishi yako ya kua Raisi kwenye mawe na kingo za madaraja? Huoni kuwa ni UCHAFU.

Tatu, mpaka unang'olewa kwenye uwaziri wa mambo ya ndani, uliacha suala la upatikanaji wa BW. BEN SANANE umefikia hatua gani.
 
NDIO PANAPO UZIMA
Mh Mwigulu heshima kwako mkuu,

Mimi ni mwananchi na mpiga kura wako. Ninafarijika sana kukuona hapa jukwaani, hakika tulio wengi tuna imani na wewe.

Mh naomba nitumie fursa hii kukukumbusha,mimi ni mshirika wa kanisa la FPCT Kiomboi karibu na idara ya maji mtaa wa lulumba kwa mchj Lazaro Mahewa, tuko kwenye ujenzi au upanuzi wa kanisa na tuliwahi kukutumia barua ya kuomba support yako kama kiongozi wetu, hujaijibu japo uliahidi (kwa mdomo) kutusaidia.

Samahani mh kama nitakuwa nimetumia njia ambayo si sahihi lakini kwangu nimeona ndiyo njia rahisi kukufikia na kukumbusha juu ya hili.

Asante mh, Mungu yuko na wewe.
 
1. Tofauti na utashi wa Rais wa Jamuhuri, wewe kwa mtazamo wako unahisi kwanini ulitumbuliwa?

2. Ebu tueleze kinaga ubaga kipindi ukiwa waziri wa mabo za ndani, kuhusu kupotea kwa Azori Gwanda na Ben Saanane....

3. Ukiwa waziri, Max Melo/Jamiiforums ilishtakiwa. Na kama wewe ni mzalendo, kwanini leo utumie mtandao/mtu mwenye jinai ku socialize..??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa kwa ulichomfanyia Abdul Nondo, sisi watu wa ujiji-kigoma huwa hatuteswi hovyo hovyo. Na huwa hatuna tabia ya kumuachia Mungu ...

Kila siku lazima tukuweke kwenye vitabu vya imani zetu za mababu wa umanyema ili kijana wetu aipate haki yake uliyomnyanganya. Tunaamini haki itapatikana hata Kama Ni baada ya miaka 100 kizazi chako kitakuja kulipa.
 
4DF09513-B15B-4540-B667-62B9F42A4CFD.jpeg
 
Yani huyu ndie alitaka kuwa Rais wa Watanzania 2015.

Ama kweli maajabu hayawezi kukoma...
Kwa hili nitamtetea, ni wangapi hapa JF ambao wanaweza kujitokeza na kujitapa kuwa organized zaidi ya huyu?

Kwa mazingira yetu, hawa angalau ndio wenye afadhali miongoni mwa wengi walalamikaji na walaumuji bila kufanya kitu chochote cha maana kwenye jambo lolote lile.
 
Sio KAWAIDA YANGU KUPANIC, SIKUPANIC KWENYE MITIHANI NIJE NIPANIC KWA SASA[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Kuna kamsemo a problem with political jokes they end up elected.....ni Kama mtu kahack I'd yako mkuu hadi Leo unakua mtu wa kulingishia skafu za bendera na elimu ya ilboru....Kuna sehem Kuna tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom