Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
Mkuu kwanza pole kwa miangaiko ya kila siku na nakushukuru kwa kutupa nafasi ya kukuuliza maswali.

Mimi binafsi sina swali lakini nina ombi.

Nakuomba uchukue nafasi hii kutuomba msamaha wananchi kwa mauaji, utekaji na uhalifu uliotokea kipindi ulicho kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Kumbuka, wizara hii inasimamia usalama wa wananchi.

Natanguliza shukrani.
 
Wachumia tumbo nyie,watu tunauliza atubu Dhambi wewe unaomba sadaka,!
Mkuu samahani kama nimekukwaza, lakini kutoa tu support kujenga nyumba ya Bwana kunamzuiaje mtu kutubu dhambi zake (kama anazo)? Tafadhali hata wasiomjua Mungu wanaweza kutumiwa kujenga ufalme, karibu na wewe mkuu wangu tusaidiane kuujenga ufalme.
 
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
Me nakushukuru kwa kujibu maswali kwa utulivu bila kuhamaki pamoja na kwamba hayawarudhishi wengi, mengine yoooote wanayokutuhumu watanzania wenzao utajijua wewe na Mungu wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
Yale mawe utayafuta lini?
Kuna maandishi mengine bado yapo njia ya Bunju. Umelipia kodi TRA? Kwa sababu tangazo limeshakaa kama miaka sita sasa hivi
 
Mkuu samahani kama nimekukwaza, lakini kutoa tu support kujenga nyumba ya Bwana kunamzuiaje mtu kutubu dhambi zake (kama anazo)? Tafadhali hata wasiomjua Mungu wanaweza kutumiwa kujenga ufalme, karibu na wewe mkuu wangu tusaidiane kuujenga ufalme.
Umenikwaza!...hayo ya sadaka ungeona haya ilhali watu wanajadili matendo yake maovu!
Hivi unamjua au akiwaambia Kilugha tu mnatosheka!

Kwa hiyo nyie hata Shetani akiwaletea sadaka mnachekelea na kuzipokea....!
 
Ni vizuri kukumbuka kisa cha Rais Mwinyi na waziri Natepe alipomfukuza Mwinyi kwenye nyumba ya serikali. Alimpora pia pia vifaa vya ujenzi. Mwinyi akajakuwa rais wa Zanzibar na JMT.

Pengine ni vema kukiri makosa maana kutesa ni kwa zamu na dunia ni mapishano.

Kuvaa skafu si uzalendo hata ni kama tangazo tu tuseme advert... yenye lengo fulani kwa manufaa ya mvaaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF tunafurahi kutuletea Hawa viongozi wetu Ana kwa Ana.

Nashauri mtuletee

KUB Mbowe Ana kwa Ana

Tulia Ackson mbuge mtarajiwa wa Mbeya mjini

Hakina Mdee mbuge asiyetarajiwa Kawe

Kibajaji Livingstone Lusinde

Lukuvi

Mwakyembe

Mh Kippi Warioba

Ally Bananga

Mayor Boniface Jacob

Bila kumsahau Attacked midfield Paul Makonda

Na wengineo Ana kwa Ana tupate kujua uwezo wao wa kutuongoza kwa kuelewa wanachowaza juu ya mustakabali wa nchi yetu na changamoto zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unazungumziaje ubora wa shule zetu pale Iramba na kwingineko Tanzania??

Kwanini wanao wasisome pale Iramba au kwenye shule za serikali kama wapiga kura wako wafanyavyo? na wewe kipindi hichi ukiwa mbunge usiishi pale Iramba for more than 60% of your life??
Wewe jamaa huwa unaunga juhudi kumbe ni kama sisi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikuangalia sikumalizi na najaribu Ku control hasira zangu na nahisi in wengi wako kama Mimi.

Tukio la kushambuliwa Lissu limetokea ukiwa waziri mwenye dhamana na usalama wa ndani lakini hadi unafukuzwa kazi (maana ulifukuzwa huku ukisemangwa kuwa mzururaji) ulikuwa kimya kabisa huku ukijua ukweli.

Lissu alikuwa mbunge mwenzako toka mkoa wa Singida na hata kama itikadi zilitofautiana lakini mlikuwa hadi kwenye RMT mko pamoja hukupata hata siku moja kwenda kumjulia hali mwenzako? Au ndio hiyo inayoitwa guilty conscious inakusumbua kijana wangu? Ulizuiwa na ukakubali usiende? Uhuru wako uko wapi wakujiamulia? Au hukuzuiwa Bali ni roho yako tuu kuwa haina upendo na wengine?

Ona mwenzako Nyalandu! Sizungumzii kujiunga Chadema maana hilo wala halina maana, Bali uamuzi wake wa kwenda kumuona tuu mgonjwa aliyepigwa risasi nyingi ulivyojenga heshima kwake ndani ya mkoa wa Singida.

Hakuna dhambi isiyo sameheka, lakini mpaka mtu aitubu kwanza. Tubu na jutia makosa yako yaliyo umiza watu na heshima yako inaweza kurudi na Mungu akakupandisha pengine zaidi ya pale ulipokuwa. Bila kusahau kusema kweli kile ukijuacho kuhusu madhila yaliyowapata watu ukiwa ofisini.

Mwisho pengine hata balaa la Singida United inaweza isikufie mkononi kwa gundu lako.
Ni ushauri tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hi Post in VITU VINGI, VINGINE KWA SASA MIMI SIO MSEMAJI WA MAMBO HAYO. ILA ANAYEHITAJI KUJUA NINACHOKIJUA ANITAFUTE KWA SIMU NIMFAFANULIE
Ukiwa waziri wa mambo ya ndani Nape Nnauye alitolewa bastola hadharani na askari anayeaminika kutumwa na Paul Makonda na wewe hukuchukua hatua yoyote kinidhamu kwa yule askari. Unazungumziaje pia hili?
 
Back
Top Bottom